Mwandishi Josephat Isango abeza kasi ya Magufuli

Mwandishi Josephat Isango abeza kasi ya Magufuli

Ah watu woote hawatampenda rais jpm lakini wengi tukonae hivo hayo ni mambo yake na maonivyake
 
Nimeshangaa kuona mtu akijitambulisha kwa jina la ISANGO akiponda jitihada za Mh. JPM! Nikajiuliza kama ni mwandishi wa kusomea au kudandia maana alionesha weledi finyu wa uandishi wa habari na chuki za wazi kwa Serikali ya CCM baada ya aliyemtarajia kuangukia pua. Kama kiwango na weledi wa waandishi wetu ni mfano wa huyu basi mitaala ya uandishi wa Habari na Vyuo vimulikwe!
 
Yeyote anaempinga JPM kwa hatua anazochukua hivi sasa hana chembe ya uzalendo kwa Tz.
Tuweke pembeni mambo ya u-chadema na u-ccm, Mh Rais anapiga kazi.
 
Tukubaliane na JPM kupingwa sababu its only the way italeta check and balance ya utawala wake wote Tukikubalianae tunaweza pelekwa pabaya maana madaraka nayo yana ulevi wake ...
 
Uloi nga mâché68;14814074 said:
Nimeshangaa kuona mtu akijitambulisha kwa jina la ISANGO akiponda jitihada za Mh. JPM! Nikajiuliza kama ni mwandishi wa kusomea au kudandia maana alionesha weledi finyu wa uandishi wa habari na chuki za wazi kwa Serikali ya CCM baada ya aliyemtarajia kuangukia pua. Kama kiwango na weledi wa waandishi wetu ni mfano wa huyu basi mitaala ya uandishi wa Habari na Vyuo vimulikwe!

Nadhani hata chombo kilichompa air time sidhani kama kina umakini wa kujua kimualike nani kuongelea nini,mada ilikuwa nzuri lakini ilikosa mtu mweledi wa kuongea,ni vyema waandishi na wataalam wengine wanapokuja hewani wajipange na kutofautisha kati ya kuongea kwenye public na kuongea kimtaani.wamiliki wa vyombo vya habari nanyi tunawategemea mtuletee watu wajuzi na weledi kwenye jambo husika mnapoamua kulichambua jambo.Jamaa alikuja kakariri jambo moja tu,eti mawaziri watakosa muda wa kujiandaa kujibu maswali ya wabunge.
 
ha ha ha ha ha ha ISANGO tapeli tu alikua TEAM LOWASA sasa hajakubali matokeo kama jamaa kaanguka
 
Waandishi wenzeke wenye weredi wanapaswa kuhiji hili kama kweli huyo mwenye post/ thread ni mwandishi mwenye weredi. Other wise apotezewe tu.
 
In the world we have different classes of people, bad and good but all are human beings. So, We must forgive each other.
 
Isango anasema ukweli Magufuli mpaka sasa ni media monger hakuna jipya alilofanya tofauti na maraisi wenzake wa CCM wanaanza kwa mikwala hivyo hivyo fagio la chuma, Mwinyi, upambanaji na rushwa,kapa kufuta mikataba mibovu Kikwete na wote hakuna aliyefaya itu huyu naye mbwemwe tu nguvu ya soda hana muda
 
Mimi binafsi nilikuwa naiheshimu sana EATV na hasa kipindi hicho cha hot mix,lakini kwa leo wamenivunja moyo,unawezaje kumleta mchambuzi WEAK kama yule kwenye issue sensitive kama ile?!kwani mbona watu waliobobea kwenye uchambuzi wa siasa ni wengi tu,unless kama tumeamua kulidhihaki neno "mchambuzi",mchambuzi ambaye mara kadhaa nae akawa anachambuliwa na mtangazaji kwa kukosolewa!au alipoalikwa kuja kuchambua alidhani anakuja kuchambua mchicha?
Kwa maoni yako lakini kwa sisi wengi kaongea ukweli magufuli hana jipya so far
 
Nilimuona huyo mtu akizungumza lakini nilichogundua ni miongoni mwa wale wasioridhika na jambo lolote linalofanywa na mtu wasio mtaka ni sawa na Kingunge na wenzake kwao ccm ingekuwa nzuri tu kama mtu wao angepitishwa lakini kwakuwa haijawezekana basi wao ni kuponda kila kitu yaani ni aina ya watu wenye chuki binafsi
kwenye mizania Magufuli bado amepata tu publicicity waandishi munawaponda ukweli ndio wamempamba kwa sababu wanaandika tu kama makasuku kwa mfano amefufua mashine za MRI na C-T scan haulizwi Magufuli kwa nini serikali ya CCM hapo awali ilikuwa hailipi madeni
 
Huhitaji kuwa mpenzi wa Magufuli ili ukosoe kwa mantiki!
Think critically and not differently!!

