Mwandishi wa habari Idhaa ya Kiswahili ya DW akutwa hajitambui ndani ya basi

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,745
4,277
Mwandishi wa habari wa Idhaa ya Kiswahili ya sauti ya Ujerumani (DW) Deokaji Makomba amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma nchini Tanzania kwa kile kinachoelezwa amelishwa sumu.

Deokaji alifikishwa hospitalini na polisi jana Ijumaa Januari 3, 2020 saa 2 usiku akiwa hajitambui.

Polisi walimpata Deokaji baada ya basi la Ally's kumpeleka hapo akiwa hajitambui na waligundua wakati abiria wengine wakishuka ndipo wakamuona akiwa amelala hajitambui na hana kila kitu.

Mwananchi limefika alipolazwa Deokaji wodi namba nne kitanda namba saba licha ya kuelezwa anaendelea vizuri, lakini bado hana nguvu na anapenda kulala.

Akizungumza kwa tabu, anasema walitoka Mwanza kwa basi la kampuni ya Ally’s lakini alikuwa na fahamu hadi walipokaribia Bahi (Dodoma) ndipo hakujua kilichoendelea hadi alipojikuta yupo hospitalini.

"Wakati tunatoka Mwanza, nilikaa na mama mmoja lakini alishuka njiani ndipo akaja mwanaume aliyejitambulisha anafanya kazi uhamiaji, katikati ya Manyoni kuja Bahi, mwenzangu alikuwa anakula biskuits akanipa kama vipande viwili au vitatu na baada ya kula sikumbuki kama Bahi niliiona hadi nimestuka leo niko hospitali," anasema.

Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Erenest Ibenzi amesema hakuwa na taarifa za mgonjwa huyo akiahidi kufuatilia.

Chanzo: Mwananchi
 
Kwa taarifa ya haraka haraka tunapata picha ya biscuits ndiyo chanzo na zilikuwa na sumu.

Otherwise ndugu mwandishi angalia story zako kama zina mlengo wa kuchafua nchi yako ili wewe uonekane mwandishi wa viwango.

Hata hivyo pole sana.
Mimi nahisi alimpa biskuti hakudhamiria kuua ila alidhamiria kuiba so biscuit ilikua n amadawa ya kulevya tuuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu tunatofautiana sana!

Sijawahi hata kuzoeana na strangers kwenye vyombo vya usafiri hata kama safari iwe ndefu vipi tutasalimiana then sina habari.

Mtu akijidai ukarimu na kujitambulisha ofisi safarini jua limbwata hilo soon utalizwa!
 
Kwa taarifa ya haraka haraka tunapata picha ya biscuits ndiyo chanzo na zilikuwa na sumu.

Otherwise ndugu mwandishi angalia story zako kama zina mlengo wa kuchafua nchi yako ili wewe uonekane mwandishi wa viwango.

Hata hivyo pole sana.
Mkuu unataka watu wasitoe taarifa ?, hata kama ni uzalendo uchwara, hautafutwi kwa style hiyo, mtu ametoa habari, kama hupendi unapita kimyakimya, hii itakuwa serikali kupitia kwa mawakala wake wa udhalimu
 
Back
Top Bottom