Mwenye ushahidi wa dhahiri juu ya ufisadi wa Lowassa aweke hapa hadharani! Tuache porojo!

Mkuu wewe unataka nini zaidi ikiwa Lowassa mwenyewe kakubali mbele ya waandishi wa habari akimjibu Manyerere (tazama video yake) amekiri kwa kujisifia kuwa mradi ule ulikuwa safi kabisa na mitambo ilikuwa state of art ulosifiwa na rais wa Marekani wakati hata hilo kadanganya, unataka nini zaidi?. He confessed on record nakala tunayo.

Hizi sio tuhuma ni KASHFA za kiongozi na hakuna mahala alipopinga kwamba hahusiki na zaidi ya hapo alikuwa waziri mkuu alopitisha mkataba ule wapewe nani..Nukuu kibao katika report ya tume unataka nini zaidi? JK sio mjinga wa Kuachia report ile ilopelekwa kwake kwanza aje airuhusu ipelekwe bungeni wakati inamhusu yeye. Jk alijua fika Lowassa kahusika na alimwambia ajiuzuru mapema kabla halijafika mbali. Alitumia uungwana wake leo mnataka kubadilisha na hata kuwatisha familia yake ati mkiingia madarakani watakiona cha moto jamani, jamani kuweni na utu japo kidogo.
 
Lowassa ndiye mtaji kwa CCM kwani ndo mwanasiasa mwenye social capital kubwa kuliko wote kwa sasa. hii ni pamoja na upinzani. Mbowe mwenyewe anathibitisha hilo


Umasikini wa watanzania hauondolewi na social capital nyie punguwani wahed(courtesy of FaizaFoxy ), unaondolewa na sera madhubuti,watanzania wamekaa mkao wa kula kusubiri sera, nyi mnaleta hadithi za paukwa pakawa, matumani yameenda yamerudi.

Sasa kama tunachagua umaarufu kwenda ikulu si tungemchagua Diamond platnumz, maana yeye ni maarufu ndani na nje ya Tanzania.

Tunachagua kiongozi, sio social capital
 
Last edited by a moderator:
Duh Ahahaha! hii kali kushinda tena tumwambie Diamond amrudie Wema ndio itashika moto kabisa itambidi Lowassa naye atoe CD yake ya kibau ukata...
 



1. Nitajie mapungufu matano ya kibinadamu alionayo lowasa kama binadamu

2.Nitajie mapungufu matano ya mheshimiwa lowasa kama kiongozi mapungufu ya kiuongozi....

Tangu 2011 tunaskia sifa zake tuu sasa naomba unijuze mapungufu au Lowasa ni malaika hana kasoro...
 


Naona una undugu na Kinjekitile wa humu Jr maana nae ni kinara wa kukumbatia ufisadi unaonuka harufu mbaya.
 
Naona una undugu na Kinjekitile wa humu Jr maana nae ni kinara wa kukumbatia ufisadi unaonuka harufu mbaya.

Yuko busy anasubili ushahidi ba sisi tunasema tunaomba Mungu apitishwe ba chama chake ndiyo atajua kuwa t unamjua uchafu wake tangy akiwa AICC, alivyoiiba NMC na kuikosakosa GT ili kuiunganisha na Yana kifupi ngoja apitishwe
 
Hivi fedha za kuchukua fomu zinapitia TRA. CCm wekeni EFD kodi ipatikane
 
Mie nadhan mwenye ushahidi na tuhuma hizi AMA maelezo tofauti atakuwa Lowassa mwenyewe,lakini Mbona katika mkutano wa safari ya matumaini hakuchimbua suala hili na kuweka peupe?sasa tunamtaka nani amsemee mambo ya ngoswe tumuachie ngoswe mwenyewe!!!!
 
kinachoendelea hapa ni mwendelezo uleule wa matumizi ya noti kumsafisha lowasa. lakini chombo pekee kinachosafisha watu ni mahakama lowasa kajiuzulu uwaziri mkuu kwa tuhuma ya richmond. je kasafushwa? watanzania tutaendelea kudanganywa mpaka lini nahawa wanasiasa maslahi?
 
Yuko busy anasubili ushahidi ba sisi tunasema tunaomba Mungu apitishwe ba chama chake ndiyo atajua kuwa t unamjua uchafu wake tangy akiwa AICC, alivyoiiba NMC na kuikosakosa GT ili kuiunganisha na Yana kifupi ngoja apitishwe
Badala ya kuweka ushahidi, unazidi kuandika porojo!
 
Hahahahahha hivi ameamka je Leo afya yake Mzee!tusiseme ya ushahidi bila kumjulia Hali Mzee vibaya hivyo hahahaha!!!
 
Mie nadhan Yeyote anayetafuta Urais kwa udi na uvumba maswali ya mtihani wake anajitungia!mwenyewe kwani vigezo vya uongozi vipo wap kwahiyo yeyote na asiye na doa anyooshe suti zake za kuvaa Ikulu maana anaweza Ingia,ila mwenye mawaa pale finyu kwake Kama ngamia kupita kwenye tundu la sindano !tunataka kujenga taifa siyo kumfurahisha Mtu hapa hata ambaye hafai!mtu Kama anampenda Mtu ambaye sauti za wengi za sema anamadudu kiuadilifu basi wewe umpendaye mkapige Naye picha ila si Urais
 
na wewe tuletee ushahidi unaonyesha lowassa amewahi kemea au kuchukizwa na ufidadi
 
Team Lowasa ninajuwa mnatumia udhaifu wa serikali na umasikin wa watanzania kusaka urais, sii kwel mnania ya dhati kuja kutawala taifa hili na hakuna asie mjuwa Rostam Azizi kaz yake ni nini na jins gan serikal fulan imekuwa ikimtumia ili kuweka serikal kwa ajili ya masilah binafsi, Rostam alipandikizwa kwa kikwete na thx God usalama wa taifa na cia+mossad wakamshitukia na ndio ikawa mwisho wake ktk serikal ya kikwete. Sasa itakuwa ni serikal ya mazuzu kumruhusu Lowasa ktk kivul cha Rostam. Hakika dunia itatushanga na mwisho wa yote tusishangae yalio tokea misri yakatokea na Tz. Tujiulize kwa nin egpt inataka kumnyonga Morsi. Ukishajuwa ndipo ujuwe hata Lowasa hawez ikimbia hiyo adhabu. Naiman jeshi kupitia idara za taifa watapindua nchi ili kumuondoa Lowasa jambo ambalo ni hatari.
 
Wewe unataka ushahidi wa aina gani?.

Kujiuzulu tu ni ushahidi tosha weee unataka upi mwingine
 
Mie nadhan mwenye ushahidi na tuhuma hizi AMA maelezo tofauti atakuwa Lowassa mwenyewe,lakini Mbona katika mkutano wa safari ya matumaini hakuchimbua suala hili na kuweka peupe?sasa tunamtaka nani amsemee mambo ya ngoswe tumuachie ngoswe mwenyewe!!!!

Unategemea Lowassa mwenyewe ajitie kitanzini kwa kueleza anavyohusika kwenye kashfa mbalimbali? Lazima azikwepe mfano, ya Richmond amesema tatizo lilikuwa uwaziri mkuu ulioratibiwa na baadhi ya wabunge waliokuwa wanamchukia. Baadae akasema alijiuzulu kwa maslahi ya chama. Sisi hatutaki wanaoweka maslahi ya chama mbele bali maslahi ya taifa.

Waliotuhumiwa na Escrow kuna aliekubali? Kila mmoja alikana kuhusika wengine wakisema fedha hazikuwa za umma, hela za mboga, za kanisa n.k. Kwahiyo mara nyingi huwezi kupata ushahidi credible kutoka kwa mtuhumiwa mwenyewe. Inabidi uje na ushahidi wako utakaoonyesha uongo wa ushahidi wa mtuhumiwa, utakaoonekana ni wa kweli beyond reasonable doubt ndo unatakiwa ukubaliwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…