Mwenge wa Uhuru 2025 kuzinduliwa Mkoani Pwani

Mwenge wa Uhuru 2025 kuzinduliwa Mkoani Pwani

upupu255

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
341
Reaction score
476
Mkoa wa Pwani umeteuliwa kuwa mwenyeji wa shughuli ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 zitakazozinduliwa Aprili 2, mwaka huu katika Uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha Pwani sherehe zitakazohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, mikoa jirani na wilaya zote za Mkoa wa Pwani pamoja na wananchi.

Kauli mbiu ya Mwenge mwaka huu ni "Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa Amani na Utulivu" ikihimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi kwa utulivu, mshikamano na uzalendo ili kudumisha amani na maendeleo ya taifa kwa ujumla na wakimbiza Mwenge watatoa ujumbe unaombatana na kauli mbiu hiyo.

"Hii ni fursa kubwa kwetu sote wana-Pwani, uzinduzi huu ni chachu ya maendeleo ya mkoa wetu na hasa katika suala la kiuchumi kama vile huduma za malazi, chakula, usafiri, vinywaji, utalii na mengineyo mengi. Nawaomba wananchi wote wa Mkoa wa Pwani na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uzinduzi huo," amesema Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Alhaji Abubakar Kunenge.

Kunenge amesema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika halmashauri zote tisa za mkoa ambapo utakagua, kutembelea na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

 
HII KITUNINALITAFUNA TAIFA.

Mwenge Hapana
Huu uchawi Unatosha.

2025 kweli Tunakimbiza Mwenge!!!!

"Hakuna umasikini Mbaya Kama Umasikini wa Fikra"
JK Nyerere.
 
Yani kumbe kamwenge kenyewe kadogo...
Matumizi mabaya sana ya akili na fedha.
Nikiwa Raisi 2025, naweka huyo National Museum
 
Kupoteza pesa tu
Tena pesa mingi sana zinapotea kwenye huu mwenge bila maana yoyote na kuna mashule huko mpaka leo hii hayana madawati, hospitals hazina madawa na vifaa vya tiba vibovu, barabara zimekatika na mvua hizi na hawana muda kuzi rekebisha.

Hivi CAG huwa hatoi report ya fedha zinazotumika na kupotea kuhusu huu mwenge?!
 
Back
Top Bottom