Mwanza: Aliyemuua Mpenzi wake aonesha alipomfukia

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
MAHAKAMA Kuu Tanzania, Kanda ya Mwanza iliyoketi Geita imeanza kusikiliza kesi ya mauaji inayomkabili mkazi wa Lunzewe, Petro Kinasa (30), ambaye ameshtakiwa kwa kosa la kumuua Esta John kwa kumnyonga shingo kisha kuchimba shimo na kumfukia.

Mshtakiwa alipandishwa kizimbani mbele ya Jaji wa Mahakama hiyo, Liliani Itemba.

Aliposomewa shtaka lake, alikana kuhusika na kuwekwa mahabusu katika Gereza la Geita.

Upande wa Jamhuri ulikuwa ukiongozwa na mawakili watatu wa serikali ambao ni Godfrey Odupoy, Mussa Mlawa na Verena Mathias, wote kwa pamoja walidai kuwa na mashahidi wanne na wako tayari kwa kuwasikiliza.

Mshtakiwa huyo alimueleza polisi Adriano kuwa marehemu Esta John alikuwa mpenzi wake na aliwahi kumpatia Sh. 70,000 kwa ajili ya biashara.

Alidai Juni 15, 2021 majira ya saa tatu asubuhi mshtakiwa alifika nyumbani kwa mpenzi wake na kuomba aende kumsaidia kuvuna mpunga na wakaondoka wakiwa watu watatu; mshtakiwa, Esta na mtoto ambaye alimtaja kwa jina moja la Winfrida.

Alidai walipofika porini mshtakiwa alichukua kamba ya katani na kumnyonga shingoni mpenzi wake na kufariki dunia papo hapo. Baada ya kumuua alienda kwenye majaruba ya mpunga na kuchukua jembe kisha kuchimba shimo la futi tatu na kumfukia.

Alidai pia alichukua kanga ya marehemu na kumziba mtoto mdomo na pua na kufariki dunia papo hapo kisha kumtupa kichakani.
 
Ndipo tulipofikia mbali kichwa Cha mtu laiti wahusika wangeona moyo wa mtenda wasingeinua mguu
 
Wanaume ni katili sana aisee!
Weeee...! Huyu kafanya unyama lakini wanawake ndio katiri namba moja duniani. Wengi wao wameripotiwa kupiga watoto wao,wasichana wa kazi hadi kutoa uhai. Wengine kutupa kichanga alichozaa,wengine walio wengi kutoa mimba
 
Weeee...! Huyu kafanya unyama lakini wanawake ndio katiri namba moja duniani. Wengi wao wameripotiwa kupiga watoto wao,wasichana wa kazi hadi kutoa uhai. Wengine kutupa kichanga alichozaa,wengine walio wengi kutoa mimba
Mwanaume gani aliyewahi kushtaki kuwa mwanamke wake ametupa kichanga chake au ametoa mimba yake?
 
Back
Top Bottom