Mwanzilishi wa Tukuyu Stars azikwa kwa Kuchomwa Moto

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,446
patel-1.jpg

MAMIA ya waombolezaji wamejitokeza kuuaga mwili wa marehemu Ramnik Patel ‘Kaka’, ambaye alifariki Oktoba 18 mwaka huu, nyumbani kwao Uhindini mkoani Mbeya ambapo kulingana na taratibu na mila za Kihindu, mwili wa mwanzilishi huyo wa timu ya soka ya Tukuyu Stars ulizikwa kwenye makaburi ya Sabasaba jijini Mbeya kwa kuchomwa moto.

patel-2-1024x768.jpg

Patel alifariki dunia baada ya kusumbuliwa na maradhi ya mguu kwa muda mrefu kutokana na kuvunjika mfupa wa nyonga kwenye mguu wake wa kushoto na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Jiji la Mbeya tangu Agosti mwaka huu kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Hata hivyo, aliruhusiwa baada ya afya yake kuimarika na kuendelea kuugua akiwa nyumbani.

patel-3.jpg

Patel maarufu kwa jina la Kaka au Banyambala ambaye ndiye mwanzilishi wa timu hiyo, atakumbukwa kwa kuipandisha daraja na kuiewezesha Tukuyu Stars kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 1986, pamoja na kuwaibua wachezaji kadhaa nyota waliotamba nchini.

Hata hivyo, msimu wa 1987 iliteremka daraja na Kaka akahangaika nayo hadi kuipandisha tena msimu wa 1988 alipoirejesha Ligi Kuu na kuikabidhi kwa Halmshauri ya Wilaya ya Tukuyu, ambako huko ndipo ilidhoofika.

patel-4-1024x768.jpg

Tukuyu inakumbukwa kwa kuibua vipaji vya nyota wengi wa soka mara zote, kuanzia akina Salum Kabunda ‘Ninja’, Justin Mtekere (wote marehemu), Godwin Aswile ‘Scania’ na baadaye akina Stephen Mussa (sasa marehemu) na Sekilojo Chambua.
Aliyewahi kuwa kocha wa timu hiyo, mwaka 2001 hadi 2004, Chuma Amos, alisema watamkumbuka marehemu hasa katika mchango wake wa kuhamasisha mchezo katika Mkoa wa Mbeya.

“Tukuyu Stars ndiyo ilikuwa timu ya kwanza Mkoa wa Mbeya kushiriki ligi kuu na kutwaa ubingwa, na baadaye kukapelekea kuibuka kwa timu nyingine kama Mecco, 44 KJ, pamoja na Tiger ambayo ilikuwa ya Tunduma,” alisema Amos.
Marehemu ameacha wajane wawili na watoto watatu. Mwenyezi Mungu ailaze mahali pema peponi,
AMEN!
 
Kuna story nyingi kuhusu huyu Jamaa akiwa na duka pale Tukuyu mjini ilikuwa ni shida

Aliacha mke wake wa kihindi na kumuoa mbongo anaitwa Neva

Dukani kwake kuna Siku mke wake wa kihindi alikuwa akajibu tu Sina change, Duka lake lilikuwa linauza vitu kwa hasara Sana yaani alikuwa anauza bei za chini Sana kulinganisha na maduka mengine

Mitaa ya Bagamoyo pale Tukuyu ndipo duka lake lilikuwepo, Kashfa kubwa mpaka aliamua kuondoka Tukuyu ni ishu za Tuhuma za kuficha watoto wadogo wakiingia Dukani kwake kuwapoteza
 
Nyuma ya pazia, Pale mitaa ya Bagamoyo lilipokuwepo duka lake kuna mengi Sana ya kusimulia

Inaaminika alitumia majini kwenye biashara zake, Alianza kufirisika baada ya kumuacha mke wake wa kihindi na kumuoa mbongo Neva akiitwa Hivyo
 
Duh ...ila wahindi kwa mambo ya MILA ndio maisha yao!
Nyuma ya pazia, Pale mitaa ya Bagamoyo lilipokuwepo duka lake kuna mengi Sana ya kusimulia

Inaaminika alitumia majini kwenye biashara zake, Alianza kufirisika baada ya kumuacha mke wake wa kihindi na kumuoa mbongo Neva akiitwa Hivyo
 
Nyuma ya pazia, Pale mitaa ya Bagamoyo lilipokuwepo duka lake kuna mengi Sana ya kusimulia

Inaaminika alitumia majini kwenye biashara zake, Alianza kufirisika baada ya kumuacha mke wake wa kihindi na kumuoa mbongo Neva akiitwa Hivyo
Neva ndio huyo hapo karibu na maua?
 
Nyuma ya pazia, Pale mitaa ya Bagamoyo lilipokuwepo duka lake kuna mengi Sana ya kusimulia

Inaaminika alitumia majini kwenye biashara zake, Alianza kufirisika baada ya kumuacha mke wake wa kihindi na kumuoa mbongo Neva akiitwa Hivyo
Neva kwasasa nasikia ni dereva Mbeya Cement, dada hafai yule alimtelekeza Kaka kipindi ugonjwa umeshika mwili kisawasawa
 
Back
Top Bottom