Mwenye Historia ya Umishenari Songea

Sema...
Tatizo la vitabu hivyo ni kuwa havina ukweli katika historia ya Tanganyika.
Waandishi wanaandika kwa kuchagua wanachokitaka si ukweli wa historia.
Swali rahisi kabisa Mzee ni imani hiyo (imani yako) iliwafikiaje hao wangoni/ wamanda huko Songea miaka hiyo?
 
Swali rahisi kabisa Mzee ni imani hiyo (imani yako) iliwafikiaje hao wangoni/ wamanda huko Songea miaka hiyo?
Loftins,
Kwani Father Johannes wa Peramiho aliyewabatiza Wangoni waliohukumiwa kunyongwa na Wajerumani alifikaje Peramiho?
 
Loftins,
Kwani Father Johannes wa Peramiho aliyewabatiza Wangoni waliohukumiwa kunyongwa na Wajerumani alifikaje Peramiho?
Ina maana njia hiyohiyo iliyotumiwa na wajerumani ndio hiyohiyo iliyotumiwa hapo awali na waarabu?

Waliua na kusilimisha watu kutoka kwenye uasili wao?
 
Loft...
Kwa nini unasema mimi nimewaita Waislam?
Kwani wao wenyewe wakijiitaje?
Wangoni ni watu wenye asili ya Afrika ya kusini tunajua hii historia, na afrika ya kusini toka enzi haijawahi kuwa na population ya hata theluthi ya hiyo imani yako.

Yani kwa kifupi mzee ambacho huwa unatusimulia kuhusu uchache wa wafuasi wa hiyo dini yako England na kwingineko miaka hiyo ndio kiko S.A hadi leo hii.

Hii inaleta ukakasi sana kujua waliupataje huo uislamu wao hao wamanda/wangoni maana Songea si pwani au walifata watumwa waarabu? 🙄 maana ndio shuhuli zao hadi leo hii wale
 
Wangoni ni watu wenye asili ya Afrika ya kusini tunajua hii historia, na afrika ya kusini toka enzi haijawahi kuwa na population ya hata theluthi ya hiyo imani yako.

Yani kwa kifupi mzee ambacho huwa unatusimulia kuhusu uchache wa wafuasi wa hiyo dini yako England na kwingineko miaka hiyo ndio kiko S.A hadi leo hii.

Hii inaleta ukakasi sana kujua waliupataje huo uislamu wao hao wamanda/wangoni maana Songea si pwani au walifata watumwa waarabu? maana ndio shuhuli zao hadi leo hii wale
Loftins,
Ushapata kusoma Across Atlantic Slave Trade?
 
Loftins,
Ushapata kusoma Across Atlantic Slave Trade?
Naaam nimepata kuisoma hii unaiamini kuwa haijachakachuliwa ila maoni ya Semahengere uliyakataa kuwa yamechakachuliwa?

😝😝
Kuna wenzako huwa wanaipinga Biblia na tukiwauliza maswali lukuki huitumia hiyohiyo kujibu hoja zetu
 
Naaam nimepata kuisoma hii unaiamini kuwa haijachakachuliwa ila maoni ya Semahengere uliyakataa kuwa yamechakachuliwa?

😝😝
Kuna wenzako huwa wanaipinga Biblia na tukiwauliza maswali lukuki huitumia hiyohiyo kujibu hoja zetu
Loftins,
Huwezi kuwa na uhakika wa asilimia mia moja kwa kazi yoyote ya mikono ya binadamu kuwa imekamilika haina makosa.

Ila tofauti baina yetu hapa ni kuwa mimi nimewazidi kwa kuwa nimetafiti masuala haya na nina papers na vitabu kadhaa nilivyoandika na kuchapwa.

Kwa ajili hii basi ukinitaka rejea ya kile nilichoandika nitakupa.
 
Manyanza,
Umetaka hstoria kamil ya Wamishionari Songea na hstoria ya Maji Maji.
Makala takuwa ndefu sana.

