Mwanza Kwawaka Moto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanza Kwawaka Moto

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mentee, Jan 29, 2011.

 1. Mentee

  Mentee Senior Member

  #1
  Jan 29, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 142
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mji wa Mwanza leo umezizima kwa masaa takribani matano baada ya Wamachinga kuteka mitaa yote ya katikati ya jiji. Uongozi wa Jiji la Mwanza umevunja vibanda vya Wamachinga katika operesheni maalumu na Wamachinga wamejikuta wakilazimishwa kuhamia umbali wa kilomita kama kumi hivi ili kuanza makazi yao mapya ya biashara. Hata hivyo, hali haikuwa kama ilivyotarajiwa kwani uongozi wa Halmashauri ya Jiji hili umejikuta ukipata changamoto kama lile la Tunisia na Misri... ingawa hapa hakuna waliojitoa muhanga na kujichoma moto lakini wamegomea amri ya kuhamia makazi mapya. Leo tangu asubuhi Wamachinga wamekuwa wakipora maduka yaliyo wazi hasa ya Wahindi na kuvunja vioo vya magari yanayopita hususan katika barabara kuu kama ya Kenyatta. Je, Watanzania wamechoka na maisha ya dhiki ya kila siku? Je, viongozi wa ngazi za juu hawasomi alama za nyakati?
   
 2. M

  MMASSY JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 225
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Ukishakuwa na serikali inayowatete wageni na kuwadharau Wananchi walioipigia kura unadhani nini kinafuata?Nguvu ya umma lazima ishinde tu.Kipindi cha kampeni wanaruhusu wamachinga hadi bustani za mkuu wa mkoa,kwanini baada ya kushindwa wawanyanyase Wamachinga ambao wanajenga taifa kuliko hata walio Ikulu?TAFAKARI!!
   
 3. R

  Radi Member

  #3
  Jan 29, 2011
  Joined: May 22, 2010
  Messages: 94
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Mkuu Mantee huko ndiko tunako kwenda sasa hivi,acha moto uwake mpaka kieleweke,si mimi tu ila watu wamechoka, ukondoo sasa basi.
   
 4. m

  mzambia JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Bado wa iringa, mbeya, tanga, songea
   
 5. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Amani ya Umaskini, haina maana! Wacha mambo yaanze.... CCM TUMEICHOKA!
   
 6. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Na bado,nazan ukombozi kamili utakuja kwa sisi wana jf tukiacha kuongelea humu ndani na kupeleka mawazo yetu barabarani na kuwa mobilize hao wamachinga mana humu ndani maneno mengi ila vitendo hakuna kitu
   
 7. m

  mzambia JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mbona machinga wa dar wako kimya? Si wangewaunga wenzao mkono
   
 8. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kama dhiki ndicho kingelikuwa chanzo cha fukuto linaloshuhudiwa hivi sasa, basi fukuto hilo lingelianzia katika miaka ya themanini; maana dhiki tuliyokuwa nayo wakati huo inazidi ya sasa. Lakini kwa wakati huo, hali ngumu ya uchumi ilikuwa inatukabili wote jopo kwa viwango tofauti, kinyume na sasa ambapo wachache wanaogelea kwenye utajiri husio elezeka, wakati wengi wamezama kwenye dimbwi la umasikini wa kutupwa. Hali kama hiyo haikubaliki hata kidogo. Hivyo wale wote wanao hubiri amani, huku wanaendekeza hali hiyo ni maadui wa amani hiyo wanayo hubiri tu majukwani.
   
 9. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  Kazi nzuri. Tunaelekea Tunisia na Misri
   
 10. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  :sick:Mwanzo kaka bado tunahitaji nguvu mambo taratibu mpaka tunafikia na kuwa na nguvu kama ya Tunisia na Misri basi Mkwere Kikwete lazima akimbie na akiondoka asimsahau Ridh1 pamoja na mama zao. Tumechoshwa kuonewa kila kila ma hawa mafisadi papa. CCm imeweka wageni kwanza mwenye baadaye sasa madhara yake ndio haya nataka hata leo kiwake kama ya Tunisia wajue kuwa hatufugi ujinga wao tena. Magogoni imegeuzwa sehemu ya starehe na Fisadi Kikwete wakati wenye nchi wanahangaika na kuonewa, mjinga Fisadi Kikwete:sick:
   
 11. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hivi jiji la mwanza linaongozwa na Chadema?
   
 12. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hivi Kikwete na Ridhiwan na mama zao wakiondoka, hawa Vuvuzela wengine wa CCM kama Makamba, Msekwa nk nao watakimbia?

  Watu kama Anna Mkapa, Mramba, Lowassa, Chenge na kagenge kao ka Mafisadi wakubwa, wanahela nyingi tu za kwenda kuishi nje. Ila hata wakikimbia, kwangu mie wanajidanganya tu kwani wamezoea kuabudiwa. Wakifika huko waendako, watakuwa Visamaki vikubwa kwenye bwawa kubwa sana. Na kibaya zaidi huko kuna akina Papa na Nyangumi.

  Walifanya makosa sana kutokuona alama za nyakati. Rostam Azziz yeye ndiyo naona aanze kutembea akiwa na Nepi maana huyu ikianza Tunisia, basi itabidi watu waanzie kwake. Pia kuna hawa Wahindi wa Rada na Ferrari yake, itabidi wawe wanaishi karibu na viwanja vyao vya ndege na huku ndege ikiwa na mafuta ya kutosha kuruka hadi nje ya nchi.

  Saa ya ukombozi imekaribia ...............
   
 13. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #13
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wamachinga wa nchi nzma waungane wamtoe panya tunduni
   
 14. tama

  tama JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 604
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni wakati wa hii serikali ya mafisadi kujua kwamba,panakofuka moshi pana moto.
   
 15. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Mkuu hakuna kwa kukimbilia siku hizi angalia hapa chini .... .... .... .. hawa tunao tu .... na ni lazima wanyee debe .... ......  Chacha njomba hakuna kwa kukimbilia, I am just waiting for that day .... ...... very soon .... .......soon indeed.
   
 16. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #16
  Jan 29, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mnapowatimua watu watafutieni maara pa kwenda sio kuwatelekeza alafu muwe wastaarabu sio kuwatia hasara.
  Bse hao ni wateja wenu hao wakati wa uchaguzi
   
 17. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #17
  Jan 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  One step
   
 18. n

  niweze JF-Expert Member

  #18
  Jan 29, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kinachotakiwa sasa ni kuunganisha Uonezi toka kila mahali na tuungane na wote Mwanza. Swala la Wamachinga ni sehemu ndogo kati ya matatizo makubwa tulionayo Tanzania. Tusikae majumbani hasa wananchi wa Mwanza na kuwatenga Wamachinga peke yao. Huko Misri na Tunisia ni kijana mmoja tu ali Inspire nchi nzima na mpaka Raisi Ben Ali akaoondoka na kukimbia Tunisia na sasa nchi itabadilika. Ni haki yetu kutaka Jk/Pinda na CCM waondoke Tanzania. Tuache kukaa majumbani kusubiri madiliko kutoka Chadema, viongozi wa Chadema hawawezi peke yao.
   
 19. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #19
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  patam hapo, mzuka wa mapinduzi unapanda,viva la revolucion. Mkwereeee, siku zako zinahesabika, kimbia nchi haraka, rafiki yako james sinclays agent wako wa madin yetu huko marekani atakupa hifadhi wewe na akina miraji au tamil somaiya mwizi mwenzio nae anaweza kukuficha huko kashmiri india wewe na wale mabinti wanaosoma lushoto shule ya kikatoliki, kwanini huku wapeleka jabal hira au hal aramain?wamachinga tupo pamoja mpaka kieleweke.
   
 20. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #20
  Jan 29, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  TUNISIA=EGYPT=TANZANI=UGANDA=ZIMBABWE=KENYA=MALAWI=ZAMBIA


  Coming sooooooooon:msela:Coming sooon! coming sooooon!:msela:
   
Loading...