Mwenye CV ya Charles Kitwanga (Kipengele cha Education) anipe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenye CV ya Charles Kitwanga (Kipengele cha Education) anipe

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Ng'wanangwa, Nov 24, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa ni full majungu na ni fisadi kiaina.

  Kada wa CCM. Mtumishi wa Benki Kuu. Amevuruga kampuni waliyoanzisha watu wanne kiasi kwamba sasa ina hali mbaya. Wahindi wameipiga bao. Kupewa Wizara ni njia ya kumsaidia kurudisha pesa yake aliyofilisi kampuni aliyobuni na wenzake. Wala siyo muadilifu kama tulivyopotoshwa na JK. Ana lake jambo.

  Pia ni swahiba wa Pombe (J. Magufuli).

  Haiwezekani kuingia tu bungeni na kuwa Naibu Waziri. Kwani yeye nani?

  Naomba CV yake.
   
 2. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Dk. Terezya Luoga-Hovisa
  Kassim Majaliwa
  Gregory Teu
  Pereira Ame Silima
  Omary Nundu
  Gerson Lwinge
  Dk. Haji Hussein Mpanda.
  Hao wote ni wapya katika Bunge na kwenye wizara pia.Labda kama ina mengine ila hoja ya kuwa Mawe Matatu kaingia tu na kupewa unaibu haina mshiko.
  anaweza kuwa alipimwa kwa utendaji mzuri akiwa Bodi ya wakandarasi kama mwenyekiti na huko BOT.
  Kuhusu hiyo company ni ipi?kama Ni Infosys naona bado iko poa na inapiga kazi NBC hadi sasa.
   
 3. eliesikia

  eliesikia JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2010
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 423
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Hoja nyingine hazina msingi.... Watu kibao ni wapya...
  Kitwanga ni msomi wa chuo kikuu dar 1987 Bsc Computing Science n Maths.... Amefanya sana kazi benki kuu kama mdogo hadi kuwa bosi kwa awamu pale IT department...
  Kuhusu infosys ni nzima watu wameenda kufanya biashara na ni ma-agent wa kuaminika wa dell....
  Kuhusu uzoefu... Mpaka sasa ni mwenyekiti wa CRB (Contractors Reg Board)
   
 4. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2010
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ahsante Mkuu Eliesikia. Hiyo short profile ya Charles ni sahihi kabisa.
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Watu mna hasira na hawa wapya!
  Hamjui walienda safisha nyota kwa yahya
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka sana. JK wakati anaanza kuitwa Rais (kwa sifa na majivuno, si kwa utendaji) alijigamba serikali yake 'haina ubia na mtu'. akaendelea zaid kusema ufike wakati wa 'kutenganisha biashara na siasa'

  Sass huyu JK? Vipi?

  Mbona Kitwanga aka Mawe Matatu ni mfanya biashara? Mbona amempa uwaziri? Au ndiyo kupozana? Kwa sababu 2005 alimwagwa kwenye kura za maoni?

  Eeeh? Nauliza.

  JK huyuhuyu hivi majuzi alikuja na staili ya kuwa atatuchagulia mawaziri 'waadilif na wachapakazi'. Vipi? Mbona Kitwanga siyo muadilifu? Mtu aliyevuruga kampuni aliyoanzisha na wenzake anafaa vipi kuwaongoza WaTz? Amesababisha kampuni kupoteza ma-Engineer na kupoteza wateja wakubwa kama NMB? Amesababisha mmoja wa wakrugenzi walioanzisha kampuni kujitoa licha ya mkurugenzi huyo kusaidia kupiga debe k=kampuni kupewa hadhi ya kuwa wakala wa DELL Tanzania? Kama ameshindwa kuongoza kampuni ya watu wasiozidi 100 ataweza Wizara inayotazamwa na WaTz 4 000 000?

  Kama kuna uteuzi wenye utata uliofanywa na JK ni huu wa kumpa Kitwanga wizara. Ni urafiki na kujuana tu. Amempa ili iwe rahisi kupata tenda za kuuza computer za DELL kwenye taasisi za serikali....siasa na biashara damdam.

  Hapo tu huwa simuamini JK.
   
 7. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Kujuana na kulindana ndio msingi wa kupata viongozi hapa kwetu...kazi tunayo wacha tupiganie katiba mpya..
   
 8. The Good

  The Good Senior Member

  #8
  Nov 26, 2010
  Joined: May 26, 2010
  Messages: 152
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ukisoma btn lines inaonekana kuna maswala binafsi hapa.
   
 9. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Lakini unakiri kimsingi kuwa jamaa siyo muadilifu, kinyume na tulivoahidiwa na JK
   
 10. A

  Anaruditena Member

  #10
  Nov 26, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Charles, sio mwadilifu kabisa katika nyanja zote - ni mmoja wa wamiliki wa Infosys. Wizi mtupu. Naibu waziri mawasiliano na sayansi na Teknlojia!
   
 11. k

  kalikenye JF-Expert Member

  #11
  Nov 26, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 1,616
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  He!! Yamekuwa hayo tena. Atawezaje kutenganisha masilahi yake binafsi na mamlaka aliyopewa.
   
 12. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #12
  Nov 26, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Ni mtu wa hongo.

  mtu wa mlungula

  mtu wa kitu kidogo

  alikuwa mwenyekiti wa ERB pamoja na kwamba kampuni yake ametimua wahandisi wote wenye akili na uwezo.

  alikuwa mwenyekiti wa ERB lakini muda wote kulikuwa na hadithi za kweli za maghorofa kuvunjika. yeye ilimradi umpe kitu kidogo poa tu. hata ujenge ghorofa kwa nondo za fito au kwa matope poa tu.

  Tz tumekwisha.
   
 13. N

  Nakwetu Member

  #13
  Nov 26, 2010
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kichwa habari kizuri sana, nilifikiri unaandika jinsi wabunge wa Chadema kila mmoja alivyoenda bungeni na wake. Kama siyo mke basi ni mtoto au mkwe au hawara na limahamsha hasira sana kwa sisi wanawake wa Chadema. Tume ya uchaguzi imekaa kimya wala haikemei jambo hilo la vigogo Chadema kuchakachua hilo.
   
 14. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #14
  Nov 26, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Mods muangalieni huyu mdau.

  Anataka kupotosha mada.

  anataka kufunika kombe. mwanaharamu (kitwanga) apite (uache kumjadili).

  majibu yako hayana maslahi kwa taifa. hoja yangu ina maslahi kwa taifa

  tuendelee na mada tafadhali.
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Nov 26, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,537
  Trophy Points: 280
  Anarudi tena, hivi uadilifu wa mtu unapimwa kwa umasikini?.
  Infosys ni moja ya makampuni yenye mafanikio makubwa kutokana na kuwa ndio sole agent wa Dell, na miradi yote inayofadhiliwa na Benki ya Dunia, computers lazima ziwe Dell.

  Nijuavyo mimi, Kitangwa ni mmoja wa wakurugenzi, yeye ni mwajiriwa wa BOT. Kaka yake ni Singili mwenye Azania Bank, jamaa wana mafanikio sana kwenye kila wanapokanyaga, hebu angalieni lile jengo lao pale Msasani Beach lilivyo kivutia!.

  Hakuna ubishi, Tanzania ni nchi masikini, na Watanzania wengi tunaishi kwa lindi la umasikini uliotopea, hii isitufanye kijenga chuki na kila mwenye nacho, simply because wengine hatuna.
  Naamini mafanikio ya Infosys sasa yanahamishiwa pale wizarani.
   
 16. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #16
  Nov 26, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,597
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  Anzisha thread yako , tumia akili kidogo tu!
   
 17. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #17
  Nov 26, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  wewe una maslahi binafsi na kitwanga.

  kama angekuwa na hizo sifa unazompatia asingepoteza mktaba na nmb

  kama angekuwa na hizo sifa unazompatia asingepigwa chini kura za maoni mwaka 2005. kwa vyovyote vile safari hii katoa mlungula kupenya kura za maoni, siyo kama anakubalika.

  awe na pesa asiwe nazo is none of our business.

  where are the morals?
   
 18. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #18
  Nov 26, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  chadema kila mtu bungeni ameenda na ukoo wake , hasa hasa wakina ndesamburo, mbowe nk. kila mtu ametoa viti maalum kwa watoto wake, wakwe, wajomba n. Hiki ni chama cha siasa kweli au kikabila? kweli 'kila mtu na wake kwa chadema'
   
 19. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #19
  Nov 26, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  changia mada. usianzishe mada ndani ya mada.

  peleka madai yako kwenye jukwaa la udaku.

  hapa tunajadili ishu sirias
   
 20. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #20
  Nov 26, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,018
  Trophy Points: 280
  Ndio tatizo lenu wabongo, msimjue mtu hata kidogo inakuwa nongwa. Kama aliweza kuanzisha kampuni na ikasimama na kutoa ajira basi anafaa manake kuna babu zenu wako bungeni toka uhuru lakini hawana hata duka la kuajiri watu wawili na katika payroll wanaondoka na 7digits kitambo.

  Mapungufu kila mtu anayo hata wewe unayo, lakini isiwe ndio sababu ya kusimamia vidole gumba kuleta utata.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...