Lakini unaweza kusoma hstoria hii kwa urefu wake katka Google na kwengineko.
Nmekuwekea hapa makala ambayo kwa kifupi itakuonyesha msimamo wa Wamishionari kabla na baada ya Vita Vya Maji Maji:

KANISA NA VITA VYA MAJI MAJI

Hassan Ilunga Kapungu

ABDULRAUF SONGEA MBANO

JEMADARI WA VITA VYA MAJI MAJI 1905 - 1907

View attachment 2226369
Abdulrauf Songea Mbano​

Nje kidogo ya mji wa Songea kuna kitongoji kinaitwa Mahenge, hapo kuna sehemu ya kumbukumbu ya vita vya Majimaji. Jambo kubwa la mahala hapo ni kaburi kubwa la halaiki ambamo askari zaidi ya sitini na… (sitini na saba) walizikwa kwa pamoja. Na kando ya kaburi hilo la pamoja kuna kaburi la Abdulrauf Songea Mbano ambae yeye alizikwa peke yake.

Kwa mara ya kwanza nilitembelea makumbusho hayo mwishoni mwaka 2007. Baada ya kusaini kitabu cha wageni na kulipa ada ya kituo muhudumu wa kituo hicho alitupa karatasi yenye orodha ya majina ya wale wote walionyongwa na kuzikwa hapo. Ukiitazama orodha hiyo na hasa ukiwa Mwislam jambo moja litakustuwa. Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam. Linaanza jina lake la Kiiislam, kisha kwenye mabano kuna jina la Kikristo na mwishoni linaishia jina la kiasili, mfano Abdulrahman [Dominic] Mputa Gama.

Muhudumu akatueleza kuwa hawa mashujaa wa vita vya Maji Maji kabla ya kunyongwa alikuwako padri ambae aliwabatiza na kuwapa majina ya Kikristo na baadae kunyongwa, wengi walibatizwa kwa hadaa kuwa wakibatizwa wataachiwa huru, wote katika hao walionyongwa walikuwa ni Waislam. Uzuri ni kwamba katika orodha hiyo kulikuwa na jina na sahihi ya yule padri aliyewabatiza, na kwa mkono wake [huyo padri] aliiyaandika hayo majina. Karatasi yenyewe ilihifadhiwa vizuri kwenye fremu ngumu ya kioo. Tuliomba kwa nguvu zote kupatiwa hiyo karatasi ya majina hata kwa kununua lakini haikuwezekana pamoja na kuwaona na kuwaona wakubwa wa kituo hicho. Niliporudi kwa mara ya pili mwezi July 2009 nilipata mstuko.

Karatasi iliyohifadhiwa kwenye fremu ngumu ya kioo, iliyokuwa na majina ya Kiislaam ya mashujaa wa vita vya Maji Maji, haikuwapo,na badala yake imewekwa karatasi nyingine ombayo ndani ya karatasi hiyo majina ya Kiislaam ya mashujaa hao wa vita vya Maji Maji yameondolewa na kuachwa majina ya ubatizo na yale ya kiasili tu, jina la padri, sahihi yake na wadhifa wake katika Kanisa Katoliki pia vimeondolewa na karatasi yenyewe haikuwa kwenye fremu ya kioo na ilikuwa katika fotokopi tu.

Nilimuuliza muhudu kulikoni? Akasema, “Songea pana mzee mmoja maarufu sana katika historia ya TANU na historia ya kuasisiwa Bakwata anaitwa kwa kifupi M. S. Mzee huyu ana binti yake ambaye ameolewa na Mzungu wa Kijerumani. Binti huyu na na mumewe wa Kijerumani walikuja hapa Songea matembezi. Hivyo kwa shinikizo la huyu mzee M.S. karatasi hiyo alipewa huyu Mzungu kwa ahadi kwamba anaipeleka Ujerumani na atairudisha. Hivyo ndivyo karatasi ile asilia ilivyotoweka. Kubwa katika karatasi ile ni ule ushahidi wa majina kuwa wote katika wale walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam, wengi katika hao walihadaiwa kuachwa huru hivyo wakabatzwa ispokuwa wachahe sana waligoma kama shujaa Abdulrauf Songea Mbano. Huyu kwa ushujaa wake wa kupambana na Wajerumani aligoma na akasumbua sana kiasi akanyongwa siku yake na peke yake na ndio sababu akazikwa peke yake.

