Mwandosya: Maji ya Victoria kufika Tabora

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Mwandosya: Maji ya Victoria kufika Tabora 2014
Tuesday, 18 January 2011 21:00

mwandosya.jpg
Mwandishi Wetu, Tabora
WAZIRI wa Maji ,Profesa Mark Mwandosya, amesema serikali itatekeleza mradi mkubwa wa kupeleka maji ya Ziwa Viktoria katika makao makuu ya Mkoa wa Tabora kabla ya mwaka 2014.

Waziri Mwandosya aliyasema hayo juzi mjini Tabora kwenye majumuisho ya ziara yake ya siku sita mkoani humo, kwa ajili ya kuona hali halisi ya maji katika mkoa ambao umekuwa na shida kubwa ya maji.

Alisema hakuna njia ya kumaliza tatizo kubwa linaloukabili Mji wa Tabora kupata maji ya uhakika isipokuwa kutumia njia hiyo ambapo alibainisha kwamba hatua za awali zimekwishaanza ijapokuwa muda zaidi unahitajika.

Waziri Mwandosya, alisema kinachosumbua kwa sasa ni jinsi gani maji yafike Tabora kutoka ama Kahama au Isaka kuja Tabora na kazi inayofanyika sasa ni kuona njia ipi bora na Miji ya Nzega, Igunga, Bukene inapataje maji kutoka katika Ziwa Viktoria.

Alisema kimsingi uamuzi muhimu kuhusu suala hilo umefanyika na kinachobakia ni utekelezaji wa hatua hiyo, kwani serikali inajua ugumu wa tatizo la maji unaoukabili mji huo na kwa kipindi kirefu tumekuwa tunahangaikia hilo.

Akizungumzia udhaifu wa vyanzo vya maji katika Mkoa wa Tabora, alisema unatokana na hali ya mkoa kuwa kwenye ukanda mgumu wa upatikanaji wa maji na kwamba katika baadhi ya visima kuna maji yenye chumvi nyingi hivyo kutoweza kutumika kwa matumizi ya binadamu.

Alisema Pamoja na tatizo hilo njia pekee ya kulikabili ni kutegemea maji ya mabwawa ambayo nayo kwa siku za karibuni yamebainika kutotosheleza mahitaji ya maji katika Mji wa Tabora kutokana na mabwawa hayo ya Kazima na Igombe kuanza kukauka na kujaa matope.

“Hivyo ndugu zangu njia bora iliyopo ni kuvuta maji kutoka Ziwa Viktoria na tuendelee kutunza vyanzo vya maji tulivyonavyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa mabwawa yetu yanaishi muda mrefu zaidi”, alisisitiza.

Awali wakazi wa Manispaa ya Tabora, walimlalamikia Waziri wa Maji kwamba Mamlaka ya Majisafi na Majitaka katika Manispaa ya Tabora ( Tuwasa) inatoa huduma mbaya ya maji kiasi ambacho kinawakatisha tamaa wananchi kupata huduma nzuri.

Walisema baadhi ya maeneo yamekuwa yakipata maji saa nane usiku, mgao mdogo wa maji kwa siku nane tu kwa mwezi na mengine yakikosa maji huku mita zikisoma hewa tu na wananchi wakitakiwa kulipia ankara za mwezi ambazo ni Sh 15,000.

Huyu Profesa mwandosya sasa ni mzigo kwa taifa..........................hajajifunza matatizo ya mradi wa awali wa kuvuta maji kutoka Ziwa Victoria hadi Shinyanga......................na kama angelikuwa siyo fisadi angelibaini yafuatayo:-

a) Ule mradi ulikadiriwa kuligharimu taifa bilioni 50 lakini ukaishia kutugharimu bilioni zaidi ya 250 hii ikiwa ni zaidi ya mara tano ya makadiro ya awali ili kuwafaidisha mafisadi............................

b) Walionufaika na mradi wa awali hawafikii wanavijiji 10, 000 walengwa ikimaanisha ya kuwa cost-benefit analysis yake iliyofanyika awali ilikuwa ni ya kupika jikoni tu isiyozingatia hali halisi ya taifa hili.........................................