Upotevu huo huo wa JK mpaka akaitwa chaguo la Mungu. Kikwete angelikuwa ameweka institutions imara za kufanya kazi, asingeliishia kuondoka na aibu ya kushindwa nchi! Huyu JPM ataishia hivyo hivyo kama hataweka institutions za kumfanyia kazi na kuweka mifumo ya kupata feedback. Let him do what he is doing now and he is fine by that, BUT akumbuke kuweka Katiba to take care of all those he is doing. Hatapata malaika! hata atakao waweka wote ni product za wezi. Aweke mifumo itakayofanya kazi anazozitaka. Checks and balances za uhakika. Let him do an immense research on that to identify which ones can make sense while he is tumbualing majipu!
 
Wananchi hatuhitaji mawaziri

kwanza Nani kamwambia wanahitaji hoja sijui majibizano ya wabunge na mawaziri

Sisi tunataka kazi tu siyo porojo bungeni
 
Itabidi itwengwe siku maalumu kwa ajili ya kumsifu na kumwabudu Magufuli, maana yaonekana ukiwa na mawazo tofauti we niwa shetani
Kula LIKE tena iwe 5 Nov kila mwaka maana imekuwa too much!.Amguse na mtoto wa mfalme aliyepita ndio tutajua anachofanya si viini macho!
 
ha ha ha ha ha ha ISANGO tapeli tu alikua TEAM LOWASA sasa hajakubali matokeo kama jamaa kaanguka

Mwenzenu anajaribu kuhalalisha mshiko aliopewa wakati wa kampeni za uchaguzi ili aonekane kufanyika kazi
 
Jipu la mauzo ya nyumba za serikali litampasukia mwenyewe magufuli!!!! na usaha utakaotoka utamchafua nguo zake zote.

SIKU HIYO INAKUJA.

Too late! Hoja hiyo imeshindwa kuwa na impact katika kampeni na kura ni basi tena. He is now the President.
 
Nimeshangaa kumuona kwenye kipindi cha matukio cha EATV akibeza kazi ya Magufuli inayoendelea.

Eti Magufuli anavunja sheria !

Anaendelea kulilia baraza la mawaziri litangazwe ili mawaziri watakaoteuliwa wapate muda wa kujiandaa kujibu hoja za wabunge.

Ongea yake pake studio iliashiria kuwa ni mtu alijidunga viroba kabla ya kuingia studio.

Ushauri wangu kwa waandishi wa habari ni mmoja tu...

Wakae kimya kwani mwaka huu wameshindwa kutumia kalamu zao kutuwekea Rais wa hovyo hovyo.

TOKA LINI NAWE UMEANZA KUMILIKI UHURU WA MTU KUJIELEZA?
-Kama hukubalini nae nawe andaa kipindo EATV na siyo kuja na thread za kitoto ati kisa KABEZA USANII WA MAGUFULI!
 
Nimeshangaa kumuona kwenye kipindi cha matukio cha EATV akibeza kazi ya Magufuli inayoendelea.

Eti Magufuli anavunja sheria !

Anaendelea kulilia baraza la mawaziri litangazwe ili mawaziri watakaoteuliwa wapate muda wa kujiandaa kujibu hoja za wabunge.

Ongea yake pake studio iliashiria kuwa ni mtu alijidunga viroba kabla ya kuingia studio.

Ushauri wangu kwa waandishi wa habari ni mmoja tu...

Wakae kimya kwani mwaka huu wameshindwa kutumia kalamu zao kutuwekea Rais wa hovyo hovyo.
Huyu jamaa alikuwa anamtaka Lowasa iwe jua iwe Mvua, sijui aliingia kwenye payroll???
 
Huyu jamaa alikuwa anamtaka Lowasa iwe jua iwe Mvua, sijui aliingia kwenye payroll???
ndio chaguo lake hakuvunja kipengele chochote cha katiba magufuli aliyepachikwa kwa mwezi mzima anafanya mazingaombwe tu
 
Back
Top Bottom