Mwanza: Mwenyekiti wa CCM, Diwani, Afisa Mtendaji washikiliwa kwa tuhuma za mauaji kisa wizi wa mihogo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
David Shilime (Diwani), William Nengo (Mwenyekiti wa CCM Kijiji cha Ikoni B) na Tiluloza Alfonce (Afisa Mtendaji) wote wa Kata ya Buzilasoga Wilayani Sengerema ni kati ya watuhumiwa 14 wanaoshikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya Getruda Dotto mkazi wa kijiji hicho wakimtuhumu kwa wizi wa mihogo.

Walimtuhumu Getruda kuvamia shamba la Scolastica John ambalo lilikuwa likimiliwa na mume wa marehemu lakini liliuzwa na wanaukoo bila kumshirikisha Getruda siku ya msiba wa mumewe, Ndebete Miharalo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema wanadaiwa kumshambulia kwa fimbo na rungu kisha kumchoma moto kwa vipande vya miti.

1.jpg



2.jpg

3.jpg

4.jpg
 
Ushirikinaaa upoo c kwa ndugu zetu tu albino wanachukuliwaa viungo kunaa watu wakawaidaa pia daily wanauwaa na viungo vinachukuliwaaa..
 
Tusha fika tar 05/12/2022 jeshi la polisi liko mbele sana ya mda hadi matukio ya mwezi wa 12 /2022 tusha yafikia
 
Kumekucha kumekucha! daaah mie ningekuwa Rais wale wote wanaoua albino wangeuliwa kwa kuburutwa na gari mtaa mzima ambako mauaji yametokea
 
Back
Top Bottom