Mwenye Historia ya Umishenari Songea

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,482
14,346
Habari zenu Wadau wa Jamii forums? Hasa katika jukwaa hili la Historia ninawaomba sana mnisaidie kupata Historia ya umishenari Songea na vile vile Historia ya Vita vya Majimaji.

Nitafurahi sana Kama nitapata kwa lugha ya Kiswahili au hata kwa lugha ya Kiingereza. Ninaomba kupata historia kamili kama kuna Mdau anayo mojawapo au zote mbili.

Natanguliza Shukrani zangu kwenu 🙏
 
Habari zenu Wadau wa Jamii forums? Hasa katika jukwaa hili la Historia ninawaomba sana mnisaidie kupata Historia ya umishenari Songea na vile vile Historia ya Vita vya Majimaji. Nitafurahi sana Kama nitapata kwa lugha ya Kiswahili au hata kwa lugha ya Kiingereza. Ninaomba kupata historia kamili kama kuna Mdau anayo mojawapo au zote mbili.
Natanguliza Shukrani zangu kwenu 🙏
Manyanza,
Umetaka hstoria kamil ya Wamishionari Songea na hstoria ya Maji Maji.
Makala takuwa ndefu sana.

Lakini unaweza kusoma hstoria hii kwa urefu wake katka Google na kwengineko.
Nmekuwekea hapa makala ambayo kwa kifupi itakuonyesha msimamo wa Wamishionari kabla na baada ya Vita Vya Maji Maji:

KANISA NA VITA VYA MAJI MAJI

Hassan Ilunga Kapungu

ABDULRAUF SONGEA MBANO

JEMADARI WA VITA VYA MAJI MAJI 1905 - 1907

1652665039166.png

Abdulrauf Songea Mbano​

Nje kidogo ya mji wa Songea kuna kitongoji kinaitwa Mahenge, hapo kuna sehemu ya kumbukumbu ya vita vya Majimaji. Jambo kubwa la mahala hapo ni kaburi kubwa la halaiki ambamo askari zaidi ya sitini na… (sitini na saba) walizikwa kwa pamoja. Na kando ya kaburi hilo la pamoja kuna kaburi la Abdulrauf Songea Mbano ambae yeye alizikwa peke yake.

Kwa mara ya kwanza nilitembelea makumbusho hayo mwishoni mwaka 2007. Baada ya kusaini kitabu cha wageni na kulipa ada ya kituo muhudumu wa kituo hicho alitupa karatasi yenye orodha ya majina ya wale wote walionyongwa na kuzikwa hapo. Ukiitazama orodha hiyo na hasa ukiwa Mwislam jambo moja litakustuwa. Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam. Linaanza jina lake la Kiiislam, kisha kwenye mabano kuna jina la Kikristo na mwishoni linaishia jina la kiasili, mfano Abdulrahman [Dominic] Mputa Gama.

Muhudumu akatueleza kuwa hawa mashujaa wa vita vya Maji Maji kabla ya kunyongwa alikuwako padri ambae aliwabatiza na kuwapa majina ya Kikristo na baadae kunyongwa, wengi walibatizwa kwa hadaa kuwa wakibatizwa wataachiwa huru, wote katika hao walionyongwa walikuwa ni Waislam. Uzuri ni kwamba katika orodha hiyo kulikuwa na jina na sahihi ya yule padri aliyewabatiza, na kwa mkono wake [huyo padri] aliiyaandika hayo majina. Karatasi yenyewe ilihifadhiwa vizuri kwenye fremu ngumu ya kioo. Tuliomba kwa nguvu zote kupatiwa hiyo karatasi ya majina hata kwa kununua lakini haikuwezekana pamoja na kuwaona na kuwaona wakubwa wa kituo hicho. Niliporudi kwa mara ya pili mwezi July 2009 nilipata mstuko.

Karatasi iliyohifadhiwa kwenye fremu ngumu ya kioo, iliyokuwa na majina ya Kiislaam ya mashujaa wa vita vya Maji Maji, haikuwapo,na badala yake imewekwa karatasi nyingine ombayo ndani ya karatasi hiyo majina ya Kiislaam ya mashujaa hao wa vita vya Maji Maji yameondolewa na kuachwa majina ya ubatizo na yale ya kiasili tu, jina la padri, sahihi yake na wadhifa wake katika Kanisa Katoliki pia vimeondolewa na karatasi yenyewe haikuwa kwenye fremu ya kioo na ilikuwa katika fotokopi tu.

