Mwanza: Wananchi Wakesha kwenye ofisi za CHADEMA ili kuwahi Maandamano

Msisumbuke na wanasiasa. Tanzania itajengwa na watanzania wote wenye hisia na uzalendo na sio CCM au Chadema au wengine.
 
Ndo maana nimeona hekaheka za malori ya Alliance yakibeba watu badala ya pamba
 
Hii ndio Taarifa Mpya iliyotufikia usiku huu, kwamba Maelfu ya Wananchi wanamiminika kwenye ofisi zote chadema za Jiji hilo kwa lengo la kukesha ili kuwahi kujiandikisha, ili washiriki maandamano.

Wananchi wengi wanadhan kwamba i ili kushiriki Maandamano hayo ni lazima ujiandikishe, hivyo wamewahi kwenye ofisi hizo ili kujihakikishia namba za usajili.

Ukweli ni kwamba Maandamano ya Chadema hayana usajili , kila mtu aliyeguswa na ugumu wa maisha anashiriki tu.

Natoa wito kwa viongozi wa chadema Mwanza na kanda ya Victoria kuelimisha wananchi kuhusu jambo hilo.

View attachment 2904329
Ukweli ni kwamba Maandamano ya Chadema hayana usajili , kila mtu aliyeguswa na ugumu wa maisha anashiriki tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa ndipo mnapokosa hekima....mkiambiwa mnabaki kulialia....surely kama taifa tuko Kwenye maombolezo tena ya mgombea urais kupitia Chadema 2015....Kwamba nyie hamkuona busara kusogeza mbele maandamano yenu hayo?

Chama kinapoteza mvuto Kwa sababu ya kuongozwa na kakikundi Ka watu wajinga....wasio na impact katika jamii,chama cha matukio.
Msidhani upinzani ni show off ya vipeperushi na ma'tshirts,upinzani ni roho....mbona mpina anakiwasha bungeni na ni CCM vipi kuhusu wabunge wenu waptao 20?
 
CHADEMA ni wapuuzi sana!
Taifa liko katika majonzi na maombolezo ya Kitaifa ambayo yametangazwa na Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dr.Samia Suluhu Hassan halafu wao wanakaidi na kuendelea kuandamana!

Musoma Mjini CHADEMA - Maandamano mmewambia viongozi wenu wapeleke waandamanaji 300 na wajigharamikie wenyewe vinginevyo viongozi wenu hao wawajibike!

CHADEMA - Maandamano inasema wao hawana hela.
Viongozi wenu ni kilio, wanasema nauli ya Tzs.24,000 (kwenda na kurudi Musoma - Mwanza) hapo bado Chakula wamesema wao hawana!

Ni propaganda tu hakuna Mwananchi mwenye akili timamu anaweza kukesha hapo CHADEMA kuwahi Maandamano! Labda hao ni vibaka wasiokuwa na mahali pa kulala!

Dr.Slaa naye mzuka umempanda baada ya Edward Lowassa kifariki anataka kuandamana/kusherehekea kifo cha Lowassa nanyi.

Maandamano yenu lazima yadode!
Usilie
 
Hii ndio Taarifa Mpya iliyotufikia usiku huu, kwamba Maelfu ya Wananchi wanamiminika kwenye ofisi zote chadema za Jiji hilo kwa lengo la kukesha ili kuwahi kujiandikisha, ili washiriki maandamano.

Wananchi wengi wanadhan kwamba i ili kushiriki Maandamano hayo ni lazima ujiandikishe, hivyo wamewahi kwenye ofisi hizo ili kujihakikishia namba za usajili.

Ukweli ni kwamba Maandamano ya Chadema hayana usajili , kila mtu aliyeguswa na ugumu wa maisha anashiriki tu.

Natoa wito kwa viongozi wa chadema Mwanza na kanda ya Victoria kuelimisha wananchi kuhusu jambo hilo.

View attachment 2904329
Huu uongo unakusaidia nini? Tangu saa 05:00hrs mvua inapiga. Route zote mahudhurio ni hafifu, na bado kuna dalili za mvua kunyesha muda wowote. Hivi ujaze watu usiweke picha?
 
Back
Top Bottom