Mwenge wa Uhuru unahifadhiwa wapi baada ya kutembezwa?

Mwenge wa Uhuru unahifadhiwa wapi baada ya kutembezwa?

agudev

Member
Joined
Apr 5, 2016
Posts
83
Reaction score
131
Habari za muda huu wanajamvi,

Naomba msaada kwa anayejua wapi mwenge wa uhuru unapohifadhiwa baada ya mbio za mwenge. Mwanangu wa shule ya msingi alinipiga hili swali jana nikawa napepesa macho tu, shuleni kwao wapo katika topic inayohusiana na mambo ya uhuru wa Tanzania pamoja na mwenge wa uhuru, alijaribu kumuuliza mwalimu wake kuhusu hili naye hakuwa na jibu.

Kwa yeyote mwenye ufahamu kuhusu hili naomba majibu na nitashukuru zaidi kama utaambatisha chanzo rasmi cha taarifa hii.

Asanteni
 
HUwa unaifadhiwa ikulu mana mwenge n sawa na rais wa nchi
Mmhh, mkuu una uhakika na hiki? katika pita pita zangu nimekuta sehemu zinasema upo chini ya Wizara ya Vijana, Utamaduni na Michezo na wanauweka Dodoma, sehemu nyingine wanasema huwa unaoneshwa makumbusho ya taifa lakini hauhifadhiwi humo ila sijakuta sehemu ikisema kuhusu Ikulu. Chanzo gani umetoa hii?
 
Baada ya mwenge kuzimwa hulindwa na kuongozwa na kikosi maalumu cha jeshi la wananchi (jwtz) ukisindikizwa kwenda mlima kilimanjaro..
Safari hii huanza mara moja baada ya kuzimwa na mheshimiwa RAIS wa jamhuri ya muungano wa tanzania..

"nilipokosea, nikosolewe"
 
Hufichwa kusikojulikana maana unachukiwa sana
 
Akili za WaTz zmefungwa mule kwahiyo ni siri huwez jua unafichwa wapi
 
Baada ya mwenge kuzimwa hulindwa na kuongozwa na kikosi maalumu cha jeshi la wananchi (jwtz) ukisindikizwa kwenda mlima kilimanjaro..
Safari hii huanza mara moja baada ya kuzimwa na mheshimiwa RAIS wa jamhuri ya muungano wa tanzania..

"nilipokosea, nikosolewe"
Hili tukio lilifanyika Mwaka jana ila sizani kama huwa ni kila mwaka japi nipo tayari kukusolewa
 
Habari za muda huu wanajamvi, naomba msaada kwa anayejua wapi mwenge wa uhuru unapohifadhiwa baada ya mbio za mwenge. Mwanangu wa shule ya msingi alinipiga hili swali jana nikawa napepesa macho tu, shuleni kwao wapo katika topic inayohusiana na mambo ya uhuru wa Tanzania pamoja na mwenge wa uhuru, alijaribu kumuuliza mwalimu wake kuhusu hili naye hakuwa na jibu.

Kwa yeyote mwenye ufahamu kuhusu hili naomba majibu na nitashukuru zaidi kama utaambatisha chanzo rasmi cha taarifa hii. Asanteni
Fort knox
 
HUwa unaifadhiwa ikulu mana mwenge n sawa na rais wa nchi
Mkuu Kuna vitu vitatu vyenye umuhinu kwa nchi kiongozi yeyote wa kitafaifa anapaswa kujua
1. Viongozi wa juu wa serikali Rais, Makamu, Waziri mkuu, Makamu Waziri mkuu

2. Mwenge wa Uhuru

3. Mtihani wa Taifa/ Necta.
Hivyo ni muhimu lakini sio kwamba vinahifadhiwa Ikulu. Hapana
 
Screenshot_2025-08-19-11-09-26-25_965bbf4d18d205f782c6b8409c5773a4.jpg
 
Back
Top Bottom