Ukiingia ndani ya kinyumba cha ghorofa, unaanza kuona picha za mashujaa wa Maji Maji wakiwa wamevaa mavazi ya vita mithili ya mahujaji wanavyovaa Ihraam wakati wa hija. Kinachoongezeka kwao ni vilemba kichwani. Chini ya kila picha kuna jina la aliyekuwa kwenye picha ile. Ukipanda gorofani utaona silaha za kiajadi kama mikuki, pinde, ngao n.k. Kinachosisimua zaidi ni mavazi ya vita. Mavazi ya vita ya askari wa Maji Maji wengi walivaa kanzu za Kiislaam na vilemba. Jambo jingine linalosisimua ni kile ambacho watu wa kituo hicho wameandika ”rosary” hili ni jina la Kikristo, hasa la Kikatoliki, ni zile shanga ambazo huning’inia msalaba lakini unapotazama hicho kilichoitwa “rosary” utaona si “rosary,” bali ni tasbihi hasa ya Kiislaam yenye kupangika hasa shanga zake, 33, 33, 34. Maneno yaliyoandikwa kuelezea “rosary” hizo ambazo ni tasbihi ni:

“Hizi ni rosary ambazo wapiganaji wa majimaji walikuwa wakitumia KUTAMBIKA kabla ya kwenda vitani kwa kuamini kwamba zitawakinga na risasi.”

Ukweli ni kwamba hawa askari wa Maji Maji wengi walikuwa ni Waislaam hivyo hawakuwa WAKITAMBIKA bali walikuwa wakitumia tasbihi hizo kufanya dhikri kwa Allah kabla ya kwenda vitani. Midhali sisi Waislaam hatujawa tayari kuandika historia yetu kama Waislaam wanaotuandikia watapotosha na kupindisha na kutuzulia wanavyotaka. Hapo gorofani kuna jambo jingine la kusisimua. Kuna magudulia na makopo. Wameandika kuwa, haya ndio makopo ambayo askari wa Maji Maji walikuwa wakiyatumia KUNAWA kabla ya kwenda vitani [kushika udhu na sio kunawa] pia kwa kuamini kuwa maji hayo yatawakinga. Muhudumu alitueleza kuwa kumbukumbu nzuri na za kuaminika ziko Jimbo Kuu la Wakatoliki Peramiho.

Tulikwenda jimboni lakini hatufanikiwa kwa sababu za ki-urasimu tu.T ulitakiwa tupate kibali cha Askofu Mkuu. Hatukukipata. Kwa yale tuliyoyaona na kuyashudia yafuatayo:

Vita vya Maji Maji havikuwa ni vita vya kizalendo, kwamba wazalendo walikuwa wakipigania nchi yao. La vilikuwa ni vita vya Waislaam wakipigana na Wakristo wa Kijerumani waliovamia maeneo asilia ya Waislaam kwa lengo la kuuwa Uislam na kusimamisha Kanisa kwani mazingira yote utayoyaona ya mashujaa wa vita vya Maji Maji ni mazingira ya Kiislaam, kingine ni kwamba hukuti mahala yalipo makaburi ya askari wa Kijerumani ila katika miji ya Waislaam kama Kilwa, Bagamoyo n.k. Kwa nini wauliwe maeneo ya Waislaam tu?

Walifuata nini huko?

Kuna upotoshaji mkubwa sana wa historia ya vita vya Maji Maji. Vinaoneshwa kama ni vita vya wazalendo wakipigana na wakoloni wa Kijerumani, wakati ukweli si hivyo. Ukweli ni kwamba vita vya Maji Maji vilikuwa ni vita baina ya Waislaam na Wakrito wa Kijerumani, Waafrika Wakristo wa Songea walijiunga na Wakristo wenzao wa Kijerumani dhidi ya Waafrika wenzao wa Kiislam.

