Mwanzo nilijua ni allergy kumbe ni aina ya sumu nilitengeneza mwilini bila kujua

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Niliwahi kuwa nawashwa sana masikio kwa ndani, nilijaribu sana kwenda hospitali nikatumia dawa zikawa zinatuliza ila sikujua kuwa kuna kitu ninachokula karibia kila siku ndio kinacho tengeneza sumu kwenye damu kiasi kwamba nikila Karanga, Tangawizi, Parachichi… nasikia masikio yana washa sana sana, nilikuwa na muda mgumu sana hadi nilifikia hatua ya kutaka kujua tatizo la allergy hutokana na nn haswa nilijifunza kwamba kunaweza kuwepo na mapungufu ya vitamin flan ambazo huwa zinasaidia kutengeneza kinga flan mwilini, sasa hapa nilipofikia nikapata ufumbuzi baada ya kuanza kujaribisha kuacha chakula kimoja kwenda kingine... ITAENDELEA

TUNAENDELEA: Kingine nilicho jifunza ni kwamba ndani ya damu huwa kuna cells ambazo huwa zina poza aina flan flan ya sumu inayoingia mwilini na kutoruhusu kuathiri mwili na viungo, nilijifunza kwamba kuna vitamins nyingi tunazipata kwa kula vyakula mbali mbali na matunda na ndivyo kuwa zinachangia kutengeneza kinga mwilini, sasa nilihoji sana mwili wangu je, ni aina ipi ya vitamin ambayo sina mwilini na inapelekea mm kula baadhi ya vitu na kujisikia nimewashwa masikioni. Hatua niliyoichukua ilikuwa ni ngumu sana, kwanza niliangaza chakula ninachokipenda na kula mara kwa mara ikiwamo na viungo ili nisikilizie itakuwaje na je masikio yataacha kuwasha, wakati naacha kla na kunywa vitu pendwa nilianza kmeza vidonge vinaitwa PREDISOLONE vile vya orange, kusema ukweli niliacha kula karanga, tangawizi, parachichi kwa ajili ya yale mafuta yake, nikaacha kunywa chai yenye sukari kabisa na soda kabisa hii ilinichukua kama wiki mbili kabisa sili vitu hivyo, nikaenda mbali sana baada ya wiki 2 ili kuendelea kusikilizia maana mm huchuja maji ya chumvi ya mawe na hivyo kuitumia kwenye chakula, niliacha kabisa kula chakula chenye chumvi pia ila vidonge nilimeza viwili asubuhi na viwili jioni kwa siku 3 tu nikaacha mana najua nimeshaacha chakula pendwa sasa nikawa nasikilizia masikio itakuwa....ITAENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom