Attache
Senior Member
- Jul 6, 2012
- 175
- 149
Nimeoa mwanamke wa Tukuyu na hivi sasa tunaishi Tanga ambapo ndio ninafanya kazi na wazazi wa upande wangu wana-reside Tanga pia. Tatizo ni kwamba wakwe wanapenda sana mke wangu awe anarudirudi nyumbani kwao.
Mwaka jana kikazi nilikua Moshi na kipindi cha christmas walikua wanakomalia sana twende au mke wangu aende kusherehekea kule japo kuwa kipindi hicho mke wangu alikua mjamzito wa miezi nane. Ilikua kazi ngumu kuwaelewesha lakini mwishoni wakakubali kishingo upande. Kuna kipindi flania wakakomalia sana twende kwenye ubatizo wa mtoto wa ndugu yao ambapo ikanilazimu niombe ruhusa ya kwenda huko na tukakaa kwa wiki moja.
Sasa mwaka huu mwezi wa tano shirika ninalofanyia kazi liliopen branch Tanga na nikapata uhamisho kuja Tanga na kwa vile tupo karibu sana na wazazi wa upande wangu nikaona ni vyema x mas hii tukasherehekea huku kwa maana haitakua picha nzuri kama tupo huku halafu kwenye sherehe hizi tukachoropoka may be kwa mwakani ndio itaeleweka. Sasa upande wa wakwe kwa juma zima wamekua wakimpigia simu kwamba tuende au yeye aende na yeye ameanza kukubaliana nao. Binafsi sipendelei sana kufanyiwa maamuzi na mtu mwingine na worse still tumeshafanya plan juu ya namna tutakavyo sherehekea huku(Tanga) lakini upande wa pili wale ni wazazi,kukataa kataa pia haileti picha nzuri. Ninawaza niache tu aende japo kuwa wazazi wa huku sidhani kama watafurahia sana kwani ni sherehe yao ya kwanza pia wakiwa na grandson wao na pia tulishaelewana kwamba this holiday tutakua Tanga.
Jambo ambalo sielewi ni kwamba je tatizo lipo kwangu kwamba ninamng'ang'ania sana mke wangu au wao? Ninaomba mchango wenu.