c) Mradi huo umeshindwa kujiendesha wenyewe ikimaanisha ya kuwa gharama za uendeshaji zinazidi mapato halisi na hivyo kusababisha kuwepo msukumo mkubwa wa serikali kufikiria kutoa ruzuku.................................

d) Pesa zilizotumiwa kwenye mradi wa kwanza yaani zaidi ya bilioni 250 zingeliweza kujenga visima 10, 000 kwa Tshs 25 miliomi kwa kila kisima na hivyo kuwaondolea zaidi ya watanzania milioni 10 kero kubwa ya maji. Pesa hizo zilitumika kuwanufaisha watanzania wasiozidi 10, 000 na ambao wameunganishwa kwenye huduma hiyo ni chini ya watanzania 6, 000. Ikimaanisha mradi huu ni zigo kubwa kwa ujenzi wa taifa hili.............Yaani hauna manufaa kabisa..................

e) Pamoja na ya kuwa kunyonya maji kutoka Ziwa Victoria ni hasara na miradi hiyo kuishia kuwa ni "WHITE ELEPHANT" viongozi wetu wamekuwa wakiisisitiza kwa udi na uvumba kwa sababu za kujijengea mazingira murua ya kulipora taifa hili masikini sana duniani..............na kujinufaisha wao wenyewe na familia zao.....................................

f) Miradi ya kufyonza maji Ziwa Victoria inahatarisha usalama wa taifa ukizingatia ya kuwa nchi za Misri na Sudan ndiyo tegemeo lao walilopewa na Mwenyezi Mungu kujipatia nishati hiyo nyeti.............................sasa tuna sababu zipi za kuwakorofisha majirani zetu hao wakat hata sisi wenyewe tunajiandikia maumivu makali kwa kujitia hasara tupu?

Ni ukweli usiopingika ya kuwa "Profesa" Mwandosya yupo hapo kwa sababu za kuulinda ufisadi na elimu yake shupavu wala hatakaa aitumie kutokana na ulafi usiojua mipaka ...........ndani ya serikali ya CCM.................................
 
Mkuu Rutashubanyuma, tunashukuru kwa analysis nzuri, ila kwa hiyo part (f) naomba nitofautiane nawe pale unaposema yale maji ya Victoria tusiyatumie kwa sababu MUNGU kaweka lile ziwa kwa ajili ya waSudan na Wamisri. Kwa kuwa hakuna andiko la MUNGU linalosema hivyo isipokuwa ni makaratasi ya kisheria yaliyokubaliwa na Wakoloni na hao Wamisri kuhusu matumizi ya hayo maji. sisi tunaozunguka ziwa hilo ni wazi nasi tunayo haki ya kuyatumia maji hayo , hilo mbona mkuu liko wazi mpaka EL aliliona pia . Kama ni usalama wa taifa kuwa hatarini naamini UWT wako proactive na wataweza kukabiliana na hilo tishio ( ukizingatia waliweza kudetect danger ya maandamano ya CDM siku moja kabla na IGP akayasimamisha kwa misingi ya kiintelijensia etc - kama ni kweli )
 
