Mwandosya ajiuzulu?

Mwandosya ajiuzulu?

hali ya afya ya Prof. Haitii matumaini...anything ...its serious....though ilianza so simple...

Dira ya mtanzania NOT RELIABLE SOURCE ni gazeti ambalo linatangazwa sana na redio clouds haliaminiki.

Nashangaa sana kwa nini huyu mbunge wa Arumeru *magharibi* naye hajajiuzuru ubunge kwani tangu achaguliwe mwaka jana hata hakuapishwa na hajawahi kuhudhuria kikao chochote cha bunge.

hali ya afya ya Prof. Haitii matumaini...anything ...its serious....though ilianza so simple...

Nlitiwa moyo sana na habari hii hapa chini wiki iliyopita, wacha niendelee kuiamini..., urudi salama Prof..

Prof. Mwandosya aendelea vyema baada ya operesheni

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 17th August 2011 @ 23:00

WAZIRI wa Maji, Profesa Mark Mwandosya amesema anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa operesheni kubwa ya mgongo nchini India.

"Nikilinganisha na hali ilivyokuwa wakati nikija (hospitali India) kwa sasa naendelea vizuri nilikuwa na maumivu makali sana," alisema.

Profesa Mwandosya alisema hayo alipozungumza kwa njia ya simu na gazeti hili kutoka Hospitali ya Apollo nchini India.

Alisema madaktari walimfanyia operesheni kubwa ya mgongo na kumshauri kuendelea kupata matibabu hadi afya itakapokuwa nzuri ndiyo maana hadi sasa yupo hospitali.

Mwandosya ambaye aliondoka nchini takribani miezi miwili iliyopita, alisema baada ya operesheni hiyo kwa sasa madaktari wanamfanyisha mazoezi na wamemshauri aendelee kubaki kwa muda.

Alifafanua kuwa operesheni kama hiyo aliyofanyiwa inachukua mtu hadi miezi mitatu kuruhusiwa kutoka hospitali, hivyo anaamini ataruhusiwa kutoka madaktari watakapojiridhisha.

"Kwa sasa nasikiliza maelekezo ninayopewa na madaktari, wakiniruhusu nitaondoka wakati wowote," alisema Profesa Mwandosya na kuwashukuru watu kutoka kila pembe ya nchi ambao wanamtumia salamu za pole na kumtakia heri ili apone haraka.

Alisema salamu za pole zimekuwa nyingi sana, hivyo anawashukuru wananchi na kuwa hana maneno ya kusema kuhusu salamu hizo na upendo wanaouonyesha, zaidi ya asante.

"Nashukuru wananchi wanaonitakia heri, wapo ambao wangependa kuona narudi mapema…niwaambie tu, wasiwe na wasiwasi hali inaendelea vizuri," alisema Profesa Mwandosya.

Pia, aliwashukuru Watanzania waliopo India wakiwemo maofisa wa ubalozi ambao wamekuwa wakimtembelea mara kwa mara.

"Unapokuwa nje ya nchi, unatamani kurudi na mapenzi kwa nchi yako yanaongezeka maradufu," alisema Mwandosya, ambaye alikuwa akitoa vijembe na utani wa hapa na pale.

Kutokana na hali hiyo, Profesa Mwandosya hatakuwepo nchini wiki ijayo kuwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji anayoiongoza, hivyo jukumu hilo
atapewa waziri mwingine.

Kabla ya kuzungumza, chumba cha habari cha gazeti hili kilikuwa kikipokea taarifa tofauti kuhusu na afya ya mwanasiasa huyo

Kwa habari nilizopata ni kuwa Mh waziri mwenyewe ameshituka kupata habari hizi za kua kaandika barua ya kujiuzulu. so inaonekana hii habari si ya kweli

Nashangaa sana kwa nini huyu mbunge wa Arumeru magharibi naye hajajiuzuru ubunge kwani tangu achaguliwe mwaka jana hata hakuapishwa na hajawahi kuhudhuria kikao chochote cha bunge.

Mbaya zaidi ni kuwa kanuni zinazohusu maslahi yao wanazitunga wenyewe kupitia ile kamati yao. Anaweza kuendelea kulipwa hadi 2015 bila kukanyaga bungeni hata siku moja.

Mbaya zaidi ni kuwa kanuni zinazohusu maslahi yao wanazitunga wenyewe kupitia ile kamati yao. Anaweza kuendelea kulipwa hadi 2015 bila kukanyaga bungeni hata siku moja.

Ni kweli mbunge mzee Sumari hajaapishwa!?

Hivi Kisheria ni nani mwenye Mamlaka ya kutangaza Kujiuzulu kwa Waziri???

Je Katiba na Sheria za Tanzania zinasema DIRA ya Mtanzania ndio litatangaza Kujiuzulu kwa Waziri ?
Vp Ubunge nao atajiuzulu pia kama ni sababu za Kiafya!!!! na Ujumbe wa NEC je?

mtu mwenye akili atajiuliza maswali haya...hataanza kuhusiha swala hili na mbio za 2015

Je kama kiongozi wa nchi awezi semea maswala nyeti na hata hili uenda limemshinda ndio akaomba wa kumsemea. LOL

Dira ya Mtanzania chini ya kanjanja Charles Mulinda lini ikawa reliable source jamani? Tunasubiri official announcement kutoka Ikulu. Tunachojua Prof. bado yupo kwenye matibabu India na anasumbuliwa na tatizo la kansaya damu (Leukamia). Tunamuombea afya njema kama binadamu yeyote na si kufurahia mwenzio anapopigania uhai wake. He was not that bad guy wanajamvi!
hata hilo gazeti sidhani lina uhakika au wanaongea mambo ya kufikirika si juzijuzi tuu alikuwa kwenye maandamano Mbeya! I hope sio kweli labda nisikie kutokka Ikulu au at least magazeti yenye akili ila sio hilo.

Long Live Mwandosya kweli kama ni kupumzika wakati umefika akae chini ale pensheni

nasikia ni kwa sababu ya serikali dhaifu ya mkweleee na afya yake!

SISI MAGAMBA TUNASEMA ANATAFUTA UMAARUUFU HUYU!

Umaarufu mbona anao atashirikiana je na serikali legelege? Ni bora akae pembeni serikali itakapoanguka asiwemo

Ndo maana labda anaumwa!pressure inapanda na kushuka!

La bajeti hata halimnyimi usingizi..yeye URAIS bwana???..tumuombee Mungu..apone ....though ni ukweli kuwa anahitaji matibabu ya muda kiasi..lets wait and see...

nimeikumbuka hii:Wanawake wanyimeni unyumba waume zenu kama watawaunga mkono wapinzani: Sofia Simba

Mbona yeye hanyimi au alitaka kuaribu ndoa za watu ndo aone raha

Back
Top Bottom