Mwenye nacho ataongezewa: Hawa ndio wakuu wa vyuo vikuu Tanzania

Chuo kikuu kina mwenyekiti wa Council. Huyu ndiye anatoa decisions. JK kama nilivyosema ni mtu wa kutunuku vyeti tu ndugu yangu!!!! Acheni kulalamika kila wakati na vitu msivyovijua. Wewe ukipewa kazi ya kujitolea utafanya?
Najua kuwa ni kutunuku tu lakini kwanini wapewe hao tu, tofautisha kulalamika na kuhoji mkuu.
 
Labda kuna kitu posho!!!!! Bado hamja angalia wenye viti wa mabaraza (council) wa vyuo- ni wale wale-huku pia ni posho na takrima kwenda mbele.
Mkuu, posho ni jina tu jingine la pesa, ishu ukitajiwa hcho kias cha posho yenyewe inaweza zid mishahara ya watu..
 
Wangekuwa vijana tayari wangeshaanzisha group lao la whatsapp halafu naona admin angekuwa Mfalme wa nyuki. Au huenda hata hawa wanalo tayari halafu wanatumiana ile video crip ya Msemakweli Mpenzi wa Mungu akiwaahidi wanafunzi wote waliochagulia chuo kupata mkopo then wanaidiscuss. Kama namwona Prof wa nyanda za juu kusini anaponda kinoma noma
 
Mkuu, posho ni jina tu jingine la pesa, ishu ukitajiwa hcho kias cha posho yenyewe inaweza zid mishahara ya watu..
Kwa upole tutaita posho. Kuna mwenyekiti mmoja wa baraza alipomaliza kipindi chake nasikia NOAH ilitafutwa na zawadi nyingine kedekede.
 
MIAKA MITATU ILIYOPITA NILIPATA KIBARUA SHIRIKA FULANI LA UMMA. KILICHONISHANGAZA ASILIMIA KUBWA YA PERMANENT STAFF WANA WATOTO/WAJOMBA/SHANGAZI/BINAMU/SHEMEJI ZAO WAMEAJIRIWA KAMA TEMPORARY EMPLOYEES. NILIPODODOSA HIZO TEMPO WANAZIPATAJE AU ZINATANGAZWA WAPI, MAJIBU NI KUWA UNALETWA NA NDUGU YAKO, HALAFU UNASUBIRI KUAJIRIWA RASMI BILA USAILI WOWOTE. HII NDIYO TANZANIA, UPENDELEO, UKABILA NA UNDUGU VIKO JUU KULIKO INAVYODHANIWA.
Nakuunga mkona,ni kweli. Nimefanya utafiti mdogo hivi karibuni. Makao makuu ya Idara inaongozwa na wazee,chini yao kuna vijana ndo wameajiriwa karibuni. Peleleza origin ya hao vijana utapata jibu. Kuna wachapakazi wazuri tu mikoani kiasi cha kuwasogeza kwenye post hizo,ni wazoefu,ila hutaona. Akisogea na si ndugu au wa kujuana hofu yao anaweza kufukua makaburi. Kuna kazi nyingine ni vyema mwanzo wa ajira uanzie kijijini,sio makao makuu ili upate uzoefu. Mfano our presda.
 
1. UDSM
-Jakaya Mrisho Kikwete (66 yrs)
-Raisi mtaafu wa Tanzania
-Kateuliwa na Raisi Magufuli

2. UDOM
-Benjamin William Mkapa (78 yrs)
-Raisi mstaafu wa Tanzania
-Aliteuliwa na Kikwete

3. MUHIMBILI
-Ali Hassan Mwinyi (91 yrs)
-Raisi mstaafu wa Zanzibar

4. State University of Zanzibar
-Dr Ali M. Shein (68 yrs)
-Raisi wa Zanzibar

5. SUA
-Joseph Warioba (76 yrs)
-Makamu wa Rais mstaafu na Waziri mkuu mstaafu

6. Nelson Mandela
-Dr. G. Bilal (71 yrs)
-Makamu wa Raisi mstaafu

7. CHUO KIKUU HURIA (OUT)
-Mizengo Pinda (68 yrs)
-Waziri Mkuu mstaafu

8. Hubert Kairuki
-Dr. Salim Ahmed Salim (74 yrs)
-Waziri Mkuu mstaafu na
-Secretary General mstaafu wa ilyokuwa OAU na baadae AU

9. Ardhi University
-Cleopa Msuya (85 yrs)
-Waziri Mkuu mstaafu

10. Mzumbe University
-Barnabas Samatta (76 yrs)
-Jaji Mkuu mstaafu

11. MUST
-Prof Mark Mwandosya (67 yrs)
-Waziri Mstaafu

Ama kwel aliyenacho ataongezewa na asie nacho akajiajiri !!!!!

A] Katka hii list Kikwete ndo mdogo kiumri
Hivi hii nafasi inaangalia umri, hata kama, Je hakuna watu wenye cv zilizotukuka wenye 50 to 60 au 65 yrs hivi
Hii nafas ina uzito kias gan mbona kuna wakuu wa nchi wenye umri chini ya miaka 50
1. John Kennedy (USA)
-alkuwa raisi akiwa 43 yrs
2. Atifete Jahjaga (KOSOVO)
-She was 36 yrs
3. Kabila (Congo)
- was 29yrs, now 45
4. Barack Obama USA
-was 47yrs, now 55
5. Andrzej Duda (POLAND)
-was 44yrs, now 45

Uraisi ni taasisi kubwa zaid ya ukuu wa chuo, so sidhan kama umri mkubwa kias hcho ndo kigezo

B] Nikadhan pia labda inabd uwe public figure au uwe na political experience
Sasa ngoja tuone hali ipoje kwa vyuo vitambulikavyo kidunia Chancellors wao :
1. HARVARD UNIVERSITY
- Drew Gilpin Faust
-Professor of History in Harvard's Faculty of Arts and Science

2. MASSACHUSETTS
-Kumble R. Subbaswamy
-Professor, Department of Physics and Astronomy

3. STANFORD UNIVERSITY
-Marc tessier Lavigne
-alkuwa chancellor wa Rockefeller university na
-Head of the Laboratory of Brain Development and Repair

Kazi kwel kwel, wateuzi na wateuliwa ni wale wale, duuu

Aliye na mtaji anateuliwa na asie na mtaji anaambiwa ajiari
Sio kwamba vijana wa 20s ndo wateuliwa la hasha, lakin akiteuliwa wa 50s, wa 40s atapanda kuziba nafasi na 30s atapanda hali kadhalika 20s atapata nafasi huku chini

Wastaafu wana nafas kubwa sana ya kuwashaur viongoz wa juu, wana access, tena hata kwa kumpigia simu tofaut na raia wengine KWANN WASIBAK KAMA WASHAUR TU, na wapate mda wa kuwa na familia zao baada ya majukumu mazito ya kulitumikia taifa hili kama alvosema Mzee Kikwete wakat anaaga ile mwaka jana???

Chancellor ni ceremonial leader, labda kuna vigezo vya kuteuliwa,
wana jamvi tusaidiane tafadhal
NB:
marekebisho yanaruhusiwa
ASANTENI NA KARIBUNI

MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUM JE?
 
Ukiuliza Je ? Hakuna Watu Wengine Wenye Sifa Wakapewa Hizo Nafasi Na Kuongoza Hivyo Vyuo Vikuu
Utapewa Jibu La Karaha Sana Mpaka Utakasirika...

Utaambiwa Eti Ni Busara Ya Kiongozi Kweli ?
Vijana Wa Umri Wa Wastani Na Wenye Sifa Wapo
Kwanini Wasiwateu Kupata Uzoefu Na Itakuwa Ndiyo Njia Ya Kuandaa Viongozi Mbalimbali Kuendeleza Nchi
 
Wazee hao hata wakipumzika wanalipwa pesa nyingi sana na huduma zote wanapata kwa iyo wanapewa izo nafasi ili wasikae bure huku wakilipwa pesa nyingi
Jaribu kufikiri vizuri sababu upo katika jukwaa la home of greater thinker! ,
Kwenye hicho cheo kacover nafasi ya mtu ambae hana ajira pia ambae hajafikia umri wa kustaafu na ana ELIMU sawa au kubwa zaidi yake!

Pili.
Bora akae nyumbani awe analipwa pension peke yake kuliko kupewa taasisi ambayo atakuwa analipwe mshahara wa taasisi husika pamoja na pension juu!
 
Back
Top Bottom