Ruta nina mashaka na analysis yako, imeifanyia utafiti wa kutosha? au una bifu na Prof Mwandosya? kahusika vipi na ufisadi wakati yeye kapokea mradi ukiwa umeshakwisha? hakuwa waziri wa maji kipindi mradi huu unajengwa, vile vile analysis yako in upotoshaji wa hali ya angalia hapa chini
part a) Mradi huu ulikuwa wa shs. 210 billion ambazo gharama zake zilipanda hadi shs. 225 Billion, sababu ya kuongeza gharama ni kuongeza maeneo ambayo hayakuwa kwenye mpango wa mradi, Jee kuongeza idadi ya wanufaika wa mradi ni ufisadi?? kwanza haya yalifanyika wakati wa Kawamba, Prof anahusika vipi? vile vile hilo ongezeko lilitumika kujenga uzio na kituo cha poliso, nyumba za operators kwa ajili ya kudhibiti vitendo vya uhalifu maeneo ya mradi, jee hii nao ni ufisadi? isingekuwa busara kama serikali isingeweka ulinzi wa kutosha kwenye mradi huu wa mabillioi ya walipa kodi, jee huu nao ni ufisadi? angalia taarifa ya Kawambwa juu ya ongezeko hilo ambayo iliwekwa wazi kwa watanzania wote kupitia vyombo vya umma
part b) mradi huu unanufaisha zaidi ya hao wanavijiji 10,000 ( si kweli wakazi wa misungwi, kahama, shinyanga na sehemu zingine za mradi wakawa 10,000 tu haiiingii akili.. MISUNGWI na kahama pekee ni zaidi ya 10,000)
c) Mradi kujiendesha wenyewe unatokana na willingness to pay by users, kama users hawawezi kuka cover costs zote ni kazi ya state duniani kote ku subsides hasa kwenye sector ya maji.. kumbuka hata UN mwaka jana wametoa tamko kuwa 'access to safe and clean water is a human right' hivyo ni jukumu la state/dola kuhakikisha haki hii haivunjwi. Maji ni uhai (bahati mbaya TZ ni kati ya dola chache ambazo hazikuunga wala kupinga azimio hili
d) pesa hizi zingetumika kuchimba visima - Hii nayo ni upotoshaji, kwani si kila sehemu ina maji ya chini ya ardhi ambayo yanakidhi viwango vya kiafya, pia kweli karne hii ya 21 bado unashauri tuendelee na technolojia ya visima na pump za mkono? kama tuna maji ya ziwa why visima? acha watu wafaidi rasilimali ambazo Mwenyezi Mungu amewawekea. Kuna chnagamoto nyingi sana katika kutumia visiwa hasa maeneo ambayo hayana umeme, maana wazo lako la visima linamaanisha kila mtu bado aende na ndoo kisimani na kuendelea kutumia zile pump za mdundiko (hand pump), I know kuna suala la solar lakini ngarama yake ni zaidi ya kuchimba kisima ili kupata solar ambayo itaendesha hiyo pump. Hivyo makadirio yako si sahihi maana umeangalia ngarama ya kuchimba kisima tu bila kungalia namna ya kutoka hayo maji toka chini mita 50 na ziadi ili yawafikie watumiaji mabao wengine wapo zaidi ya km 5 toka kilipo kisima.
e) Mradi huu sio hasara, angalia ni watanzani wangapi hadi leo wanapata haki yao ya msingi ya kupata huduma ya maji safi na salama? watoto wangapi hawatakufa kwa kuhara na magonjwa mengine yaletwayo na maji? ni mabinti wangapi sasa watapata fursa sawa ya kielimu kama watoto wengine wa kiume? kumbuka wanawake na mabinti ndo waliokuwa wakihangaika kwenda kutafuta maji mbali kabla ua mradi huu, ni ndoa ngapi zitapona sasa (yasemakana kuna wamama husingizika kwenda kwenye maji kumbe waenda ka mabwana wa nje.. a joke), shughuli za kiuchumi kwa wamama, watoto wa kike kusoma na n.k ni sehemu ya manufaa ya kuwa na maji karibu, usisahu hata rape cases zitapungua maana hakuna tena cha kufuata maji mbali na tena usiku.
f) soma comment ya NGOKO HAPO.
 
