Mwenye kujua gharama za kujenga msingi wa nyumba ya vyumba viwili, sebule, jiko, stoo na chumba cha chakula

Wajameni kama hamjawahi kujenga nyumba piteni tu, hapa jamaa anataka wale ambao wamejenga watoe uzoefu. kwa mfano unaeleza umetumia tofali ngapi, mchanga kiasi gani, mifuko ya cement mingapi, kokoto kiasi gani, gharama za maji, malipo ya mafundi n.k. kuna mada zingine zinaelekeza, zinafundisha, sasa watu wanaleta masihara.
 
Ni mita ila kwa ukubwa wa eneo hilo na nyumba anayotaka kujenga kwa kiwanja hicho atakos pa kuchimba choo na pa kuanikia nguo
unazingua ukubwa huo nyumba inajengwa na nafasi ya banda la kuku inabakia.
 
Kwa kifupi unatakiwa uwe na ramani ya nyumba hiyo na kibali cha ujenzi, vinginevyo ni kosa kisheria.
Nilidhani utanielewa huo ni ujenzi mkubwa.
Ungemuelewesha na sisi tukaelewa tupo kwa ajili ya kushikana mikono tulipo kwama.
 
wajameni kama hamjawahi kujenga nyumba piteni tu, hapa jamaa anataka wale ambao wamejenga watoe uzoefu. kwa mfano unaeleza umetumia tofali ngapi, mchanga kiasi gani, mifuko ya cement mingapi, kokoto kiasi gani, gharama za maji, malipo ya mafundi n.k. kuna mada zingine zinaelekeza, zinafundisha, sasa watu wanaleta masihara.
upo sahihi kabisa
 
Itakuwa sio nyumba hiyo ni banda.
Ndugu mimi nimejenga .
Sema kwa yeye kwa kiwanja chake ni cha kuanzia maisha kwa kujishikiza tuu kitamtosha ukijenga hapo nyumba ya kuishi familia inavyotakiwa ni kidogo sana atakosa hata pa kupaki gari kama analo
Sijui unaongelea nyuma gani wewe hata sikuelewi yaani ulubwa kiwanja 20×29 unasema atakosa pa kupaki gari kwani kasema anajenga hekalu na swimming pool ndani?

Kuna raman nzuri kabisa zina 12×13 au 11×13 na ina kila kitu na nafasi ndani nzur tu ina maana haitoshi hapo kwenye eneo hilo?

Tena kuna ramani ya ghorofa 1 ni nzuri kabisa ina 5×15 vyumba vitatu master vyote sebule kubwa dinning nk na ni nzuri , we mwenzetu sijui unaongelea ramani za miaka ya 1947 huko.

Au we mwenzetu bado unatumia mifumo ya ramani za kizamani zenye korido kama handaki. Mambo yasha badilika siku hizi ramani za kisasa na nzuri na ina nafasi lakini hachukui eneo kubwa
 
Tafuta mtaalam, ma civil engineer wamejaa kibao mtaani, kwa nyumba ya chini hata fundi wa mtaani tu anaweza kukuanyia
 
Back
Top Bottom