Mwenye Nyumba agoma kurudisha pango

Dam Boe

Senior Member
Jul 29, 2022
128
87
Habari za majukumu mawakili, kuna mkwaruzano umetokea kati ya mwenye Nyumba na mpangaji Sasa msaada wa ushauri kwenu mawakili.

Ni hivi jamaa ameingia mkataba na baba mwenye Nyumba huo mkataba unasema alipe kodi ya miezi sita, ila yeye hakua na kodi ya miezi hiyo yote hivyo wakakubaliana alipe mitatu baada ya siku kadhaa amalizie hiyo mitatu, kama atashindwa kupeleka hiyo pesa atarudishiwa kodi yake ya miezi mitatu akatafute kwingine, yule mpangaji hakuwahi Kukaa pale wala mkataba na funguo hajakabidhiwa kwa madai kwanza amalize pesa.

Sasa zile siku alizopewa kupeleka salio lililo baki zimekwisha na baba mwenye Nyumba kagoma kurudisha pesa na pia amekataa yule jamaa asikae pale huku akisema mkataba unahesabika tarehe.

Je hili kisheria limekaaje na afanye nini kupata usuluhishi wa jambo lake aidha apate Kukaa kwa kodi hiyi ya miezi mitatu au arudishiwe pesa yake.
 
Ni hivi jamaa ameingia mkataba na baba mwenye Nyumba huo mkataba unasema alipe kodi ya miezi sita, ila yeye hakua na kodi ya miezi hiyo yote hivyo wakakubaliana alipe mitatu baada ya siku kadhaa amalizie hiyo mitatu, kama atashindwa kupeleka hiyo pesa atarudishiwa kodi yake ya miezi mitatu akatafute kwingine, yule mpangaji hakuwahi Kukaa pale wala mkataba na funguo hajakabidhiwa kwa madai kwanza amalize pesa. Sasa zile siku alizopewa kupeleka salio lililo baki zimekwisha na baba mwenye Nyumba kagoma kurudisha pesa na pia amekataa yule jamaa asikae pale huku akisema mkataba unahesabika tarehe.
Je hili kisheria limekaaje na afanye nini kupata usuluhishi wa jambo lake aidha apate Kukaa kwa kodi hiyi ya miezi mitatu au arudishiwe pesa yake.
Mzee mwenye nyumba yuko sahihi.Mkataba uko hai kabisa.
 
Mwenye nyumba yuko sahihi, maaana siku ile mpangaji alivyotoa ile hela ya miezi tatu, hela ilianza kutumika siku hiyo hiyo. Sasa kama siku zimeisha na huyo mpangaji hajajakuongezea ile hela maana yake mkataba wake umeishia pale hela ya miezi mitatu ilipokuwa inaisha. Hapa labda aanze kuandika mkataba mwingine wa miezi sita na kodi nyingine kabisa.
 
Hii ishu ya Mpangaji na Mwenye nyumba hapa Bongo ipo kienyeji sana hivyo hutegemea tu busara ya Mpanganji au Mwenye nyumba.

Kwa mfano tu Mimi nilikuwa na fremu mahali ila baada ya kuona biashara inasuasua na mkataba upo ukingoni nikamfuata Jamaa nikamwambia Mimi siendelei tena, hivyo nitalipa kwa mwezi huu ujao mmoja ila mpaka tarehe kumi na tano nitakuwa nimeshatoa vitu vyangu...na hapo ni tarehe 28.

Jamaa akaniambia basi we jitahidi tu mpaka hiyo tar 15 fremu iwe wazi wala usilipe...ukiangalia kwa haki nilipasw kumlipa kwani nimempa taarifa kwa kuchelewa...basi na nikatoa vitu by tar 12-14, tukaagana kwa amani.

Kila mmoja aking'ang'ania sheria tunaumizana tu.
 
Mwenye nyumba yuko sahihi, maaana siku ile mpangaji alivyotoa ile hela ya miezi tatu, hela ilianza kutumika siku hiyo hiyo. Sasa kama siku zimeisha na huyo mpangaji hajajakuongezea ile hela maana yake mkataba wake umeishia pale hela ya miezi mitatu ilipokuwa inaisha. Hapa labda aanze kuandika mkataba mwingine wa miezi sita na kodi nyingine kabisa.
Sasa hataki mpangaji atumie chumba hiko ilhali mpqngaji hajaweka chochote mule ndani
 
Vijana tutafute hela kwa nguvu zote, tujenge, tujiepushe na kudhalilishwa kwenye nyumba za watu
 
Habari za majukumu mawakili, kuna mkwaruzano umetokea kati ya mwenye Nyumba na mpangaji Sasa msaada wa ushauri kwenu mawakili.

Ni hivi jamaa ameingia mkataba na baba mwenye Nyumba huo mkataba unasema alipe kodi ya miezi sita, ila yeye hakua na kodi ya miezi hiyo yote hivyo wakakubaliana alipe mitatu baada ya siku kadhaa amalizie hiyo mitatu, kama atashindwa kupeleka hiyo pesa atarudishiwa kodi yake ya miezi mitatu akatafute kwingine, yule mpangaji hakuwahi Kukaa pale wala mkataba na funguo hajakabidhiwa kwa madai kwanza amalize pesa.

Sasa zile siku alizopewa kupeleka salio lililo baki zimekwisha na baba mwenye Nyumba kagoma kurudisha pesa na pia amekataa yule jamaa asikae pale huku akisema mkataba unahesabika tarehe.

Je hili kisheria limekaaje na afanye nini kupata usuluhishi wa jambo lake aidha apate Kukaa kwa kodi hiyi ya miezi mitatu au arudishiwe pesa yake.
Comon sense hapo hauhitaji mwanasheria. KWANZA nimeshituka kusikia kwama alisema endapo atashindwa kumalizia atarudishiwa hela yake. Kwa nini kwa sababu kutoa hiyo miezi mitatu tayari umezuia yeye kupangisha nyumba yake kwa mtu mwingine haijalishi umeishi au haujaishi. Mawazo yangu ni kwamba mwenye nyumba yuko sahihi. Labda tu akuonee huruma tu na aamue kukurudishia pesa yako kinyume na hapo sidhani kama kuna mahali atapata usaidizi wowote. Unasema ana mkataba alafu unasema hakuwahi kukabidhiwa sasa ana mkataba gani?
 
Back
Top Bottom