Mwenye CV ya Charles Kitwanga (Kipengele cha Education) anipe

Status
Not open for further replies.
Ndio tatizo lenu wabongo, msimjue mtu hata kidogo inakuwa nongwa. Kama aliweza kuanzisha kampuni na ikasimama na kutoa ajira basi anafaa manake kuna babu zenu wako bungeni toka uhuru lakini hawana hata duka la kuajiri watu wawili na katika payroll wanaondoka na 7digits kitambo.

Mapungufu kila mtu anayo hata wewe unayo, lakini isiwe ndio sababu ya kusimamia vidole gumba kuleta utata.

Hoja ni kuwa tuliahidiwa kuletewa watu waadilifu.

Kuwa na kampuni ya kuajiri watu na kuwalipa kwa payroll siyo kipimo cha uadilifu.

bado ume-divert hoja.

tuendelee na mada.
 
changia mada. usianzishe mada ndani ya mada.

peleka madai yako kwenye jukwaa la udaku.

hapa tunajadili ishu sirias

Kwani hili la kupeana uongozi kwa kutumia udini, ukabila, ukanda na ukoo sio seriouss ? Duh kweli waona jua mchana kweupee wasema huo ni mwezi.
 
Hizi ni chuki binafsi tu hapa. wivu na uzushi. Jerusalemu acha hizo. Tuletee mawazo ya kujenga nchi sio ulalamishi tu!!!!! you are expected to be a great thinker...!!!
 
chadema kila mtu bungeni ameenda na ukoo wake , hasa hasa wakina ndesamburo, mbowe nk. kila mtu ametoa viti maalum kwa watoto wake, wakwe, wajomba n. Hiki ni chama cha siasa kweli au kikabila? kweli 'kila mtu na wake kwa chadema'

:target:
 
Ni mtu wa hongo.

mtu wa mlungula

mtu wa kitu kidogo

alikuwa mwenyekiti wa ERB pamoja na kwamba kampuni yake ametimua wahandisi wote wenye akili na uwezo.

alikuwa mwenyekiti wa ERB lakini muda wote kulikuwa na hadithi za kweli za maghorofa kuvunjika. yeye ilimradi umpe kitu kidogo poa tu. hata ujenge ghorofa kwa nondo za fito au kwa matope poa tu.

Tz tumekwisha.

Who the hell is he mpaka bifu zake binafsi za kiuendeshaji wa kampuni unazileta hapa?
 
Hizi ni chuki binafsi tu hapa. wivu na uzushi. Jerusalemu acha hizo. Tuletee mawazo ya kujenga nchi sio ulalamishi tu!!!!! you are expected to be a great thinker...!!!

nitasema kweli daima, fitna kwangu mwiko.

huyu askari wa mwavuli wa JK si chaguo sahihi kwa WaTz.

Atafanya kazi ya kuponya majeraha

kujilimbikizia mali kulipiza pesa yake binafsi aliyotumia kusaka ubunge tangu 2005
badala ya kulitumikia taifa

amepewa uwaziri kireja-reja ili arudishe pesa yake kirahisi.

ni maoni yangu tu.

lakini nashawishika kusema yana ukweli.

simsingizii. ni kweli tupu.
 
chadema kila mtu bungeni ameenda na ukoo wake , hasa hasa wakina ndesamburo, mbowe nk. kila mtu ametoa viti maalum kwa watoto wake, wakwe, wajomba n. Hiki ni chama cha siasa kweli au kikabila? kweli 'kila mtu na wake kwa chadema'

Mbona sielewi ,haya yanaingiaje hapa jamani? Duh!!!!
 
Nakumbuka sana. JK wakati anaanza kuitwa Rais (kwa sifa na majivuno, si kwa utendaji) alijigamba serikali yake 'haina ubia na mtu'. akaendelea zaid kusema ufike wakati wa 'kutenganisha biashara na siasa'

Sass huyu JK? Vipi?

Mbona Kitwanga aka Mawe Matatu ni mfanya biashara? Mbona amempa uwaziri? Au ndiyo kupozana? Kwa sababu 2005 alimwagwa kwenye kura za maoni?

Eeeh? Nauliza.