Huyu Profesa mwandosya sasa ni mzigo kwa taifa..........................hajajifunza matatizo ya mradi wa awali wa kuvuta maji kutoka Ziwa Victoria hadi Shinyanga......................na kama angelikuwa siyo fisadi angelibaini yafuatayo:-

a) Ule mradi ulikadiriwa kuligharimu taifa bilioni 50 lakini ukaishia kutugharimu bilioni zaidi ya 250 hii ikiwa ni zaidi ya mara tano ya makadiro ya awali ili kuwafaidisha mafisadi............................

b) Walionufaika na mradi wa awali hawafikii wanavijiji 10, 000 walengwa ikimaanisha ya kuwa cost-benefit analysis yake iliyofanyika awali ilikuwa ni ya kupika jikoni tu isiyozingatia hali halisi ya taifa hili.........................................

c) Mradi huo umeshindwa kujiendesha wenyewe ikimaanisha ya kuwa gharama za uendeshaji zinazidi mapato halisi na hivyo kusababisha kuwepo msukumo mkubwa wa serikali kufikiria kutoa ruzuku.................................

d) Pesa zilizotumiwa kwenye mradi wa kwanza yaani zaidi ya bilioni 250 zingeliweza kujenga visima 10, 000 kwa Tshs 25 miliomi kwa kila kisima na hivyo kuwaondolea zaidi ya watanzania milioni 10 kero kubwa ya maji. Pesa hizo zilitumika kuwanufaisha watanzania wasiozidi 10, 000 na ambao wameunganishwa kwenye huduma hiyo ni chini ya watanzania 6, 000. Ikimaanisha mradi huu ni zigo kubwa kwa ujenzi wa taifa hili.............Yaani hauna manufaa kabisa..................

e) Pamoja na ya kuwa kunyonya maji kutoka Ziwa Victoria ni hasara na miradi hiyo kuishia kuwa ni "WHITE ELEPHANT" viongozi wetu wamekuwa wakiisisitiza kwa udi na uvumba kwa sababu za kujijengea mazingira murua ya kulipora taifa hili masikini sana duniani..............na kujinufaisha wao wenyewe na familia zao.....................................

f) Miradi ya kufyonza maji Ziwa Victoria inahatarisha usalama wa taifa ukizingatia ya kuwa nchi za Misri na Sudan ndiyo tegemeo lao walilopewa na Mwenyezi Mungu kujipatia nishati hiyo nyeti.............................sasa tuna sababu zipi za kuwakorofisha majirani zetu hao wakat hata sisi wenyewe tunajiandikia maumivu makali kwa kujitia hasara tupu?

Ni ukweli usiopingika ya kuwa "Profesa" Mwandosya yupo hapo kwa sababu za kuulinda ufisadi na elimu yake shupavu wala hatakaa aitumie kutokana na ulafi usiojua mipaka ...........ndani ya serikali ya CCM.................................

Ni vema ukaacha kupotosha Jamii,

Idadi ya wananchi wanaonufaika na huu mradi ni kubwa na kumbuka sio wananchi tu hata mifugo,,,sasa unataka kila kitu kiendeshwe kwa faida,,so unamaanisha na Mahospitali na yenyewe yaendeshwe kwa faida,,,kumbuka Mkoa wa SHINYANGA unatoa almasi na dhahabu ambayo inawaingizia watawala pesa si kidogo sasa wewe unaona part tu kidogo ya hiyo pesa ikitumika kuwapatia angalau hao wananchi maji safi na salama ni kosa

Tumechelewa maji ya ziwa Victoria hayatakiwi TABORA tu hayo maji yanatakiwa DODOMA mpaka Singida kwa garama yoyote
 
The late mwl.JK nyerere alipewa offer na Israel apelekewe maji to dodoma ,akakataa kwa sababu za kisiasa,ila kwa dunia ya sasa maji ni kama oil/petroli and nyuklia. Marekani wakulima na wafugaji wameshaanza majadiliano na kesi juu ya maji ktk mito and Aquifers.
Jordan kuna ubishi wa maji,Israeli wavuvi wanalalamika samaki wameisha ktk ziwa Galilaya kwa kuwa wakulima wanatumia maji mengi sana.
wazo tanzania ina maziwa mengine,like ziwa Nyasa and Tanganyika,ni heri kuweka mifereji/canals kama ulaya walivyofanya miaka ya 1880-to 1940's ila kwa ufisadi uliopo wa kukodisha magrader and excavators kwa 600,000 per day itakuwa balaa kwa mlala hoi
 
Back
Top Bottom