Mwenye shida ni mimi au wakwe zangu?

Mwenye shida ni mimi au wakwe zangu?

Well said King'asti, asnte sana.
Aaah, mie ni mwanamke na wala sikubaliani na hili. Wewe ndo kichwa cha nyumba, na haujaolewa tukuyu bali umeoa. Na uzingatie sio tabia nzuri sana kwa mwanaume kuwa karibu na wakwe zako (actually Paw hawezi kulala kwetu, hata kama ni msiba anaapaswa akalazwe kwa jirani pamoja na mie). Na ni kwa nia nzuri, baba mkwe na mama mkwe wakianza kuzozana ama baba akiamua kumpiga mkeo vibao kwa vile ni mwanae utafanyaje?

Ushauri wangu, muambie mkeo aongee na wazazi. Yeye ana mji wake sasa, mamake nae angekuwa anaendaga kwa baba yake kila xmas inngekuwaje? Pangeni mipango yenu na muitelekeze, kama baba mkwe hana watoto wa kiume mjipange mkiweza pasaka mkawe nao ili wamfaidi mjukuu pia. Kwenda kwenye ubatizo haikuwa mbaya, ni nafasi ya wewe kujuana na ndugu zake pia. Lakini haiwezekani kila xmas ukakae ukweni kaka.
 
Asante, but naomba nitofautiane na wewe hapo uliposema kuwa sina msimamo toka mwanzo, kuna masuala mengine nikiyavaa kwa pupa inawezasababisha mifarakano ambayo ingeweza kuzuilika, but asante
Tatizo unalo wewe! Inaelekea huna msimamo kutokea mwanzo halafu unasema hupendi mtu akuamulie mambo? Waambie unakula sikukuu na mkeo PERIOD kama wana busara wataelewa kuwa wamevuka mipaka na watajirekebisha
 
Asante sana Timtim, tatizo ni kwamba probably wamezoeshwa na wakwe wengine, waume wa dada zake wana tendency ya kwenda huko na wake zao mara kwa mara, binafsi hilo suala ni gumu kwangu.
Tatizo lipo huko ukweni kwako lakini kosa ni la kwako vile ulivyowazoesha ndio wameshazowea. Inakuwaje eti xmas mkeo akale kwao wakati anaacha nyumba yake na mumewe? Funguka wewe mwanaume na hata huyo mkeo mtizame kwa jicho la tatu. Mwanamke anatakiwa awe na mumewe na hakuna vya kuamrishwa. Mbona wao wakwe hawaji kwenu kula ckukuu.
 
Nimekuelewa sana mkuu, nitafanyia kazi uliyoyasema.
Nadhani kuna kosa umeshafanya - umempa uhuru sana mkeo na amejisahau.
1. Wakwe zako huwa wanapanga haya mambo na mkeo kwanza kabla wewe hujapewa taarifa. Huu ni ushenzi ambao unapaswa kukemewa kwa nguvu zote.
2. Mkeo haoni ni vibaya- bado hajahama kwao huyo at least katika mawazo na roho yake.Ukimuuliza anaona kwa wazazi wake ni kwao. Huyo anahitaji sana kuwekewa mipaka
3. Tatizo ni kubwa kuliko haya tunayoyaona. Unapaswa kufunguka na kupima uwezo wake wa kusema UKWELI na kama anakuhusisha kiasi gani katika huo ukweli.
4. Mkeo hana msimamo na anahitaji kuchagua upande atakaoupa kipaumbele
Vingenevyo una kazi!
 
Asante sana Timtim, tatizo ni kwamba probably wamezoeshwa na wakwe wengine, waume wa dada zake wana tendency ya kwenda huko na wake zao mara kwa mara, binafsi hilo suala ni gumu kwangu.

Sababu watu wa tanga ni noma sana. Vichwa vigumu mno, upenda ubwana, ndio maana kila jambo kwao gumu. Kha
 
Sio kuwa nataka kushindana na wakwe, kama ni hivyo ningekataa moja kwa moja, kuna circumstances ambazo wao inapaswa waelewe and mimi viyo hivyo. Inapofika kipindi ambapo wanapush hata sehemu ambapo inkua ngumu hapo ndipo pananipa ugumu na mimi. Nkiwa na familia yangu bado hatujawahi sherehekea na wazazi wangu, na sasa imetokea bahati nipo huku karibu nao, sasa instead of kuwa nao katika kipindi hiki nifungashe tena na kwenda mbali?kwa event ya mwakani walau inaweza kueleweka
kha, Kwaiyo unamaana mke ni chombo cha mwanamme na anaweza kukifanyia anavotaka yeye?
Huyo mwanamke kanunuliwa bei gani? dini zote zinasema kwamba unaweza kuachana na kila mtu lakini huwezi kuachana na wazazi, kwaiyo sikubaliani na wewe umepotoshwa na umekubali kuwa mtumwa wa mwanaume. Siku mume wako hakutaki tena, je utakimbilia wapi? au siku unaumwa kila kitu hapo hapo, unajikojolea na kujinyea unafikiri wakwe zako watazoa mavi yako? au huyo mumeo atazoa amvi yako? Kumbuka baba yako tu au dada zako ndio watakusafisha wewe.

Mie naona wanampa matatizo huyo mwanamke, wanamueka njia panda, hajui wapi aende. maana wazazi wake ni muhim kwake na mume ni muhim kwake.

Kama mume anampenda mkewe basi amsaidie waende japo siku 3 wawafurahishe wazee tu na warudi.
yaonesha huyu jamaa anataka kushindana na wakwe, sio kitu kizuri
 
mwambie mkwe wako na yeye amruhusu mkewe akalie sikukuu kwao. ngoma droo.
 
Funguka tu mkuu, ndio tunaelimishana
inawezekana wazazi wa mke hawajazoea kuwa mtoto sasa hayupo mikononi mwao.

Cha kufanya ni kuamua kama mwanaume, waeleze hamwezi kwenda kuna mipango mlishapanga, nyie mtafute wakati mwingine kama fedha itakuwepo muende

sababu ya pili kwa nini wazazi wa mke wanafanya hivyo naihifadhi maana nitashambuliwa na kuitwa mkabila loh
 
wakati wanamfanyia sendoff,walifikiria nini?napenda sana wazazi wa kisukuma ukishaolewa umeolewa tena wanakuambia ukigombana na mmeo mshitaki kwa wakwezo,na akikuudhi kimbilia kwa wakwe zako.Sasa hao wa tukuyu na wenyewe wanaleta mambo ya ajabu.binti yao nae ana familia yake bado wanamcontrol tu.

kama wakwe zako wamekufa je utakimbilia wapi? Na kama unaishi USA utarudi kijijini cha basukuma wakati unaitajika kazini, pooo
 
Kaza buti Mkuu ili ule sahani moja na wakwe zako. Usiwape nafasi kabisa ya kuendesha nyumba yako kama watakavyo. Waambie wewe ndio mwenye maamuzi ya mwisho kuhusu mkeo na siyo wao ili waache kukubughudhi vinginevyo watakuendesha kama gari bovu na si ajabu kukuvunjia ndoa yako.
 
wewe umeoa, hujaolewa. Kama mwanaume kuwa na sauti katika familia yako, kauli yako iwe ya mwisho(iwe ya maana na kueleweke lakn). Hao ni wanyakyusa wa wapi wa kumtaka mwanao kila wakati ikiwa wanajua ameolewa.
Ninachofahamu wanyakyusa kwa mila zao binti akiolewa haruhusiwi kwenda kwao bila ridhaa ya mumewe. Na wako tayari hata kukufukuza urudi kwako ili kulinda heshima yao kama wazazi.
Cha msingi hapo ni wewe kuonyesha ubaba katika nyumba yako.
 
Hayatuhusu. This is your private life.

sema hayanihusu sio hayatuhusu,umeombwa uchangie?watu wengne sijui mpoje jamani,kwani kilichokuleta kwa hilijukwaa ni nini?watu wengne bna ebu kapshe ukoooo,huna point piga KIMYAAAA
 
Nimeoa mwanamke wa Tukuyu na hivi sasa tunaishi Tanga ambapo ndio ninafanya kazi na wazazi wa upande wangu wana-reside Tanga pia. Tatizo ni kwamba wakwe wanapenda sana mke wangu awe anarudirudi nyumbani kwao.

Mwaka jana kikazi nilikua Moshi na kipindi cha christmas walikua wanakomalia sana twende au mke wangu aende kusherehekea kule japo kuwa kipindi hicho mke wangu alikua mjamzito wa miezi nane. Ilikua kazi ngumu kuwaelewesha lakini mwishoni wakakubali kishingo upande. Kuna kipindi flania wakakomalia sana twende kwenye ubatizo wa mtoto wa ndugu yao ambapo ikanilazimu niombe ruhusa ya kwenda huko na tukakaa kwa wiki moja.

