Mwandishi Josephat Isango abeza kasi ya Magufuli

Mwandishi Josephat Isango abeza kasi ya Magufuli

Hawana uweledi hawa waandishi wa habari wetu kwanza vigeugeu sana...

Mimi nimeacha kusoma magazeti kwani akina Isango wamechanganyikiwa tangu ukawa walipokosa urais. Anayemlaumu rais Magufuli apimwe akili. Hilo baraza la mawaziri lisingefanya kazi alizofanya mpaka sasa. Mwacheni aweke msingi ili wateule wawe na mwongozo wa kufanya kazi kwa kasi na weledi wake.
 
Nimeshangaa kumuona kwenye kipindi cha matukio cha EATV akibeza kazi ya Magufuli inayoendelea. Eti Magufuli anavunja sheria!

Anaendelea kulilia baraza la mawaziri litangazwe ili mawaziri watakaoteuliwa wapate muda wa kujiandaa kujibu hoja za wabunge.

Ushauri wangu kwa waandishi wa habari ni mmoja tu. Wakae kimya kwani mwaka huu wameshindwa kutumia kalamu zao kutuwekea Rais wa hovyo hovyo.

mod weka kitufe cha likeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Haya ni maoni yake na ya watu wengine pia. Urais ni taasisi na siyo one-man-show. Hivi fedha anayoelekeza kwenye barabara na hospitali imeidhinishwa na nani? Nani atafuatilia matumizi yake?
Fedha za kununua vitanda ilienda moja kwa moja MSD.
 
Aweke wazi itikadi yake kwanza! Ndo hao baada ya kula, kushiba na kuvimbiwa walikuwa wakisema Serikali ya CCM kwa miaka 54 haijafanya kitu chochote, wengine wakiwa ni viongozi wakuu wastaafu, ambao kama isingekuwa Katiba kutowaruhusu kuendelea, wangekuwa madarakani hadi leo!
 
Hivo yale majina ya wakwepa kodi ambayo yamesitiliwa ni akina nani?! Au inagusaa wajumbe wa CC?!
 
Hoja yake ni kwamba mawaziri watakaoteuliwa kwa kuchelewa watashindwa kujibu hoja za wabunge.

This is nonsense!

Mbona hoja inaeleweka. Bunge ni mwezi ujao bado mawaziri hawajateuliwa huoni tatizo
 
Josephat Isango yuko sahihi kabisa, watu wanaosifia sifia kila kitu bila kujipa mda wa kutathimini ni mabwege tu. hizo ni tabia za kike,watu wenye akili lazima tuusceen huu utawala wa Mwalimu Magufuli,

Walitaka Isango aseme, " Magufuli kwa utendaji huu asiunde kabisa baraza la mawaziri maana yeye na PM wanaweza kabisa. Pia ikiwezekana hata Bunge alivunje tuu kwa Wananchi wameonyesha kuwa na Imani naye kwa siku hizi 30 alizofanya kazi"
Hizo zingekuwa akili matope kabisa. Anachohoji Issango ni sahihi.
 
Nimeshangaa kumuona kwenye kipindi cha matukio cha EATV akibeza kazi ya Magufuli inayoendelea. Eti Magufuli anavunja sheria!

Anaendelea kulilia baraza la mawaziri litangazwe ili mawaziri watakaoteuliwa wapate muda wa kujiandaa kujibu hoja za wabunge.

Ushauri wangu kwa waandishi wa habari ni mmoja tu. Wakae kimya kwani mwaka huu wameshindwa kutumia kalamu zao kutuwekea Rais wa hovyo hovyo.

Msafara wa mamba haukosi kenge
 
RIP Isango
Paskali
 
Back
Top Bottom