Mwenye utaalamu wa zao la korosho tusaidiane

Mandison

Senior Member
Mar 10, 2017
191
109
Habari wana JF. Naomba mwenye uzoefu au utaalamu wa zao la korosho anisaidie kujua mahitaji ya kuanzisha kilimo hiki. Nataka nitafute shamba(virgin land) kwa kilimo hiki, napenda nijue maeneo ambayo zao hili hustawi sana, mbegu bora ya muda mfupi, gharama za kuhudumia hadi kuanza kuvuna ikiwa ni pamoja na madawa, mbolea kama itahitajika na masuala mengineyo.
 
Ninachojua mimi kuhusu korosho ni kwanza Unapanda mstari kwa mstari ni mita 12 na mche kwa mche ni mita 12 hivyo ndani ya eka moja unakuwa na miche kama 27 au 30,
VITU VYA KUZINGATIA
1. Chimba mashimo ya futi mbili upana, futi mbili urefu na futi mbili kimo, ukichimba futi moja kutoka juu udongo wake usichanganye na futi moja iliyobaki, kisha chukua Samadi changanya na udongo wa chini kabisa kisha fukia na upande miche yako.
2. hakikisha unapanda miche wakati wa mvua, au kama kuna maji, yaani hakikisha ukipanda mche usipigwe na jua kwa muda mrefu nila maji kuepo.
3. Baada ya miche kufikia Miezi 4 mpaka 6 unakuwa umekata vizuri kweny ardhi, hivyo weka mbolea ya miti (zinajulikana) hakikisha tuu baada ya kuweka mbolea hiyo kuwe na maji iwe ya mvua ya kumwagilizia.
4. Piga sumu kwa ajili.ya wadudu na Ukungu maana Korosho inaliwa sana na wadudu, na ukicheza hapo utakuta miche yote imekauka.
5. hakikisha unafanya palizi kuzunguka mche wakati wa kiangazi, ili wadudu wasipate makazi na kama kunakuwa na moto usiunguze mche kwa kiasi kikubwa pia fyeka shamba lote wakati wa masika kwa ajili majani yanayoota kwa wingi, masika lima mazao mengine ya muda mfupi ndani ya shamba ili kutoruhusu majani mengi kuota. kama shamba lako ni kubwa sana, ruhusu watu wengine walime ndani ili kusafisha shamba.
6. Korosho za kisasa unavuna baada ya miaka 3 baada ya kupanda, hivyo usafi wa shamba na kupiga dawa kila baada ya miezi 6 ni muhimu zaidi pamoja na mbolea ni vitu vya kuzingatia zaidi. Hii ni pamoja na kupalilia kuzunguka mche na kufyeka kila majani yanapoota
BINAFSI
mimi mwenyewe nimelima Katavi wilaya inaitwa Mpanda. sasa hivi miche ina miaka2 na toka nilipo lima mpaka sasa nimeona vitu vya kuzingatia ni hivyo ila sijajua bado wakati wa uvunaji kama kuna changamoto za aina gani, tutaendelea kujuzana.

P11121-123220.jpg
 
Back
Top Bottom