Mwenye kujua gharama za kujenga msingi wa nyumba ya vyumba viwili, sebule, jiko, stoo na chumba cha chakula

kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
1,350
2,000
Habarini ndugu zangu,

Naomba kujua gharama za kujenga msingi tu wa nyumba kama nilivyoelezea hapo juu

-Vyumba viwili (viwe na makabati ya ukutani na viwe master),
-Sebure
-dinning
-jiko
-store

Eneo langu ni 20*29
Mahala ni: Mbezi ya Kimara, Dar es Salaam

Naomba kujua, ni kiasi gani nikikiandaa naweza jenga msingi wa nyumba hiyo

Karibuni

Sent using komputa mpakato
 

akatanyukuile

JF-Expert Member
Sep 13, 2019
314
500
Na vyumba hivyo unataka viwe na ukubwa upi? Maana unakuta nyumba nyingine inaukubwa wa square mita 400 ila ina chumba na sebure tu. Hivo elezea kinagaubaga mchoro wa nyumba ya ndoto yako ikoje

Sent using Jamii Forums mobile app
 

king kan

JF-Expert Member
May 6, 2011
1,504
2,000
Ni mita ila kwa ukubwa wa eneo hilo na nyumba anayotaka kujenga kwa kiwanja hicho atakos pa kuchimba choo na pa kuanikia nguo
Ushawahi kujenga wewe? Hilo eneo ni almost sqaure metre 580 anashindwa vipi kujenga. Nyumba anayopendekeza kwa haraka haraka itacover square metre 60-70. Eneo linalobaki ni kubwa sana.

Watu wamejenga nyumba kwenye plot ya Mita 15 kwa 15 na vyote unavosema vipo.
 

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
19,151
2,000
Itakuwa sio nyumba hiyo ni banda.
Ndugu mimi nimejenga .
Sema kwa yeye kwa kiwanja chake ni cha kuanzia maisha kwa kujishikiza tu kitamtosha ukijenga hapo nyumba ya kuishi familia inavyotakiwa ni kidogo sana atakosa hata pa kupaki gari kama analo
Ushawahi kujenga wewe? Hilo eneo ni almost sqaure metre 580 anashindwa vipi kujenga. Nyumba anayopendekeza kwa haraka haraka itacover square metre 60-70. Eneo linalobaki ni kubwa sana.

Watu wamejenga nyumba kwenye plot ya Mita 15 kwa 15 na vyote unavosema vipo.
 

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
42,113
2,000
Msingi unategemea
1. Eneo likoje, tambarare au kuna bonde
2. Unamwaga jamvi au msingi wa tofali za kulaza na kufunga mkanda
3. Gharama za fundi hazilingani
 

king kan

JF-Expert Member
May 6, 2011
1,504
2,000
Kupata gharama za jumla kadiria ukubwa wa eneo zidisha na 600k utapata gharama za kujenga nyumba ya kisasa yote na makorokoro yote. Nyumba ya kawaida zidisha mara 450k. Nyumba ili mradi unaishi zidisha mara 350k.

Ukitaka mchanganuo inabidi utoe taarifa za kina sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom