Mwandishi Josephat Isango abeza kasi ya Magufuli

Mwandishi Josephat Isango abeza kasi ya Magufuli

meningitis

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Posts
8,464
Reaction score
4,832
Nimeshangaa kumuona kwenye kipindi cha matukio cha EATV akibeza kazi ya Magufuli inayoendelea. Eti Magufuli anavunja sheria!

Anaendelea kulilia baraza la mawaziri litangazwe ili mawaziri watakaoteuliwa wapate muda wa kujiandaa kujibu hoja za wabunge.

Ushauri wangu kwa waandishi wa habari ni mmoja tu. Wakae kimya kwani mwaka huu wameshindwa kutumia kalamu zao kutuwekea Rais wa hovyo hovyo.
 
Hii ni habari, opinioni au kero?
Hebu jipange mkuu tuliza panick na utueleze kilichojiri halafu tuanze kudadavua mada.
 
Hawana uweledi hawa waandishi wa habari wetu kwanza vigeugeu sana...
 
magamba toka mh rais amegusa vipele kidogo wana nyodo kweli,kila wakati wananyanyua midomo juu utafikiri kabla ya magufuli kushika nchi,nchi ilikuwa inaongozwa na cuf au chadema
 
Sasa hivi magufuli ni mungu. Ni bora kuanza vibaya kuliko kumaliza vibaya
 
Jipuu kuu la Zanzibar limeshindikana nini? Dhulma kwa wanzazibari na Ukiukaji wa katiba hadi lini?
 
Hata mm nilimsikiliza nikajiapiza mtoto wangu akiniambia anataka kua mwanahabari, tamchapa vibao.
Halafu nyinyi EATV mmekosa wachambuzi!
 
Tuliosoma nae SAUT akiwa mbele yetu mwaka mmoja BAMC 2005 hadi BAMC 2008 huku tukishinda nae ktk vijiwe vyote vya pale nsumba - malimbe na mara nyingine akituacha kwa kututoroka kwenda kunywa gongo zake maeneo ya kule sweya akiwa na wale wavuvi tunasema tunawaombeni sana radhi kwa wote mlioumizwa na alichokisema.

Hii ni sehemu ndogo sana ya mapungufu yake ambayo kama nikiyaweka humu hadharani mnaweza kulia kwa uchungu mkubwa sana na hata pengine kumuonea huruma. Mwenyezi Mungu amsamehe tu.
 
kuna watu wanataka tufikirie kama wao kwa kila kitu...mmoja wapo mleta mada,ukifikiria tofauti kosa,,,,hivi hoja ya kuchelewesha cabinet aliyotoa isango ina tatizo gani
 
Tena wakome kabisa wasituzoee na uandishi wao uchwara usiokuwa na maana isango mwenyewe anahongwa mpaka elfu kumi tu.
 
Back
Top Bottom