JK huyuhuyu hivi majuzi alikuja na staili ya kuwa atatuchagulia mawaziri 'waadilif na wachapakazi'. Vipi? Mbona Kitwanga siyo muadilifu? Mtu aliyevuruga kampuni aliyoanzisha na wenzake anafaa vipi kuwaongoza WaTz? Amesababisha kampuni kupoteza ma-Engineer na kupoteza wateja wakubwa kama NMB? Amesababisha mmoja wa wakrugenzi walioanzisha kampuni kujitoa licha ya mkurugenzi huyo kusaidia kupiga debe k=kampuni kupewa hadhi ya kuwa wakala wa DELL Tanzania? Kama ameshindwa kuongoza kampuni ya watu wasiozidi 100 ataweza Wizara inayotazamwa na WaTz 4 000 000?

Kama kuna uteuzi wenye utata uliofanywa na JK ni huu wa kumpa Kitwanga wizara. Ni urafiki na kujuana tu. Amempa ili iwe rahisi kupata tenda za kuuza computer za DELL kwenye taasisi za serikali....siasa na biashara damdam.

Hapo tu huwa simuamini JK.
sijakuelewa... umeandika kama vile wote tuko kichwani mwako

details please maana inaonekana unamjua
 
kichwa habari kizuri sana, nilifikiri unaandika jinsi wabunge wa chadema kila mmoja alivyoenda bungeni na wake. Kama siyo mke basi ni mtoto au mkwe au hawara na limahamsha hasira sana kwa sisi wanawake wa chadema. Tume ya uchaguzi imekaa kimya wala haikemei jambo hilo la vigogo chadema kuchakachua hilo.

vigezo viliwekwa na kutangazwa, kama hukutimiza isiwe nongwa. Hata sisi mitaani hatugombei kwa kuwa baadhi ya vigezo hatunavyo. Uongozi sio kitu cha kukimbilia. Kuana nini huko?
 
Mkuu Pasco,jengo zuri lililopo Msasani Beach ni Info-tech House...linamilikiwa na Mufuruki... Hilo la Infosisy ni lipi?
 
Anarudi tena, hivi uadilifu wa mtu unapimwa kwa umasikini?.
Infosys ni moja ya makampuni yenye mafanikio makubwa kutokana na kuwa ndio sole agent wa Dell, na miradi yote inayofadhiliwa na Benki ya Dunia, computers lazima ziwe Dell.

Nijuavyo mimi, Kitangwa ni mmoja wa wakurugenzi, yeye ni mwajiriwa wa BOT. Kaka yake ni Singili mwenye Azania Bank, jamaa wana mafanikio sana kwenye kila wanapokanyaga, hebu angalieni lile jengo lao pale Msasani Beach lilivyo kivutia!.

Hakuna ubishi, Tanzania ni nchi masikini, na Watanzania wengi tunaishi kwa lindi la umasikini uliotopea, hii isitufanye kijenga chuki na kila mwenye nacho, simply because wengine hatuna.
Naamini mafanikio ya Infosys sasa yanahamishiwa pale wizarani.

kumbe ni mali ya mtu, nilikuwa nazani ni ya serekali.
 
Mkuu Pasco,jengo zuri lililopo Msasani Beach ni Info-tech House...linamilikiwa na Mufuruki... Hilo la Infosisy ni lipi?

Hajui Jiji huyo.

Achana naye.

Twende kwenye mada.

Urafiki huu wa JK na watu wake kwenye masuala ya uongozi wa nchi utatufikisha wapi?
 
kumbe ni mali ya mtu, nilikuwa nazani ni ya serekali.

Naunga mkono hoja.

Ndiyo benki ambayo wahujumu uchumi hasa kwenye ishu za ujenzi hupitishia pesa.

huwezi kuamini. mtu alipewa kujenga barabara wilaya fulani wakati hana hata greda. vyote vya kukodi. Wakati huo ERB iko chini ya uenyekiti wa huyu anayeitwa mawe ma3.

pesa ya ujenzi ilipitia Azania Bancorp.

Made in JK.
 
wewe una maslahi binafsi na kitwanga.

kama angekuwa na hizo sifa unazompatia asingepoteza mktaba na nmb

kama angekuwa na hizo sifa unazompatia asingepigwa chini kura za maoni mwaka 2005. kwa vyovyote vile safari hii katoa mlungula kupenya kura za maoni, siyo kama anakubalika.

awe na pesa asiwe nazo is none of our business.

where are the morals?
Jerusalemu, sina maslahi yoyote binafsi na Kitwanga, nimekuelimisha tuu kuwa yeye ni muajiriwa BOT, tafuta track record yake kazini kwake. Infisys ni mradi tuu na ulikuwa na waendeshaji.

Kukosa tenda ya NMB ni kuzidiwa kibiashara ambalo ni jambo la kawaida kwenye ushindani, kama wewe umwahi kumiliki kampuni, utanielewe what does it take kushinda hizi tenda kubwa kubwa.

Morals is something else, sasa kama unataka tumjadili on morals standards na sio mafanikio yake, ungesema na ungeanza na hizo moral standards za aliyemteua.

Tukiamua kudiscredi mtu, tumdiscredit with facts sio with feelings, itaishia kuonekana ni chuki binafsi tuu, dhidi ya mafanikio yao.

Mengi ya majengo marefu ya mjini tunayayaona, yanamilikiwa na wenzetu wenye asili fulani!, mswahili ngozi nyeusi akifanikiwa na kushuka ile kitu kama kina Kitwanga waliyoishusha pale Msasani beach, basi mane ndio yanaanza, sasa kateuliwa ndio basi!, hii haisadii katika kujenga nchi yetu.

Kama unazon tuhuma zake zozote zimmwage, usiishie kulalama.
 
Nakumbuka sana. JK wakati anaanza kuitwa Rais (kwa sifa na majivuno, si kwa utendaji) alijigamba serikali yake 'haina ubia na mtu'. akaendelea zaid kusema ufike wakati wa 'kutenganisha biashara na siasa'

Sass huyu JK? Vipi?

Mbona Kitwanga aka Mawe Matatu ni mfanya biashara? Mbona amempa uwaziri? Au ndiyo kupozana? Kwa sababu 2005 alimwagwa kwenye kura za maoni?

Eeeh? Nauliza.

JK huyuhuyu hivi majuzi alikuja na staili ya kuwa atatuchagulia mawaziri 'waadilif na wachapakazi'. Vipi? Mbona Kitwanga siyo muadilifu? Mtu aliyevuruga kampuni aliyoanzisha na wenzake anafaa vipi kuwaongoza WaTz? Amesababisha kampuni kupoteza ma-Engineer na kupoteza wateja wakubwa kama NMB? Amesababisha mmoja wa wakrugenzi walioanzisha kampuni kujitoa licha ya mkurugenzi huyo kusaidia kupiga debe k=kampuni kupewa hadhi ya kuwa wakala wa DELL Tanzania? Kama ameshindwa kuongoza kampuni ya watu wasiozidi 100 ataweza Wizara inayotazamwa na WaTz 4 000 000?

Kama kuna uteuzi wenye utata uliofanywa na JK ni huu wa kumpa Kitwanga wizara. Ni urafiki na kujuana tu. Amempa ili iwe rahisi kupata tenda za kuuza computer za DELL kwenye taasisi za serikali....siasa na biashara damdam.

Hapo tu huwa simuamini JK.

Jerusalemu tuchambue hoja hoja kwa hoja. Hujasema kwamba huyu bwana Kitangwa amesababishaje hadi hao ma-engineer kuondoka, je sababu ya uongozi wake mbaya, au yeye alikuja na sera ya kubana matumizi kwa hiyo hao ma-engineer wakaamua kuondoka baada ya kuona mafao haya toshi?

Kitu ambacho mtoa hoja anatakiwa kufahamu kwenye hizi kampuni zinazofanya kazi za aina hii ya infosisy, hawa ma-engineer wanaweza wakawa wanafanya contact na wateja nje ya utaratibu wa kampuni japo huwa wanatumia vifaa vya ofisi, hapo wao wanapata mapato zaidi lakini kwa upande huo huo wanaiumiza kampuni. Sasa anapokuja meneja mpya na akaziba huo ufa, automatically wale waliozoea tabia hiyo lazima watakimbia sababu mifereji yao imeziba kwa hiyo kukimbia kwa ma-engineer baada ya kuingia meneja mpya sio kipimo sahihi cha ubovu wa Meneja.

Ni vema mtoa mada kwa sababu unaonekana unamfahamu vizri huyu jamaa ungeainisha weziwazi wapi ulipo ukosefu wa maadili kwa huyu jamaa mteule wa rais
 
wewe una maslahi binafsi na kitwanga.

kama angekuwa na hizo sifa unazompatia asingepoteza mktaba na nmb

kama angekuwa na hizo sifa unazompatia asingepigwa chini kura za maoni mwaka 2005. kwa vyovyote vile safari hii katoa mlungula kupenya kura za maoni, siyo kama anakubalika.

awe na pesa asiwe nazo is none of our business.

where are the morals?

Kupoteza mkataba na benki hakumaanishi wewe si muadilifu au si mtendaji. Kunatokana na kutoridhiana kwa pande mbili mteja na msambazaji. Pengine walitoa terms ambazo yeye Charles hakuridhika nazo sasa tatizo lipo wapi? Acha chuki binafsi ndugu lete data zaidi ameiba mahali, ameboronga mahali (kiutendaji), amepokea rushwa sehemu (hasa kama data unazo). Si kuzusha ndugu otherwise wewe sema unasikia tetesi anapokea kitu kidogo lakini sio kumhukumu mkuu.

Tuacheni chuki binafsi jamani
 
Jerusalemu tuchambue hoja hoja kwa hoja. Hujasema kwamba huyu bwana Kitangwa amesababishaje hadi hao ma-engineer kuondoka, je sababu ya uongozi wake mbaya, au yeye alikuja na sera ya kubana matumizi kwa hiyo hao ma-engineer wakaamua kuondoka baada ya kuona mafao haya toshi?

Kitu ambacho mtoa hoja anatakiwa kufahamu kwenye hizi kampuni zinazofanya kazi za aina hii ya infosisy, hawa ma-engineer wanaweza wakawa wanafanya contact na wateja nje ya utaratibu wa kampuni japo huwa wanatumia vifaa vya ofisi, hapo wao wanapata mapato zaidi lakini kwa upande huo huo wanmaumiza kampuni. Sasa anapokuja meneja mpya na akaziba huo ufa, automatically wale waliozoea tabia hiyo lazima watakimbia sababu mifereji yao imeziba kwa hiyo kukimbia kwa ma-engineer baada ya kuingia meneja mpya sio kipimo sahihi cha ubovu wa Meneja.

Ni vema mtoa mada kwa sababu unaonekana unamfahamu vizri huyu jamaa ungeainisha weziwazi wapi ulipo ukosefu wa maadili kwa huyu jamaa mteule wa rais

kama kuna kampuni inaongoza kwa ku-hire na ku-fire mameneja, hakuna nyingine. ni hii ya mawe ma3. muulizeni kati ya 2000 na 2010 kaajiri mameneja wangapi? ana kauli mbiu yake: "we can hire anybody by any cost". hii ni kauli ya kinyanyasaji. unyanyasaji kwa kuwa yeye ana pesa. anataka watu wafunge midomo. wasidai haki. huyu mzee bwana, dah!

siyo kiongozi wa kustahili kupewa uwaziri.

hapo ninadiriki kumkosoa JK nikiwa kifua mbele.

JK inabidi anisikilize. kama alivyosikiliza maoni ya wadau. akamtosa mama meghji ishu ya uwaziri. licha ya kumbatiza jina la 'mwanamke chuma'. hata mimi ni mdau. JK nisikilize.
 
kama kuna kampuni inaongoza kwa ku-hire na ku-fire mameneja, hakuna nyingine. ni hii ya mawe ma3. muulizeni kati ya 2000 na 2010 kaajiri mameneja wangapi? ana kauli mbiu yake: "we can hire anybody by any cost".

Acha chuki binafsi ndugu lete data kumdiscredit badala kulazimisha JK akusikilize au mzee unampigia debe mtu wako nini ashike nafasi yake?
 
kama kuna kampuni inaongoza kwa ku-hire na ku-fire mameneja, hakuna nyingine. ni hii ya mawe ma3. muulizeni kati ya 2000 na 2010 kaajiri mameneja wangapi? ana kauli mbiu yake: "we can hire anybody by any cost".

siyo kiongozi wa kustahili kupewa uwaziri.

Swali moja zaidi, je hivyo vigezo vya kuwa-fire mameneja viko wazi?? Ninachoelewa ni kwamba kwa kampuni kama infosisy inakabiliwa na competition kubwa na inakuwa vigumu kumvumilia meneja ambaye anashindwa ku-meet target, mkuu kama umewahi kumiliki kampuni hili unaeza ukalielewa vizuri.

Jamaa atakuwa si muadilifu akama atakuwa anafukuza watu bila kuwalipa stahiki zao au kuwafukuza bila kuwepo kwa vigezo vya wazi. na ni mbaya zaidi kama atakuwa anatumia rushwa kuifluence kupata tenda kubwa kubwa za makampuni au za serikali.

Labda kama unadetails za wrong-doing events zozote, uziweke otherwise hoja hii itaonekana kama ni kumsakama tu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom