Mwenye mkono mrefu ni mwizi

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,843
Hiki ndicho tulichofundishwa udogoni na hata shule za msingi na sekondari... Huu ni msemo wa hekima wa wahenga kwamba tafsiri ya mkono mrefu ni wizi yaani mwizi kwa tafsiri nyingine ni mtu mwenye mkono mrefu....
Siku hizi mambo yamebadilika tafakuri zimekuwa nyingi... Nimeikuta mahali watu wakijadili kuhusu mkono mrefu wa serikali.... Kwamba eti serikali ina mkono mrefu . .... SERIKALI INA MKONO MREFU.... sitaki nichague tafsiri ile ya wahenga najitahidi kubaki na tafsiri husika ila inaniwia vigumu mno kukubaliana na huu ukweli.... Kwamba mkono mrefu wa serikali sio kwa tafsiri ile ya wahenga.... WIZI
 
1 Wizi wa kuuwa wanasiasa
2 Wizi wa kuuwa wanafunzi
3 Wizi wa kupotea Watanzania wenzetu
4 Wizi wa madaraka
5 Wizi wa kodi kwa wanyonge
6 Wizi wa rasilimali ya taifa
7 Wizi wa kuhujumu democracy nchini
Siku moja kwenye ishu za miamala ya kufanya malipo ya serikali pale bandarini kwetu nikakosea Baada ya kulipa elfu hamsini nikalipa laki 5 tasilimu kwa njia ya mtandao
Fujo zangu za kufuatilia nirudishiwe kilichozidi zilinifikisha kwa kamishna na kuambulia jibu la SIRIKALI HUWA HAIRUDISHI CHENCHI...!!! Nilichoka
 
Duuu
 
Kosea Miamala Yote Ila Ikiingia Kwenye Account Ya Serikali Hapo Ndiyo Utajua Kwanini Paka Havuki Mto Tra Mwanza Laki 7 Tangu 2013 Mpaka Nikasamehe Pigwa Danadana Mwanzo Mwisho Wakati Makosa Yalikuwa Yao
 
Halafu bahati mbaya sana hawalogeki :( :( :(
 
Back
Top Bottom