Wakristo wameitafiti hakika hii na wakaijua kisha wameificha kwa maslahi yao.




sina nia ya kuponda lakini kusema vita ya maji maji ilikuwa ya kidini hapo inafikirisha sana, hakika huyu mtu aliyeiandika hakufanya tafiti ya kutosha.
 
sina nia ya kuponda lakini kusema vita ya maji maji ilikuwa ya kidini hapo inafikirisha sana, hakika huyu mtu aliyeiandika hakufanya tafiti ya kutosha.
Just...
Nimefanya utafiti wa kutosha na nakuwekea kipande usome nimekitoa katika kitabu changu, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924- 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,'' Minerva Press, London 1998.

Kipande hicho hapo chini ni kutoka tafasiri ya Kiswahili:

''Ukristo ulipingwa na Waislam tokea mwanzo.

Katika kila pambano la silaha dhidi ya ukoloni, Waislam walichukua nafasi hiyo kuwashambulia wamishionari na taasisi zao.

Waislam waliwaona wamishionari na wakoloni kama washirika wakishirikiana kupiga vita Uislam na kwa hiyo wote ni maadui.

Ukakamavu wa Uislam dhidi ya ukoloni na Ukristo una historia ndefu.

Kanisa likawa kama kibaraka likijikurubisha na kujinasibisha na ukoloni hata kuwa upande wakoloni dhidi ya majeshi ya wazalendo.

Kuelewa hali ya Uislam wakati ule, unahitaji kusoma barua iliyoandikwa na Nduna Abdulrauf Songea Mbano wakati alipokuwa akikusanya nguvu za raia wake dhidi ya majeshi ya Wajerumani na huku akijaribu kupata ushirika wa machifu wengine katika sehemu za kusini ya Tanganyika na ng'ambo ya Mto Ruvuma, Msumbiji. Barua hii aliyoandikiwa Sheikh, Sultan Mataka bin Hamin Massaninga inasema:

''Sultan Songea bin Ruuf anasema:

Kwa Sheikh Sultan Mataka bin Hamin Massaninga.
Asalaam Aleikum,

Ninakuletea barua kupitia Kazembe.

Tumepata amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa Wazungu lazima waondoke nchini.
Tupo katika kupigananao hapa.

Naamini tumeshapatana muda mrefu, (kwa hiyo) niletee wanao, ili tufanye ushirikiano.

Nilitaka kukuletea mifugo kama zawadi, lakini sipo katika hali ya kuweza kufanya hivyo, kwa kuwa vita ambavyo Mwenyezi Mungu amevitaka vinaendelea.

Niletee watumiaji bunduki mia moja, na niunge mkono katika kulivamia Boma (Songea).
Ninakuletea chupa ya Mtume Muhammad, ambayo ndani yake ipo nguvu ya kuwashinda Wazungu.

Usiwe na shaka nayo, ina uwezo mkubwa.
Tutakapoliteka Boma (Songea), tutakwenda kwenye vituo katika Nyasa pamoja, mimi na wewe.

Hivi sasa tusahau ugomvi wetu wa zamani.
Chupa hii, na daíwa, imeletwa na Chinyalanyala mwenyewe, kiongozi wa vita.

Ameleta vilevile kombe, na anakupa salamu nyingi.
Endapo watu wako watakuja, Chinyalanyala mwenyewe atafika na atakupa vitu vingi vilivyo vitukufu.

Hassan bin Ismail anakusalimu.
Salam nyingi,

Sultan Songea bin Ruuf.''

1653084061594.jpeg

Abdulrauf Songea Mbano
 
Kwa hiyo yule kinjekitIlie ngwale ni wa kutungwa kwenye historia mpya ya CCM...
 
Sema...
Tatizo la vitabu hivyo ni kuwa havina ukweli katika historia ya Tanganyika.
Waandishi wanaandika kwa kuchagua wanachokitaka si ukweli wa historia.
kweli kabisa...kama vita ya majimaji iko highly distorted as if walipigana wangoni tu, ilhali vita hiyo ilitapakaa karibia mikoa yote ya sasa (lidi, mtwara, mbeya,iringa,njombe rukwa na ruvuma yenyewe) lakini inavyoelezewa ni kama ilipiganwa songea tu
 
Kwenye swala la historia kila mtu anamtazamo wake kwa sababu kila kitu kipo kichwani kumbukumbu zenye ushahidi wa kweli ni chache akija mkristo ataweka yake na akija muislamu kadharika ataweka yake
 
Kwenye swala la historia kila mtu anamtazamo wake kwa sababu kila kitu kipo kichwani kumbukumbu zenye ushahidi wa kweli ni chache akija mkristo ataweka yake na akija muislamu kadharika ataweka yake
Alex,
''Kadhalika,'' si ''kadharika.''
Katika historia ya TANU kama kungekuwako na kitu miaka mingi kingeshawekwa hapa.

Mimi nimeandika historia ya wazee wangu vipi waliasisi African Association 1929 kisha Al Jamiatul Islamiyya 1933 na mwisho kuunda TANU 1954.

Historia hii ikafutwa.
Mwaka wa 1998 nikachapa kitabu hicho hapo chini kueleza historia ya jamii niliyotaka mimi.

Hakuna historia nyingine ya TANU zaidi ya hii.
Hata historai ya Mwalimu Nyerere haiwezi kushindanishwa na hii niliyoandika.

Soma kitabu cha Mwalimu kilichoandika na Prof. Shivji, Prof. Saida Othman na Dr. Ng'waza Kamatha tafuta ndani yake historia ya African Association na TANU.

African Association mwaka wa 1929 Nyerere ana umri wa miaka saba wala Abdul Sykes miaka mitano lakini baba yake ni mmoja wa waasisi wa African Association.

Njoo katika kuasisi TANU 1954.

Kadi No. ! Julius Nyerere na kadi hiyo kaiandika Ally Sykes (na kadi kachapa yeye Printpak kwe fedha zake), kadi No. 2 Ally Sykes na kadi No. 3 Abdul Sykes.

Historia ya TANU si ya ati ''kila mtu ana mtazamo wake,'' wala si jambo la mtazamo ni historia ambayo ina watu waliokuwapo katika nyakati hizo na wakafanya mambo kwa ushahidi.

Mchango wa Waislam ni mkubwa sana katika siasa za ukombozi wa Tanganyika kuanzia Maji Maji na ushahidi upo.

Wala huna haja ya wewe kujihisi unyonge kwa ajili ya hili.

Safari ya Nyerere UNO 1955 sherehe ya kumuaga imefanyika Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika jengo la Waislam.

Huu ndiyo ukweli wa historia.
Mkutano wa Kura Tatu umefanyika Parish Hall, Tabora ukumbi wa Kanisa Katoliki.

Huu ndiyo ukweli wa historia.

1653197091945.jpeg
 
Hivi hao Muslim's mashujaa wa vita vya majimaji walizaliwa waisilamu au walisimishwa na wakoloni wa kiarabu...
Remmy...
Ushauri wangu kwako ni kuwa jifunze historia ya ukoloni kwanza ndiyo utakuwa katika nafasi nzuri ya kujadili.
 
Historia ya Misheni ya Songea (Peramiho) haitokamilika kama hatoanza mwanzo kabisa wa safari yao huku Tanganyika.

Hawa ni Wakatoliki wa shirika la Benedictine lenye makao yake makuu huko Ujerumani kwenye nyumba iliyopewa jina la St. Ottilia.

Ni shirika la tatu la kikatoliki kuingia nchini wakitanguliwa na mashirika mengine mawili. Benedictine walifika kwanza Zanzibar mwaka 1888 baadaye wakaenda Pugu, Lindi, Nyangao, Lukuledi, Namupa, Ndanda na hatimaye walifika Songea.

Historia inalitaja eneo la Dar, Mahenge, Gairo, Iringa, Njombe, Ruvuma, Lindi na Mtwara hadi Mpaka bahari ya Hindi kuwa ni Jimbo la Zanzibar Kusini kwa wakati huo.
Mkuu umeanza kunitoa tongotongo
 
Hivi hao Muslim's mashujaa wa vita vya majimaji walizaliwa waisilamu au walisimishwa na wakoloni wa kiarabu...
Hawezi kujibu hili swali abadani.
Muislamu mweusi huwa anamuona na kumuabudu muarabu kama Mungu (mtakatifu).

Ukitaka kuyaamini haya zungumza lolote baya la kikoloni la muarabu uone kama kuna muislamu atakuwa upande wako
 
Back
Top Bottom