Mwanaume Vyakula gani unaweza kupika?

Behind the camera

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
226
500
Ukiachana na wale wenzetu ambao wamesomea elimu ya kupika Vyakula mbali mbali, kuna sisi wapenda kula lakini kupika mtihani.

Leo nimejiskia kupika firigisi na ugali. Sema hapa kwenye firigisi najiona kabisa nimechemka

Aisee mpaka nimemkumbuka mama watoto aliyekwenda kujifungua huko mkoani Tanga.

Chakula gani ewe baba/kaka/baby

Kinakusumbua kupika? Au ni mwenzangu na mimi?
 

Fereke

Member
Apr 13, 2011
91
150
Mimi nilikuwa namuona Baba yetu..mama akisafiri tuu au kuumwa.basi yeye alikuwa anaahirisha outing zake zote sijui kunywa au marafiki baa...akitoka kazini anawahi home.

Anatupikia yaani saa 11 jioni chakula cha usiku tayari..SAA12 mezani mnakula..dah saa mbili wote kulala..tulikuwaa tunachukia...utoto tuu tulikuwa hatuelewi.

Anatufulia nguo,anatunyoshea na mengine mengi tuu.

Nilijifunza mengi sana..suala la mwanaume kupika kufua ni mtizamo tuu..

Kuna kipindi nikakaa kidogo huko nje ndio nikajifunza zaidi.
Maisha yangu yote ya gheto nafurahia chakula nachopika mwenyewe...

Nikiwa ofisini nikitamani chochote nawauliza staff wenzangu ambao ni wanawake wanifundishe ..wanielekeze kupika aina fulani ya Chakula..nanunua mahitaji nikiwa home napika mwenyewe nafurahia maisha..kwa njia hiyo nimejifunza kupika vyakula vingi sana sana.

Hata nilipokuja kuoa aaa wife ndio anajua raha yake..nikajifunza mapishi mengi kwake..nikawa bora zaidi..

Kwangu kupika sio ishu kabisa kabisa..nilifundishwa tangu darasa la kwanza na mama na ilikuwa lazima tukakua tumezoea naona poa tuu.
 

Behind the camera

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
226
500
Mimi nilikuwa namuona Baba yetu..mama akisafiri tuu au kuumwa.basi yeye alikuwa anaahirisha outing zake zote sijui kunywa au marafiki baa...akitoka kazini anawahi home.
Anatupikia yaani saa 11 jioni chakula cha usiku tayari..SAA12 mezani mnakula..dah saa mbili wote kulala..tulikuwaa tunachukia...utoto tuu tulikuwa hatuelewi...
Hongera mkuu
 

SK2016

JF-Expert Member
Apr 6, 2017
7,887
2,000
Ugali ,wali na dagaa, samaki na nyama na mboga.

Mengine sijui kabisa, nayakuta kwa mama ntilie huko nje.
 

denis fourplux

JF-Expert Member
Aug 17, 2017
837
1,000
Chips, pilau, chapati, pizza, biriani, Tender chicken, wali ata kwenye gasi, mboga zote tena kwa karanga au nazi,rosti la nyama na Main ya kuku, samaki rosti, Tambi za nazi, mandazi na keki.

Inshort najua vingi vingine nimejifunza kupitia youtube vingine utundu n vingi n mazingira sisi tusiokua na wazazi malezi yalitufany tujifunze vyote kupika mpk kazi nyingine
 

Patra31

JF-Expert Member
Apr 24, 2020
685
1,000
Mimi kila ninachopenda najua kukiandaa mwenyewe na sijasomea sehemu. Wali, ugari, ndizi, miogo, samaki, dagaa, nyama aina zote zinazoliwa, mboga za majani, maandazi, cake,pilau, bagia, nk nimechoka kuandika.

Yan Kiukwel mother alitulea vizur watoto wake sema ujana ndio ulituharibu
 

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
16,721
2,000
Nasubiria nipate mualiko wa kwenda kula msosi aliopika mwana JF. Ila niwepo akiwa anaanza kupika hadi mwisho sio nikute ameshapika hapana.

Tomaso Kasinde.
 

isajorsergio

Platinum Member
Apr 22, 2018
2,755
2,000
Binafsi nimejikuta napenda kupika na kuhusudu ladha ya mikono yangu.

Naweza kupika ndizi na kumenya pia, chapati za kusukuma na maji, wali, ugali, tambi, chips, mboga aina mbalimbali, kwa ufupi napika vyakula vyote muhimu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom