Mwanga wa ajabu wa Jua leo Dar es Salaam saa 12:10 jioni, rangi ipo Kama nyekundu au Chungwa

Mwanga wa ajabu wa Jua leo Dar es Salaam saa 12:10 jioni, rangi ipo Kama nyekundu au Chungwa

Miss Madeko

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
4,444
Reaction score
5,747
Sijui ule mwanga ulikuwa na ishara ya nini kwa anaejua maana lilikuwa jua kali lilowaka wa muda wa dakika 10 mpk 15.

Nina imani wakazi wengi wa Dar es Salaam wameuona

======

TAARIFA KWA UMMA
KUHUSU MWONEKANO WA ANGA KUWA NA RANGI NYEKUNDU AU CHUNGWA KATIKA BAADHI YA MAENEO NCHINI.

Dar es Salaam, 17 Aprili 2020:
Kumekuwa na hali ya taharuki na maswali kutoka kwa umma terehe 16 Aprili, 2020 jioni kuhusu mwonekano wa anga kuwa na rangi nyekundu au chungwa katika baadhi ya maeneo nchini. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa ufafanuzi kuhusu hali hiyo ya anga kama ifuatavyo;

Mwonekano huo wa rangi ya anga ni hali ya kawaida ambayo hutokea wakati jua linapozama au kuchomoza katika mazingira yenye kuwa na hali ya hewa kama vile mawingu, matone madogo madogo ya maji na barafu katika anga mara mvua inapokatika na jua linapokuwa katika upande tofauti na eneo mvua inaponyesha. Hali ambayo husababisha kutawanywa kwa miale ya mwanga wa jua.

Hivyo kutokana na ukubwa wa matone ya maji katika wingu na chembechembe za vumbi katika anga, sehemu ya miale ya jua inayotawanywa zaidi katika mazingira hayo ni mawimbi ya miale ya jua inayohusiana na rangi nyekundu au chungwa hivyo kufanya anga kuonekana katika rangi hizo (Mawimbi madogo sana huwakilisha rangi ya blue na makubwa rangi nyekundu au rangi ya chungwa). Hali hii haina tofauti sana na namna Upinde Mvua unavyojitokeza angani, isipokuwa upinde mvua unakuwa na rangi zote saba za spectrum ya mwanga. Mabadiliko hayo ya hali ya anga hayana madhara yeyote.


Katika hali iliyozoeleka mara nyingi, anga huonekana kuwa rangi ya bluu kutokana na kutawanywa kwa mawimbi ya miale ya jua kunakofanywa na gesi ya Nitrojeni na Oksijeni ambazo ndizo hufanya sehemu kubwa ya gesi katika hewa.

Hali hiyo inatokana na molekuli za gesi hizo kuwa ni ndogo sana hivyo hutawanya sehemu ya mawimbi madogo zaidi ya miale ya jua iliyo katika rangi ya blue katika spectrum ya mwanga. Rangi hiyo huonekana katika macho ya binadamu kwa kipindi hicho.
1587101283922.jpg

B78B7D3B-B333-40CC-9784-146D81790B5E.jpeg
D47825B4-59C8-4054-90FE-CDE8AABDDAD9.jpeg



 
Sijui ule mwanga ulikuwa na ishara ya nini kwa anaejua maana lilikuwa jua kali lilowaka wa muda wa dakika 10 mpk 15.

Nina imani wakazi wengi wa Dar es Salaam wameuona
Woww kumbe tumeona wengi
Nilikua ghorofani natizama baharini
Nikaona hiyo halii

Very differeeent
The memory is only in my mind sikuchukua hata picha
 
Ule mwanga hamkuuelewa ule mwanga ulitokea upande wa anga la mashariki jua libapochomoza, anga la mashariki lilireflect or kupokea mwanga wa jua then likang'aa na kurudisha ule mwanga duniani, kama kumulika kioo vile then mwanga unatupwa kwingine, or kama mwezi unapopokea mwanga kutoka kwenye jua then unafiak hadi duniani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom