Brigedia Chan-ocha
JF-Expert Member
- Mar 7, 2014
- 1,353
- 2,846
Jana baada ya kutoka kazini, nilikuta ugomvi kwa jirani yangu ambaye alikuwa ameenda likizo na mkewe sasa wakati wanataka kurudi kazini ikabidi wapiti kwao mwanamke kuwasalimia, sasa zogozogo lilianza hapa, baada ya kufika kwao mwanamke, walikaribishwa vizuri na wakaoga, wakala na sasa ikafika zamu ya kwenda kupumzika.
Sasa mwanamke kumbe alikuwa ameshamtaarifu boyfriend wake wa siku nyingi hapo mtaani kwao kwamba nitakuja siku fulani, siku hiyo wakati wa kulala, mwanamke alikataa kulala na mumewe ndani ya nyumba yao binti (nyumba ya ba mkwe), eti akidai (mwanamke) kwamba siyo vizuri kulala pamoja eti yeye na mumewe kitanda kimoja kwenye nyumba ya baba yake, akihoji je, ikitokea "mwanaume akahitaji mchezo"?
Basi jamaa (mumewe) ikabidi awe mpole amruhusu mkewe akalale chumba kingine lakini ndani ya nyumba hiyo, sasa mkewe akatumia mwanya huo, kufungua mlango na kwenda kwa ex boyfriend wake wa muda mrefu, akarudi asubuhi ya saa 11 alfajiri.
Wakati anarudi akakutana na baba yake nje, ndo baba yake akaanza kumuuliza anatoka wapi usiku huo yeye peke yake huku akihoji mume wake alipo! Kumbe wakati anamuhoji mkewe, mumewe alikuwa anasikia maana dirisha la chumba alicholala mumewe lipo upande wa getini, mke wake alishindwa kutoa majibu yoyote huku akiomba radhi kwa baba yake tena kwa sauti ya kunong'oneza sana.
Kumbe mumewe alisikia yote na alipoamka alikaribishwa chai akanywa na baadae akaomba kuondoka ili kuwahi kazi akidai likizo yake ilikuwa imekwisha.Wakaondoka pamoja na mkewe, sasa kufika nyumbani ndo maswali yakaanza na ugomvi mkubwa umetokea jana, na ikabidi mwanaume ampe nauli mkewe arudi kwao kwanza ili atafakari hatua nzuri za kuchukua dhidi yake.
Kiufupi, Mwanamke hakukubali kosa, alikataa ila mmewe alipomuuliza swali aliloulizwa na baba yake juzi na jibu ambalo yeye alimjibu baba yake ndipo mwanamke akaishiwa nguvu, mumewe akamwambia nguo aliyovaa siku hiyo ya alfajiri na baba yake alivyokuwa amevaa siku hiyo ya alfajiri.
Sasa ndugu zangu wanaume kazi kwetu kwa wale mliooa tayari kazi kwenu, sisi wengine tunajifunza kwanza.