Mwenendo wa kufoji nyaraka za serikali haukubaliki

leonaldo

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
2,585
3,179
Nimesikitishwa sana na kinachoendelea sasa hapa nchini na huku watu tukigawanyika na kuyachukulia kana kwamba ni masuala ya kisiasa, bado sijasahau kipindi kile watu walipokuja na zuio la mahakama feki kuzuia uchaguzi wa meya wa jiji la Dar, najua mlipotezea wala sijui ni hatua gani zilichukuliwa kwa aliye lidanganya taifa hili na kusababisha mtafaruku usio kuwa wa lazima.

Watu walipigwa,wangine waliwekwa ndani wengine wana kesi hadi leo, lakini kuna mtu alienda mbali na kuangalia chanzo cha tatizo hilo ni nini? nakumbuka sinema iliisha pale tu mkuu wa kaya aliposema anachotaka ni meya bila kujali ametoka chama gani.

Jingine ni hili la juzi tume ya maadili wamekanusha kuhusika na barua zilizotumwa kwa wabunge Tundu Lisu na Philmon Mbowe, zikiwataka wajieleze kuhusiana na masuala mbalimbali ya kimaadili staki kuingia ndani zaidi kuhusiana na suala hili, Ila kilichonikela rohoni ni jinsi gani taifa letu limeanza kubobea katika kutotimiza wajibu, nakubali watu wanawajibika kwenye mambo madogo madogo na kuacha mambo makubwa kwa sababu tu yanawahusu wale,

Hivi kuna hatua zozote zimechukuliwa kujua ni nani anafoji nyaraka muhimu hizo za serikali? na kwa nini afanye hivyo? je analitakia mema taifa hili? je ni adui wa nje au ndani? je nia yake ni nini.?

Najua ushabiki wa kisiasa umeteka fikra za watu wengi matokeo yake ni kwamba tayali tumeruhusu ukomo wa fikra hatufikilii tena nje ya boksi tumetekwa kifikra tuko utumwani na hatujitambui ni heri kama tungetambua kuwa sisi ni mateka tungetafuta uhuru wetu. ole kwa taifa langu kwa kuwa umeruhusu hili mimi nasema vyombo vya usalama visikae kimya bila kupata majibu ya maswali hayo, kwani kwa sasa wapo wanaodai CHADEMA

Wametengeneza nyaraka hizo ili wapate kiki, wapo wanaofikili kuwa nyaraka hizo kweli zimetoka tume ila walipogundua kuwa zina mapungufu wakazikana, lakini pia tupo tunao fikili kuwa nyaraka hizi hazitokani na yeyote katika hao bali zinatokana na watu wanaotaka kulichafua taifa letu, wachochezi pengine yaweza kuwa hata maadaui wa taifa hili. ndio maana nasema iko haja ya vyombo vya usalama kumtafuta aliye gushi nyaraka hizi na hata ile ya zuio ili awajibishwe kwa makosa ya kugushi nyaraka za serikali pia anastahili kuwajibika kwa uchochezi.
 
Unakumbuka haya matatu in summary?
  • Sahihi na hati ya Muungano
  • Hati ya Mahakama ya kuzuia Uchaguzi wa Meya
  • Barua ya Tume kwenda kwa Lisu na Mbowe
Halafu zote hizi zinaigusa Mahakama aiseeee duh, ooghh please
 
Nimesikitishwa sana na kinachoendelea sasa hapa nchini na huku watu tukigawanyika na kuyachukulia kana kwamba ni masuala ya kisiasa, bado sijasahau kipindi kile watu walipokuja na zuio la mahakama feki kuzuia uchaguzi wa meya wa jiji la Dar, najua mlipotezea wala sijui ni hatua gani zilichukuliwa kwa aliye lidanganya taifa hili na kusababisha mtafaruku usio kuwa wa lazima, watu walipigwa,wangine waliwekwa ndani wengine wana kesi hadi leo, lakini kuna mtu alienda mbali na kuangalia chanzo cha tatizo hilo ni nini? nakumbuka sinema iliisha pale tu mkuu wa kaya aliposema anachotaka ni meya bila kujali ametoka chama gani.
Jingine ni hili la juzi tume ya maadili wamekanusha kuhusika na barua zilizotumwa kwa wabunge Tundu Lisu na Philmon Mbowe, zikiwataka wajieleze kuhusiana na masuala mbalimbali ya kimaadili staki kuingia ndani zaidi kuhusiana na suala hili, Ila kilichonikela rohoni ni jinsi gani taifa letu limeanza kubobea katika kutotimiza wajibu, nakubali watu wanawajibika kwenye mambo madogo madogo na kuacha mambo makubwa kwa sababu tu yanawahusu wale, hivi kuna hatua zozote zimechukuliwa kujua ni nani anafoji nyaraka muhimu hizo za serikali? na kwa nini afanye hivyo? je analitakia mema taifa hili? je ni adui wa nje au ndani? je nia yake ni nini.?
najua ushabiki wa kisiasa umeteka fikra za watu wengi matokeo yake ni kwamba tayali tumeruhusu ukomo wa fikra hatufikilii tena nje ya boksi tumetekwa kifikra tuko utumwani na hatujitambui ni heri kama tungetambua kuwa sisi ni mateka tungetafuta uhuru wetu. ole kwa taifa langu kwa kuwa umeruhusu hili mimi nasema vyombo vya usalama visikae kimya bila kupata majibu ya maswali hayo, kwani kwa sasa wapo wanaodai CHADEMA wametengeneza nyaraka hizo ili wapate kiki, wapo wanaofikili kuwa nyaraka hizo kweli zimetoka tume ila walipogundua kuwa zina mapungufu wakazikana, lakini pia tupo tunao fikili kuwa nyaraka hizi hazitokani na yeyote katika hao bali zinatokana na watu wanaotaka kulichafua taifa letu, wachochezi pengine yaweza kuwa hata maadaui wa taifa hili. ndio maana nasema iko haja ya vyombo vya usalama kumtafuta aliye gushi nyaraka hizi na hata ile ya zuio ili awajibishwe kwa makosa ya kugushi nyaraka za serikali pia anastahili kuwajibika kwa uchochezi.
Ni lini na ni wapi uliwasikia tume ya mahakama kukanusha barua aliyotumiwa Tundu Lissu?
 
Ni lini na ni wapi uliwasikia tume ya mahakama kukanusha barua aliyotumiwa Tundu Lissu?

waliotakiwa kukanusha ama kuikubali sio tume ya mahakama kama unavyosema wala hiyo barua haikutoka huko, bali aliyekanusha kupitia vyombo vya habali ni mwenyekiti wa tume ya maadili ya viongozi ambayo ndiyo iliyokuwa inadaiwa kuandika barua hiyo, hapo upo?
 
Back
Top Bottom