Mwandishi Munga Tehenan: YUPO WAPI?

R I P Munga
Kiukweli mafundisho yako ndio yaliyoniongoza sana kiasi kwamba leo hii sitetereki kabisa,
Nimekuwa sio mtu wa kuongozwa na hisia bali mimi ndio huongoza hisia zangu.
Nyumba ya utambuzi ilikuwa pale Rombo karibu na kona kimara,huyu jamaa alikuwa kichwa sana ila sijawahi kujua alikufaje.
 
Nyumba ya utambuzi ilikuwa pale Rombo karibu na kona kimara,huyu jamaa alikuwa kichwa sana ila sijawahi kujua alikufaje.
Mi nilikuwa nafatilia makala zake kwenye magazeti ya Jitambue tu. Tena kipindi hicho nilikuwa bado mdogo sana kiasi kwamba binafsi sikuwa na hela hata ya kununua gazeti hivyo kama baba hakuleta hilo gazeti basi siku hiyo nilikuwa nakosa raha.
Pia nimekuja kupata video zake mwaka huu huu ila kumbe tayari ameshaucha mwili
 
Mi nilikuwa nafatilia makala zake kwenye magazeti ya Jitambue tu. Tena kipindi hicho nilikuwa bado mdogo sana kiasi kwamba binafsi sikuwa na hela hata ya kununua gazeti hivyo kama baba hakuleta hilo gazeti basi siku hiyo nilikuwa nakosa raha.
Pia nimekuja kupata video zake mwaka huu huu ila kumbe tayari ameshaucha mwili
Naomba uni_PM hizo video japo moja please.....na kama vip naweza kupatia ka namba ka whatsup unitumie kama hautajali mkuu.
 
Hata mimi niliwahi kusoma makala zake fulani, nikazipenda sana. Kama nakumbuka vizuri kichwa cha habari cha makala yake mojawapo kilikuwa "MAKUWADI WA MABOSI" na kama nimekosea, wenzangu mliopata kusoma hii makala, kama haikuwa yake, mnisahihishe. Naikumbuka hasa kwasababu ilikuwa inahusu tabia za baadhi wafanyakazi ambao hupenda kujipendekeza kwa mabosi na kuwasaliti wenzao kwenye masuala ya kudai haki na maslahi mbalimbali kazini. Watu wa aina hii wapo wengi hata sasa kwenye siasa na vyama vya wafanyakazi; na ndio hao ambao wakijipenyeza kwenye uongozi wa vyama huyumbisha umoja na kurudisha nyuma juhudi za vyama hivi katika kusimamia mambo mengi ya wanachama au wafanyakazi.
RIP Munga T.
 
Ndugu zanguni, nimeshtushwa sana na habari hii,
Kumbe ndugu yetu Munga Tehenan alishatangulia mbele ya haki?

Bwana alitoa, na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe. Amen.
Muda mrefu sana nilikua ni mmoja wa kufatilia habari zake... Munga tehenani Kuna mambo alinishauri vizuri sana... Nilitamani ifike jumatano ninunue gazeti Lake la kutambue mpk leo nina stoo ya magazet yake.. Alitutoka mapema mnooo. Bado tulikua tunamuhitaji.. Mungu amlaze mahali pema peponi
 
Hivi hakuna mwenye elimu ile so far hapa Tz...mmmmh
Muda mrefu sana nilikua ni mmoja wa kufatilia habari zake... Munga tehenani Kuna mambo alinishauri vizuri sana... Nilitamani ifike jumatano ninunue gazeti Lake la kutambue mpk leo nina stoo ya magazet yake.. Alitutoka mapema mnooo. Bado tulikua tunamuhitaji.. Mungu amlaze mahali pema peponi[/QUOTE]
Hivi hakuna mwenye elimu ile so far hapa Tz...mmmmh
 
Wadau naomba kujuwa alipo mwandishi maarufu wa makala, na one time mhariri na mmiliki wa gazeti la JITAMBUE.

Ameandika vitabu vingi vya lugha na hadithi, na kuna wakati alikuwa na TALK SHOW pale TBC1 Wakati ikiwa TVT. Pia amewahi kuwa Majira Publishers, nadhani mhariri wa vitabu among other things...

MHARIRI, MUNGA TEHENAN!
duu imenikumbusha mbali ..sana enzi za miaka ya mwanzo ya JF ....RIP MUNGA TEHANAN

PALE KIMARA KULIKUWA NA NYUMBA YAKE AMEANDIKA JITAMBUE HOUSE
 
Ndio sababu yagazeti lajitmbue kutotoka tena mpaka leo alikufa muda sana nilikuwa namwelewa sana huyu bwana hasa kwenye kioengele chake ktk gazeti lajitambue kinaitw JINSI NILIVYOFEDHEHEKA, R.I.P Munga Tehenani
 
<br />
<br />




Hata Mimi sielewielewi ninayoyasoma hapa,Munga Tehenan anawezaje kufa halafu habari yake iwe siri? Media haiku-cover habari hii?
Mm amenisaidi sana,Tehenan nilikuwa sikosi Gazeti la Jitambue,hata siku moja sikosi!!
Amenisaidia saaana,i never thot kwamba hatunaye kimwili tena,duuuuh!!!
2008 ni Mwaka Juzi tu,ama kweli Media za Bongo ni zaidi ya huzijuavyo!!!
Chanzo chagazeti lajitambue kutotoka nikifo chake nasio mwak juzi nimuda zaidi yamwKaka juzi
 
Tutajaribu kutengeneza mashujaa fake (chui wa karatasi) lakini mwishowe tutawatambua kwa matunda yao hivyo kuamua kurudi nyuma na kuwatambua mashujaa wa kweli ndilo naliona hapa!
Sio rahisi kugundua kuwa baada ya watu wa aina ya Munga Tehanan kuondoka ndio mambo yameanza kutepeta kila mahali. Asante sana JF kwamba huyu mtu amewahi kujadiliwa hapa na kumbukumbu zake zipo ili kutusaidia kujua kuwa uandishi sio kushika karamu tu bali kuna vitu vya ziada unavyotakiwa kuwa navyo kama alivyokuwa huyu bwana. Nafurahi pia kuwa nilibahatika kukutana naye ana kwa ana japo haikuwa official lakini nilibaki na kumbukumbu.
 
habari hii imenisikitisha sana , nilikuwa sijui kama Munga wa gazeti la jitambue alikufa. mke wangu (enzi hizo akiwa girlfriend) alikuwa anapenda sana magazeti yake... nimemwambia katoa machozi!! nitakupigia
Pole kanyagio ila alikufa miaka mingi nandio chanzo chagazeti lajitambue kufa kabisa, r.I.p munga tehenan
 
Nilikuwa madongo kuinama sikuwa na mawasiliano na dunia ya umeme.
Nimesikitika sana.
Pole sana kamanda. Yule jamaa na timu yake walikuwa ni wako vizuri sana na muhimu sana hasa kwenye suala la saikolojia
 
Munga alikuwa tofauti na waandishi wengi ambao waliamini ili habari zao zisomwe ama waandike habari za siasa, mapenzi au michezo yeye alijikita zaidi kuandika mambo yanayohusu jamii na suluhisho lake alikuwa anaeleza vizuri mambo ya dini bila mtu kujua yeye dini gani pia hata mambo ya ushirikina pia alikuwa akielezea kwa ufasaha ni mwandishi ambaye mpaka sasa sijaona pengo lake likizibika binafsi namkumbuka wakati akiandikia gazeti la cheche,Dar leo na jitambue
 
Back
Top Bottom