The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,535
Kama wasukuma wangekuwa wana ukabila usingeona makabila mengine yakishamili kibiashara katika maeneo ya wasukuma.
Leo hii ukienda kwenye mikoa yenye wasukuma wengi utakuta wafanyabiashara wa kichaga wamejaa na biashara zao zinapata mafanikio makubwa kwa sababu wanunuzi ni wasukuma.
Wakina dada wengi wa makabila mengine wameolewa na wasukuma.
Kwa ujumla, wewe unaodhani wasukuma wana ukabila inawezekana ukawa ni mkabila namba moja.
Huwezi kujua kama fulanio ni chawi kama huna elimu ya kichawi!
Acheni kuwalazimisha wasukuma wawe wakabila na siku wakiwa wakabila itakuwa ni jadi kwa serikali kuongozwa na watu kutoka katika kabila la wasukuma. Kwenye siasa, namba zinahesabika!
Haitatokea wasukuma mpendane na eti mchaguane ninyi kwa ninyi..!
By the way, suppose na haya mengine (makabila) zaidi ya 120 yaungane kuwapinga wasukuma mtasimama wapi? Mtaweza?
All in all, kama kiongozi mkuu wa nchi, ndugu yenu juzi kama kawaida yake alichemka kwa kauli yake whether mnapenda ama hampendi...
Na matokeo yake ni haya sasa. Kila mtu anaitafsiri kwa namna yake...
Mbaya zaidi wale wa maeneo mengine ya nchi hiihii wanajisikiaje taratibu na sheria hizo hizo zinatumika kuwabomolea makazi yao huku wale wa nyumbani kwa Rais anatangaza msamaha wa waziwazi tena mchana kweupe?
Haya ndiyo matatizo ya kupewa nafasi ya uongozi ktk ngazi ya juu kwa kushtukizwa kwa mtu kama huyu...!!