Aggrey Mwanri ateuliwa Kuwa Naibu katibu Mkuu wa CCM, RC Chacha kuwa Katibu wa Oganaizesheni CCM

Aggrey Mwanri ateuliwa Kuwa Naibu katibu Mkuu wa CCM, RC Chacha kuwa Katibu wa Oganaizesheni CCM

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
39,473
Reaction score
31,966
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (NEC), imemteua aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora na mbunge wa zamani wa Siha, Mkoa wa Kilimanjaro, Aggrey Mwanri kuwa Naibu Katibu Mkuu- Bara akichukua nafasi ya John Mongella.

Aidha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), imemteua Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha kuwa Katibu wa Oganaizesheni wa chama hicho akichukua nafasi ya lssa Haji Gavu, ambaye pia ni Mwakilishi Chwaka, Zanzibar.

Uteuzi huo umefanyika leo Jumatano, Julai 29, 2026 katika kikao kilichofanyika Zanzibar chini ya uenyekiti wa Rais Samia Suluhu Hassan na kutangazwa kwa umma na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi.

 
CCM ina Hazina nyingi sana ya Watu wenye Uwezo wa kuongoza Na kushika nafasi mbalimbali ndani ya chama na serikali. Wakati wao CHADEMA kupata tu mgombea Urais inakuwa ni patashika na mtafutano Hadi kuomba Msaada kutoka CCM kama ilivyofanyika 2015
 
Taarifa zinazoendelea kusambaa hivi sasa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii zinaeleza Ndg.Aggrey Mwanri a.k.a Mtamisemi au mzee wa sukuma mdani ameteuliwa kupokea kijiti kutoka kwa Mongela.

Mimi napenda CCM

Zidumu Fikra za Mwenyekiti wetu wa CCM

CCM OYEEEEEEEE
 
CCM ina Hazina nyingi sana ya Watu wenye Uwezo wa kuongoza Na kushika nafasi mbalimbali ndani ya chama na serikali. Wakati wao CHADEMA kupata tu mgombea Urais inakuwa ni patashika na mtafutano Hadi kuomba Msaada kutoka CCM kama ilivyofanyika 2015
Ccm ina wingi mbovu na si ubora. Inaonekana unajua Tanzania ilikuwa na uchaguzi mmoja tu wa vyama vingi wa 2015. Cdm hawajawahi kujivunia wingi bali ubora. Watu wajinga hujivunia wingi ama ukubwa, wakati watu smart huangalia ubora na ufanisi.
 
Angalia kwenye ramani ,nyie watu wa mkoa angalieni asije kuwaingiza mkenge ,Engineer soma hiyo.
unatuletea habari ya Abunuasi eti kalume kenge alikataa kwenda shule..huu mkutano ni wangu sitaki kusikia mtu anaongea na simu nitamfyekelea mbali..Kuna muda tuli enjoy wakati ule...Hapo hujakutana na Kangi Lugola a.k.a Ninja mzee wa kuyakata mauno..daaa! kila zama na zama zake.
 
CCM ina Hazina nyingi sana ya Watu wenye Uwezo wa kuongoza Na kushika nafasi mbalimbali ndani ya chama na serikali. Wakati wao CHADEMA kupata tu mgombea Urais inakuwa ni patashika na mtafutano Hadi kuomba Msaada kutoka CCM kama ilivyofanyika 2015
SUKUMA NDANI
 
Baba Mchungaji ndani ya chama cha mboga mboga.
"Soma hiyooo" na "sukuma ndanii".
Ila CCM, khaaah. 😂😂😂😂
 
Ateuliwe kuwa katibu mkuu huyo mtu wa UN hawezi kupambana na waswahili
 
Back
Top Bottom