Sasa mwaka huu mwezi wa tano shirika ninalofanyia kazi liliopen branch Tanga na nikapata uhamisho kuja Tanga na kwa vile tupo karibu sana na wazazi wa upande wangu nikaona ni vyema x mas hii tukasherehekea huku kwa maana haitakua picha nzuri kama tupo huku halafu kwenye sherehe hizi tukachoropoka may be kwa mwakani ndio itaeleweka. Sasa upande wa wakwe kwa juma zima wamekua wakimpigia simu kwamba tuende au yeye aende na yeye ameanza kukubaliana nao. Binafsi sipendelei sana kufanyiwa maamuzi na mtu mwingine na worse still tumeshafanya plan juu ya namna tutakavyo sherehekea huku(Tanga) lakini upande wa pili wale ni wazazi,kukataa kataa pia haileti picha nzuri. Ninawaza niache tu aende japo kuwa wazazi wa huku sidhani kama watafurahia sana kwani ni sherehe yao ya kwanza pia wakiwa na grandson wao na pia tulishaelewana kwamba this holiday tutakua Tanga.

Jambo ambalo sielewi ni kwamba je tatizo lipo kwangu kwamba ninamng'ang'ania sana mke wangu au wao? Ninaomba mchango wenu.
mfundishe mwenzio kuto kukubali anayoambiwa na wazaziwake kable hajajadili na wewe. yapo mambo ambayo unatakiwa kuwatii. sioni kwanini hawa wakwezako wawe wanasisitiza safari za mkeo kwenda kwao. mke wako alishatoka kwao ni yeyena wewe. utakuwa hujafanya kosa ukiwa wazi kwao kuwa huu si wakati wa mkeo kusafiri. tena huhutaji kutoa sababu. hapo watatia adabu. huyo ni mkeo na wewe ni mume. wasiwaiingilie.. ingekuwa ni ugonjwa sherehe ... hapo ungesema ni muhimu kwenda. lakini si xmas. kama wanahitaji sana wafunge safari waje kwako xmas
 
Hayatuhusu. This is your private life.

Wewe hata kwa ile thread ya yule dada aliyekuwa anauliza ushaur wa kusafir na mimba ya miez 9..ulimwambia hayatuhusu...so wewe nin kinakuhusu?n why usiseme hayanihusu?hayatuhusu wewe na nan?
 
Mpwa ndoa zina changamoto sana na kila mtu akiweka la kwake hapaaa mmmhh tutakufuru hizi zinazoitwa ndoa takatifu...mwaka jana Mke wangu alikua mjamzito wa miezi nane Mama Mkwe akalazimisha nimsafirishe eti akajifungulie Tanga, nilienda kwa Gyno (sp) akashauri kuwa kwa hali ilivyo asingeruhusu asafiri but Mama alikazania aende hadi last minute nikampeleka hospital akajifungulia hapa hapa Dar, in short ni ngumu sana
 
Kuna kipindi flania wakakomalia sana twende kwenye ubatizo wa mtoto wa ndugu yao ambapo ikanilazimu niombe ruhusa ya kwenda huko na tukakaa kwa wiki moja

ofisi walikuruhusu uende kwenye ubatizo nje ya likizo yako? au ulidanganya kuuguliwa?
hawa wakwe watakuharibia kazi bure, usipowapa msimamo wako wanaweza kukuyumbisha hata kuvunja ndoa.
 
Haha hahaa .. I wish my wife wako angempata huby wangu lol.

Just simple; utasikia umeolewa ..wewe ni mke wa mtu(mke wangu) so u have to stay with ya family.

More over; atakwambia ukiolewa unaachana na wazazi unaambata na mume wako (na familia yako)

Nachoweza kukushauri rafiki usikubali maamuzi ya kuhusiana na familia yako yafanywe na watu wengine. Ni wewe kwa kushauriana na mkeo. Otherwise labda kama kuna ishu muhimu sana.

Mfano kama hyo mlioenda ya ubatizo nimesikia kucheka lol...... Mnawezaje kuacha majukumu yenu ili mhudhurie ubatizo mbeya.... Tena wa ndugu .. Dah!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom