Mwenye akili haambiwi tazama

REALITY

JF-Expert Member
Jul 2, 2014
4,297
1,828
Wakuu ifike mahali tuwe serious,maana nachoona ndani ya taifa ni mkanganyiko,malalamiko,ubabe,uzembe,itikadi za kisiasa,malumbano,siri za hapa na pale,kusifiana,kubezana,kutusi,kupeana moyo,hofu,taharuki,ukweli,uwongo ,ujinga na uerevu bila kusahau makosa na maombi.


Ushauri wangu

1.Waliothibitisha uwepo wa ugonjwa wasikilize kwa umakini,mf.madaktari na manesi wa wuhan na hubei huko uchina ,chukua mbinu zao na utakuwa salama maana wao washamkanyaga mdudu na shughuli zinaendelea.

2.Kama huna kazi za kufanya tulia kwako,soma vitabu au sikiliza hata updates kwa binafsi yako na faida yako na familia yako.

3.Achana na malumbano ya siasa kwenye ugonjwa ,kama ni siasa tulia huko kwenye siasa na uchukue tahadhari kwa wataalamu waliogundua kirusi kiukamilifu na kama ni issue ya ugonjwa tuzidi kukumbushana tu ni jinsi gani tunaliepuka hili jangu kitaaluma na kiutashi na sio kusikia uganda madereva 6 watz wana covid.

4.Tumia akili zako vizuri ,kama huwezi ni bora ukae kimya sio kudhihirisha ulimwengu ujinga wa wengi wetu.

5.Watu waungane kwenye jitihada ,waweke pembeni itikadi na kuwa na mlengo mmoja wa kusimamia na kuokoa uhai wa kila mmoja wetu katika jamii maana sote ni watanzania.

6.Akili za kuambiwa changanya na zako ,sio muda wa kukurupuka sasa ni muda wa kutulia,kuondoa mihemko na kusaidiana,wazungu sio wehu kirusi si chetu tulizeni akili.

MWISHO.
TAFAKARI SANA KABLA HUJACHUKUA MAAMUZI MAANA KINACHOKUJA MBELE NI MPINGA KRISTU SIO KRISTU.

#Stayhome
#besafe
#barakoa za virusi sio vumbi.

MAWAZO HURU .
 
Tuchape kazi huku tukichukua tahadhari zinazotolewa na viongozi wetu wa Afya kuhusu kupambana na corona
 
Kama madereva 6 wa malori wanakutwa Uganda wakiwa positive manake ni kwamba wapo wagonjwa angalau 10,000 nchi nzima.
 
Back
Top Bottom