Mwenye auditing firm, au mfunga mahesabu Arusha aniokoe

Mwenye auditing firm, au mfunga mahesabu Arusha aniokoe

Adrian2716

Member
Joined
Oct 23, 2023
Posts
98
Reaction score
293
salamu wakuu, mwenye hiyo sehemu arusha tafadhali anisaidie japo kikazi kidodogo nipate hata mlo wa mchana tu

Nina degree ya Accounting and Finance
 
Mkuu pole kwa changamoto ya kukosa ajira, pili kwenye uandishi kuna kitu kinaitwa sanaa ya uwasilishaji. Bandiko lako limekosa hii kitu.

Kwa Arusha maeneo ya Sakina kwa Idd kuna NGO inahusika na utafiti wa jamii na maendeleo CORDS kama huwa unasikiliza taarifa ya habari za dunia kila siku ..BBC, DW... Nahakika utakuwa na uelewa mpana wa kuwashawishi ukapata chochote. Watu wanataka watu wenye vitu vya tofauti. Kila mara jitahidi kuwa tofauti/ Go beyond your comfort zone....Exceeds someone expectations, hata cheti hutaulizwa muhimu uwezo wako Tu.

Ungeweza kuanza kwa kujieleza kwa ufupi wewe ni nani, uwezo wako katika fani uliosomea. Unaweza kumsaidiaje mtu atakayekuwa na uhitaji wa kukuajiri. Kumshawishi mtu aone umuhimu wako katika kazi zake au biashara zake.

Unaweza kuwasilisha kitu kibaya kwa namna nzuri pia unaweza kuwa na hoja nzuri ukashindwa kuiwasilisha kwa lugha ya kueleweka na watu wengi wakahisi unapiga tu kelele.

Kumaliza shahada ya kwanza sio jambo dogo kabisa. Tatizo wahitimu wengi sikuhizi hawawezi kuonyosha umahiri wa elimu yao katika jamii na hata katika maeneo ya kazi.

Mtu mwenye digrii ni mtu mkubwa sana kiuelewa wa dunia na mambo yake. Kuanzia ukweli na propaganda za mataifa ya magharibi na mustakabali wa mtaifa ya Afrika.

Tatizo sio kusema ukweli au kusema uongo, muhimu ni kupima matokeo baada ya wewe kusema na hii ndio kanuni kubwa ya dunia ya sasa. Kuna umuhimu wa shule kufundisha namna ya kufikiria/ Reasoning vs cognitive thinking.

Watu wengi pamoja na watanzania hawawezi kutumia akili yao sababu ya kukosa mahitaji muhimu ambayo ni chakula, malazi, mavazi na usalama wa mwili. Wachache wenye navyo na hawawezi kufikiri vizuri kwa kuwa mazingira hayawawezeshi.

Wahitimu tambueni ajira sio msaada ama hisani ili mtu akuajiri au akupe kibarua lazima aone kuna kitu utamsaidia. Hakuna mtu atakupa ajira kwa sababu uweze kujikimu hilo halipo katika dunia ya leo.

Unapoenda kuomba ajira popote jitambue nini mchango wako katika ofisi husika je wewe una nini cha ziada ili uajiriwe mwenzako abaki. Mfano unaweza kuwa 1. Unajiamini sana [emoji3581] 2. Unajua kujieleza [emoji3581] 3. Mbunifu [emoji3581] 4. Una haiba ya kuvutia/Nuru [emoji3581] 5. Mchangamfu [emoji3581] 6. Unamaono [emoji3581] 7. Huogopi kujaribu [emoji3581] 9. Mvumilivu [emoji3581]

Mwisho: Bahati katika maisha zipo, maisha ni foleni zamu yako itafika. Ukihisi umechelewa kufikia kumbuka kuna uliozaliwa nao leo hii walishatangulia mbele za haki na wewe bado upo tu. Hivyo shukuru kwa kila hatua na zidi kusonga mbele. [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Back
Top Bottom