Mwenye kujua sifa na matukio ya uongozi wake afande Awadhi Anijuze. Ni yule aliyekuwa RPC Kinondoni

mwenyewe nani mkuu?

yaani huu uzi unachekesha mpaka basi,awadh. kuna watu wakisikia tu hili jina wanazima simu kabisa.

nakumbuka kuna uzi humu 2015 ulikuwa unatoa update awadh yuko kipande gani ili watu wapandishe soksi.
Kwani hizo daladala za Nanga boy ni za nani , kwanini zisiguswe?
 
Hahahaaaa.... Na ndio maana sikutaka kwenda jeshini. Najijua kuwa mimi ni mbishi na mwenye kufanya mambo kwa sababu za msingi... Mambo ya NDIYOOOOOOOOOOOOOO, afandeeeeeeeeeee... Ningefukuzwa tu. Kuna jamaa yangu ana akili sana. Aliingia jeshini lakini hakumaliza hata mafunzo akafukuzwa.
wakati jeshini mwenye cheo ndio mwenye akili.
 
Hahahaaaa.... Na ndio maana sikutaka kwenda jeshini. Najijua kuwa mimi ni mbishi na mwenye kufanya mambo kwa sababu za msingi... Mambo ya NDIYOOOOOOOOOOOOOO, afandeeeeeeeeeee... Ningefukuzwa tu. Kuna jamaa yangu ana akili sana. Aliingia jeshini lakini hakumaliza hata mafunzo akafukuzwa.
kwani unadhani ungefukuzwa mkuu??waala.

ila kitu ungefanywa ungetoroka kabisaaa bila kuaga.
 
ACP Awadh hafai kuwa Polisi wa Africa

Akikukamata sahau mambo ya kumpa simu sijui aongee na bosi gani sijui Mh. Nani

Aliwahi kukamatwa Mke wa Mh. Balozi Mahiga akamtingisha Askar mdogo yule Askar akampa simu aongee na Awadh, alimpa Makavu live bila ya chenga


Alipokuwa RTO Kinondoni tabia ya kutanua Barabaran ilitoweka kabisa na kuna siku nilimshuhudia akimkamata Askar wa JWTZ alietanua

Naskia kapotezwa kwny ramani kwa kujifanya ‘Mjuaji mfuata sheria na miongozo

Sie tusiopenda Sheria tunamchukia sana kwa kuwa kawaida yetu ni kufanya vurugu barabaran halafu ukikamatwa unampa simu aongee na Bosi wake alikuwa anakataa anasema kwanza akukatie ile fine then ndio anapokea simu
Sasa hivi Kinondon inapumua na hata Makusanyo sio kama zaman ‘
Dhambi yake ni kufuata sheria? Mwenyezi Mungu ambariki aisee.
Hakuna kitu kibaya kama uonevu
 
Back
Top Bottom