Gharama ya ujenzi wa vyumba vitatu, sebule, jiko na choo cha ndani

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,699
9,775
Wakuu, Natumai mko vyema na mmejiandaa kikamilifu kuhesabiwa.

Unaambiwa upange maisha yako kwanza, uhakikishe unakuwa kwenye mstari wa mafanikio kisha uwaze kuhusu maisha ya ndoa. Uki-vise verse tambua kabisa utakuja kupigwa na kitu kizito kichwani mpaka ushangae. Nimeishuhudia mahali

Twende kwenye hoja:
Nahitaji kujenga nyumba ya vyumba vitatu (3 bedrooms), sebule ya ukubwa wa kawaida (yaani lisiwe casino), dining room iliyounganika na kitchen room kiaina, bila kusahau choo na bafu la ndani. Nahitaji kuweka vigae pamoja na singboard. Kupiga leap na kupakaa rangi nje na ndani. Madirisha ya aluminium yatakuwa sita nyumba nzima jumlisha na tu aluminium tudogo tuwili twa choo na bafu! Nahitaji kufanya wiring na kuweka umeme kabisa.

Niko mbele zenu ili kujua gharama zinazohitajika kwa ajili ya kukamilisha jukumu hili. Gharama za jumla kwa wenye uzoefu, ili kusudi nikienda kuchukua huu mkopo benki nimalize suala hili moja kwa moja, yasiwepo masuala ya aliishia kwenye renta! Hata kama una uzoefu may be na mchanganuo wa matofali, au sementi, au mabati (msaudhi) yatakayotosheleza pamoja na mbao zake naomba msaada wako kuhusu gharama. Nafahamu wengi wenu humu mmejenga!

Mawazo tafadhari!
 
Ujenzi wa nyumba ( gharama zako tofauti na za wengine) ni kama kuingia kwenye ndoa (changamoto zako tofauti na za wengine).

Kwann tofauti? Material tofauti, Umbali wa site tofauti, mafundi tofauti, ardhi (hivyo muundo wa msingi) tofauti, ukubwa tofauti, shimo la choo tofauti, n.k

Nyumba Anza tu kujenga mkuu. Hela yako itakapoishia ndiyo hapo hapo. Utakuja kumalizia utakapokopa tena baada ya kumaliza deni la mkopo wako wa Sasa.
 
Habari mkuu, ili upate makadilio yanayoakisi uhalisia, ni vyema ukawa na ramani yenye vipimo vyote na specification za nyumba.
Lakini kwa uzoefu tu kwa sasa, boma mpaka kuezeka itacheza 18m -25m kulingana uchaguzi wa materials.

Kuhusu finishing, hii haina formula kwa kuwa materials zipo za aina na bei tofauti tofauti. Lakini pia kwa uzoefu uwe na 15m +. Hapo utahamia

Ukitaka mambo ya kitaalamu zaidi, tuwasiliane kwa 0715477041.
 
Wee unajielewa.
 
Raman ya nyumba ipoje...? Ramani ina ukubwa gani (Square meters)...? Kiwanja chako kikoje...? Upo mjini au kijijini..? Haya na mengine mengi yana determine gharama za ujenzi... All in all ukitaka ikamilike roughly uwe na 40M ukitaka ya kuhamia tu mengine yataendelea ukiwa ndani uwe na 25M. Hii ni estimation ya popote Tz
 
Mkuu fuata uzi huu.
 
Mkuu japo wewe ni mtaalamu usitishe watu.
Vyumba vitatu kwa millioni mia kwa mtu anayejenga nyumba ya kwanza maishani mwake ?
 
We jamaa wa ovyo kbsa.... Anakwambia nyumba ya kawaida... Ww unampa bajeti ya bangaroo..

Nyie ndio mnakatisha watu tamaa
Ukiniambia Nyumba itakua na Square Meter ngapi naweza kukupa Makadirio ya Msingi Tu, au Ujenzi mpka finishing.

Kwa Bei Ya Vifaa ya Sasa makadirio inaweza kugharimu million 100. Mpka Finishing. Gharama hyo inaweza Kuongezeka au kupungua Kutokana na Bei ya Vifaa Vya UJENZI na Upatikanaji Wake kwenye eneo Husika.

Hii Hapa ni mfano wa Vyumba 3. Nyumba ya Makazi.
  • Masta 1, Vyumba vya Kawaida 2.
  • Study/ Prayer Room
  • Sebule, Dinning, Open Kitchen na Stoo yake
  • Choo Cha public
  • Bafu Public.
Ina Sqm 217.5. Kitalaamu Gharama ya Ujenzi Mpaka Kukamilka Kila Kitu ni Tsh 108,750,000/=

Huo ndio Ukweli Mchungu, Bila kukuongopea.
 
Wakuu, Natumai mko vyema na mmejiandaa kikamilifu kuhesabiwa.

Unaambiwa upange maisha yako kwanza, uhakikishe unakuwa kwenye mstari wa mafanikio kisha uwaze kuhusu maisha ya ndoa. Uki-vise verse tambua kabisa utakuja kupigwa na kitu kizito kichwani mpaka ushangae. Nimeishuhudia mahali

Twende kwenye hoja:
Nahitaji kujenga nyumba ya vyumba vitatu (3 bedrooms), sebule ya ukubwa wa kawaida (yaani lisiwe casino), dining room iliyounganika na kitchen room kiaina, bila kusahau choo na bafu la ndani. Nahitaji kuweka vigae pamoja na singboard. Kupiga leap na kupakaa rangi nje na ndani. Madirisha ya aluminium yatakuwa sita nyumba nzima jumlisha na tu aluminium tudogo tuwili twa choo na bafu! Nahitaji kufanya wiring na kuweka umeme kabisa.

Niko mbele zenu ili kujua gharama zinazohitajika kwa ajili ya kukamilisha jukumu hili. Gharama za jumla kwa wenye uzoefu, ili kusudi nikienda kuchukua huu mkopo benki nimalize suala hili moja kwa moja, yasiwepo masuala ya aliishia kwenye renta! Hata kama una uzoefu may be na mchanganuo wa matofali, au sementi, au mabati (msaudhi) yatakayotosheleza pamoja na mbao zake naomba msaada wako kuhusu gharama. Nafahamu wengi wenu humu mmejenga!

Mawazo tafadhari!
Kama Ni kajumba tu kadogo, at least huwe na mil.40
 
Kama unataka nyumba iwe complication ya mambo mengi andaa kama mil 25 hadi 35..

Lakin kama unataka nyumba ya kawaida tu.. Hapo andaa mili 15 hadi 25... Kwa bajeti ya chini kbsa..

Wakuu, Natumai mko vyema na mmejiandaa kikamilifu kuhesabiwa.

Unaambiwa upange maisha yako kwanza, uhakikishe unakuwa kwenye mstari wa mafanikio kisha uwaze kuhusu maisha ya ndoa. Uki-vise verse tambua kabisa utakuja kupigwa na kitu kizito kichwani mpaka ushangae. Nimeishuhudia mahali

Twende kwenye hoja:
Nahitaji kujenga nyumba ya vyumba vitatu (3 bedrooms), sebule ya ukubwa wa kawaida (yaani lisiwe casino), dining room iliyounganika na kitchen room kiaina, bila kusahau choo na bafu la ndani. Nahitaji kuweka vigae pamoja na singboard. Kupiga leap na kupakaa rangi nje na ndani. Madirisha ya aluminium yatakuwa sita nyumba nzima jumlisha na tu aluminium tudogo tuwili twa choo na bafu! Nahitaji kufanya wiring na kuweka umeme kabisa.

Niko mbele zenu ili kujua gharama zinazohitajika kwa ajili ya kukamilisha jukumu hili. Gharama za jumla kwa wenye uzoefu, ili kusudi nikienda kuchukua huu mkopo benki nimalize suala hili moja kwa moja, yasiwepo masuala ya aliishia kwenye renta! Hata kama una uzoefu may be na mchanganuo wa matofali, au sementi, au mabati (msaudhi) yatakayotosheleza pamoja na mbao zake naomba msaada wako kuhusu gharama. Nafahamu wengi wenu humu mmejenga!

Mawazo tafadhari!
 
Ukiniambia Nyumba itakua na Square Meter ngapi naweza kukupa Makadirio ya Msingi Tu, au Ujenzi mpka finishing.

Kwa Bei Ya Vifaa ya Sasa makadirio inaweza kugharimu million 100. Mpka Finishing. Gharama hyo inaweza Kuongezeka au kupungua Kutokana na Bei ya Vifaa Vya UJENZI na Upatikanaji Wake kwenye eneo Husika.

Hii Hapa ni mfano wa Vyumba 3. Nyumba ya Makazi.
  • Masta 1, Vyumba vya Kawaida 2.
  • Study/ Prayer Room
  • Sebule, Dinning, Open Kitchen na Stoo yake
  • Choo Cha public
  • Bafu Public.
Ina Sqm 217.5. Kitalaamu Gharama ya Ujenzi Mpaka Kukamilka Kila Kitu ni Tsh 108,750,000/=

Huo ndio Ukweli Mchungu, Bila kukuongopea.
We jamaa chenga Sana , unajua vyumba vitatu anavyomaanisha mtoa mada
 
Back
Top Bottom