Mwanza hii tabia ya kutulisha mbwa acheni

Pa
:mad::mad: Wakazi wa Mwanza, Mungu anawaona. Hii tabia iliyotamalaki ya kulisha watu kitoweo cha mnyama mbwa sijaipenda.

Tukio la kwanza lilitokea eneo maarufu Buswelu Centre, sehemu inayoitwa MSUKUMA PUB, kuna kaka pale anapika supu maarufu Mangi japo ni Mmeru anaitwa Mbise, wiki chache zilizopita alikamatwa usiku na askari wa doria akiwa na mzigo walipomtilia shaka na kumpekua akakutwa na VICHWA 4 (vinne) vya mbwa. Baada ya kubananishwa akakiri kuwa huwa anachanganya nyama ya mbwa na mbuzi, alikaa mahabusu siku kadhaa baadae wamemwachia anaendelea na biashara yake.

Tukio/matukio mengine ni kule sehemu za viwanja vya nane nane Nyamhongolo nako viliokotwa vichwa viwili (2) vya mbwa maeneo ya karibu na uwanjani, puuuuuuuuuuuuuuu!!! kumbe baadhi ya washenzi walikuwa wanachoma nyama za mbwa.

Tuhurumiane jamani, mbwa sio utamaduni wetu.
Pale msukuma pub nimekula Sana supu ya mbuzi kumbe majanga Tena Ila sijutii supu yao in radha na Ni nzito ukipiga na CD inakaa tumboni vyema...karibu buswelu, mbogamboga
 
Back
Top Bottom