Nilimuuliza muhudu kulikoni? Akasema, “Songea pana mzee mmoja maarufu sana katika historia ya TANU na historia ya kuasisiwa Bakwata anaitwa kwa kifupi M. S. Mzee huyu ana binti yake ambaye ameolewa na Mzungu wa Kijerumani. Binti huyu na na mumewe wa Kijerumani walikuja hapa Songea matembezi. Hivyo kwa shinikizo la huyu mzee M.S. karatasi hiyo alipewa huyu Mzungu kwa ahadi kwamba anaipeleka Ujerumani na atairudisha. Hivyo ndivyo karatasi ile asilia ilivyotoweka. Kubwa katika karatasi ile ni ule ushahidi wa majina kuwa wote katika wale walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam, wengi katika hao walihadaiwa kuachwa huru hivyo wakabatzwa ispokuwa wachahe sana waligoma kama shujaa Abdulrauf Songea Mbano. Huyu kwa ushujaa wake wa kupambana na Wajerumani aligoma na akasumbua sana kiasi akanyongwa siku yake na peke yake na ndio sababu akazikwa peke yake.

Ukiingia ndani ya kinyumba cha ghorofa, unaanza kuona picha za mashujaa wa Maji Maji wakiwa wamevaa mavazi ya vita mithili ya mahujaji wanavyovaa Ihraam wakati wa hija. Kinachoongezeka kwao ni vilemba kichwani. Chini ya kila picha kuna jina la aliyekuwa kwenye picha ile. Ukipanda gorofani utaona silaha za kiajadi kama mikuki, pinde, ngao n.k. Kinachosisimua zaidi ni mavazi ya vita. Mavazi ya vita ya askari wa Maji Maji wengi walivaa kanzu za Kiislaam na vilemba. Jambo jingine linalosisimua ni kile ambacho watu wa kituo hicho wameandika ”rosary” hili ni jina la Kikristo, hasa la Kikatoliki, ni zile shanga ambazo huning’inia msalaba lakini unapotazama hicho kilichoitwa “rosary” utaona si “rosary,” bali ni tasbihi hasa ya Kiislaam yenye kupangika hasa shanga zake, 33, 33, 34. Maneno yaliyoandikwa kuelezea “rosary” hizo ambazo ni tasbihi ni:

“Hizi ni rosary ambazo wapiganaji wa majimaji walikuwa wakitumia KUTAMBIKA kabla ya kwenda vitani kwa kuamini kwamba zitawakinga na risasi.”

Ukweli ni kwamba hawa askari wa Maji Maji wengi walikuwa ni Waislaam hivyo hawakuwa WAKITAMBIKA bali walikuwa wakitumia tasbihi hizo kufanya dhikri kwa Allah kabla ya kwenda vitani. Midhali sisi Waislaam hatujawa tayari kuandika historia yetu kama Waislaam wanaotuandikia watapotosha na kupindisha na kutuzulia wanavyotaka. Hapo gorofani kuna jambo jingine la kusisimua. Kuna magudulia na makopo. Wameandika kuwa, haya ndio makopo ambayo askari wa Maji Maji walikuwa wakiyatumia KUNAWA kabla ya kwenda vitani [kushika udhu na sio kunawa] pia kwa kuamini kuwa maji hayo yatawakinga. Muhudumu alitueleza kuwa kumbukumbu nzuri na za kuaminika ziko Jimbo Kuu la Wakatoliki Peramiho.

Tulikwenda jimboni lakini hatufanikiwa kwa sababu za ki-urasimu tu.T ulitakiwa tupate kibali cha Askofu Mkuu. Hatukukipata. Kwa yale tuliyoyaona na kuyashudia yafuatayo:

Vita vya Maji Maji havikuwa ni vita vya kizalendo, kwamba wazalendo walikuwa wakipigania nchi yao. La vilikuwa ni vita vya Waislaam wakipigana na Wakristo wa Kijerumani waliovamia maeneo asilia ya Waislaam kwa lengo la kuuwa Uislam na kusimamisha Kanisa kwani mazingira yote utayoyaona ya mashujaa wa vita vya Maji Maji ni mazingira ya Kiislaam, kingine ni kwamba hukuti mahala yalipo makaburi ya askari wa Kijerumani ila katika miji ya Waislaam kama Kilwa, Bagamoyo n.k. Kwa nini wauliwe maeneo ya Waislaam tu?

Walifuata nini huko?

Kuna upotoshaji mkubwa sana wa historia ya vita vya Maji Maji. Vinaoneshwa kama ni vita vya wazalendo wakipigana na wakoloni wa Kijerumani, wakati ukweli si hivyo. Ukweli ni kwamba vita vya Maji Maji vilikuwa ni vita baina ya Waislaam na Wakrito wa Kijerumani, Waafrika Wakristo wa Songea walijiunga na Wakristo wenzao wa Kijerumani dhidi ya Waafrika wenzao wa Kiislam.

Wakristo wameitafiti hakika hii na wakaijua kisha wameificha kwa maslahi yao.

Natanguliza Shukrani zangu kwenu
Nenda library, Kasome kitabu Cha Historia Cha darasa la Tano miaka ya 1980-1990 utapata hivyo vitu unataka
Ukikosa nicheck inbox
 
Manyanza,
Umetaka hstoria kamil ya Wamishionari Songea na hstoria ya Maji Maji.
Makala takuwa ndefu sana.

Lakini unaweza kusoma hstoria hii kwa urefu wake katka Google na kwengineko.
Nmekuwekea hapa makala ambayo kwa kifupi itakuonyesha msimamo wa Wamishionari kabla na baada ya Vita Vya Maji Maji:

KANISA NA VITA VYA MAJI MAJI

Hassan Ilunga Kapungu

ABDULRAUF SONGEA MBANO

JEMADARI WA VITA VYA MAJI MAJI 1905 - 1907

View attachment 2226369

Interesting. Kama ipo Shehe wangu naiomba hata kama itakuwa ndefu vipi. Kama ni file la PDF unaweza ukanitumia kwenye email. manyanza@jamiiforums.com
 
Mleta mada soma hiyo...
 
Mzee utawafelisha watoto kwenye mitihani yao kwa historia zako ambazo hazina vyanzo vya kuaminika
Huko shule ya nikishatoka miaka ya 2005 nahitaji hizo historia kwa ajili ya mambo mengine naomba ambaye anazo full package anisaidie
 
Lupweko,
Mimi sina historia iliyo yangu.
Historia ni kama ilivyotendwa na wahusika hao ndiyo wenye historia yao.

Wala vitabu nilivyoandika mimi haviko katika mtaala kwa hiyo hakuna mwalimu anaesomesha kitabu changu katika shule za Tanzania kwa hiyo uwezekano wa mwanafunzi kufeli mtihani haupo kabisa.

Labda tuzungumze historia ya Maji Maji na yale ambayo mimi nimeyasahihisha katika historia hiyo na nitakuwekea ushahidi.

Majemadari wa Maji Maji walionyongwa na Wajerumani na kuzikwa katika kaburi la halaiki isipokuwa mmoja Songea Mbano ambae jina lake khasa ni Abdulrauf Songea Mbano.

Katika hao walionyongwa yuko mwanamke mmoja ambae siku zote anatambulishwa kwa jina moja tu la Mkomanile.

Jina lake huyu mama ni Khadija.
Jiulize kwa nini majina ya Kiislam yameondolewa kwa hawa mashujaa?

Majemadari hawa wote walikuwa Waislam na walipopitishiwa hukumu ya kunyongwa Father Johannes kutoka Peramiho aliwaendelea na kuwaambia kuwa endapo wataukana Uislam na kuwa Wakristo hukumu ya kuuliwa itafutwa.

Father Johannes wa Peramiho akawabatiza baadhi na kuwapa majina ya Kikristo.

Ukisoma majina ya hawa yaliyoandikwa katika mnara wa kumbukumbu ya Maji Maji, Mahenge, Songea utaona majina yao ya Kiislam hayapo yameandikwa majina ya Kikristo.

Ushahidi wa haya unatokana katika utafiti niliofanya na mwingine katika haya ninayokueleza hapo juu upo katika kitabu cha Prof. James Giblin kuhusu Maji Maji: ''Lifting the Fog of War,'' (2010).

Kuwa vyanzo vyangu haviaminiki si kweli.
Usijipotezee nafasi ya kujifunza kwa hofu isiyokuwa na sababu.

Ama kuhusu kufeli wanafunzi hawa wamashafelishwa kwa kusomeshwa historia iliyoandikwa kwa ghilba.

Nakuwekea hapo chini picha ya Prof. Giblin niliyompiga ofisini kwake University of Iowa akiwa ameshika kitabu cha Abdul Sykes.

Prof. Giblin ni mwalimu wa African History chuoni hapo.
Huu ni mwaka wa 2011.

PICHA:
1. Prof. James Giblin.
2. Mnara wa kumbukumu wa majemadari 66 wa Maji Maji walionyongwa na Wajerumani hapo penye mnara ndipo lilipo kaburi lao.
3. Kaburi la Abdulrauf Songea Mbano
4. Abdulrauf Songea Mbano ambae wanahistoria wameruka jina lake la Kiislam ''Abdulrauf'' na kubakisha, ''Songea Mbano.''

Screenshot_20220516-145949_Facebook.jpg
 
Thread za kidini hua zinatia uvivu sana kusoma.
Sijui ni mm tu au na ww ?
Nasema uongo ndugu zangu.
1gb,
Kwanza nataka nikufamisha kitu.

Kuandika historia ya Waislam kama sehemu ya jamii Tanganyika ambayo ina historia ya pekee katika kupambana na wakoloni na ukoloni si udini.

Hii ni historia.

Mfano Wakikuyu Kenya mchango wangu katika kupambana na ukoloni wa Waingereza ni wa kipekee.
Wakikuyu walinyayua silaha kuiokomboa Kenya.

Kuandika historia ya Wakikuyu si ukabila.

Hii mosi.
Lakini pili tuchukue kuwa wewe hupendezewi na historia hii ninayoandika hapa JF.

Unachotakiwa kujifanyia ni kuacha kunisoma.
Hili si jambo zito kufanya.

Huna sababu ya kutaka wasomaji wengine wakuunge mkono katika kile unachoamini wewe.

1652703573561.png
 
Habari zenu Wadau wa Jamii forums? Hasa katika jukwaa hili la Historia ninawaomba sana mnisaidie kupata Historia ya umishenari Songea na vile vile Historia ya Vita vya Majimaji.

Nitafurahi sana Kama nitapata kwa lugha ya Kiswahili au hata kwa lugha ya Kiingereza. Ninaomba kupata historia kamili kama kuna Mdau anayo mojawapo au zote mbili.

Natanguliza Shukrani zangu kwenu 🙏
Ninayo machache lakini napata taabu kuyaandika hapa.
 
Na pia mtoa mada kama upo nchini hapa,pls nenda mwenyewe pale Songea na Pata habari za ukweli, tembelea pale Peramiho mission upate upande wao na tembelea mahenge, mpitimbi, likuyu fusi, Bombambili, lumecha etc etc,na mwishowe karibu Hulu Lingusenguse
 
Historia ya Misheni ya Songea (Peramiho) haitokamilika kama hatoanza mwanzo kabisa wa safari yao huku Tanganyika.

Hawa ni Wakatoliki wa shirika la Benedictine lenye makao yake makuu huko Ujerumani kwenye nyumba iliyopewa jina la St. Ottilia.

Ni shirika la tatu la kikatoliki kuingia nchini wakitanguliwa na mashirika mengine mawili. Benedictine walifika kwanza Zanzibar mwaka 1888 baadaye wakaenda Pugu, Lindi, Nyangao, Lukuledi, Namupa, Ndanda na hatimaye walifika Songea.

Historia inalitaja eneo la Dar, Mahenge, Gairo, Iringa, Njombe, Ruvuma, Lindi na Mtwara hadi Mpaka bahari ya Hindi kuwa ni Jimbo la Zanzibar Kusini kwa wakati huo.
 
Kutoka sehemu iliyoitwa wakati ule Apostolic Vicariate of South Zanzibar, baadaye maeneo ya kusini pamoja na huko Ruvuma ikawa sehemu ya jimbo la kitume Lindi. Hii ni mwaka 1913.

Dec 1931 Idara ya Uenezi Imani ya Roma iliamua kuligawanya eneo kubwa la Lindi katika Abbasia Mbili, yaani Abasia ya Ndanda na Peramiho.
 
Vita vya Maji Maji havikuwa ni vita vya kizalendo, kwamba wazalendo walikuwa wakipigania nchi yao. La vilikuwa ni vita vya Waislaam wakipigana na Wakristo wa Kijerumani waliovamia maeneo asilia ya Waislaam kwa lengo la kuuwa Uislam na kusimamisha Kanisa kwani mazingira yote utayoyaona ya mashujaa wa vita vya Maji Maji ni mazingira ya Kiislaam, kingine ni kwamba hukuti mahala yalipo makaburi ya askari wa Kijerumani ila katika miji ya Waislaam kama Kilwa, Bagamoyo n.k. Kwa nini wauliwe maeneo ya Waislaam tu?
Mzee hao unaowaita waislamu kupigana na hao unaowaita wakristo wa kijerumani waliupataje huo uslamu wao?
 
Back
Top Bottom