Mwanaume una faida gani kwenye ndoa?

ContinousImprovement

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
290
268
Tumegombana sisi, kaamka kwa hasira, alikuwa ananyonyesha mtoto nikamwambia niachie mtoto. Sasa mtihani mtoto analia anataka kunyonya. Bado kidogo na mimi nilie sikujua nifanyeje? Nikawaza nimpe maji nichanganye na Glucose? Hapana. Ikabidi nirudi kwa wife nikambembeleza anisamehe. Aamke ampe mtoto nyonyo.

Mtoto alikuwa analia sana. Nusura na mimi nilie. Sikutaka kuonyesha kwamba I can handle the kid bila yeye kwa kumpa chakula au kumuandalia kitu kwa kisingizio cha mimi kulala kuonyesha kwake kuwa namjali mtoto.

Wake zetu wana mbinu nyingi za kutikisa kibiriti. Ila nimewaza, wanaume tuna msaada gani kwenye Familia? Au ni kuleta hela tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoto alie, mke alie na mme tena anataka kulia, blaza chunga sana.

Nakuelewa. Nilikuwa na hasira. Ila nililazimika kujizuia maana alikuwa very provocative.

Sikuielewa coonection ya ugomvi wetu na kuzuia mtoto kunyonya.

Mara kadhaa nilikuwa najaribu kumuamsha kwa nguvu ili mtoto anyonye. Hapo ndipo niliona kama ningeendelea basi ningemdhuru.

Lakini Sasa mtoto ananyonya.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bro! Kama umeoa na hujui faida ya baba katika ndoa, unaniaminisha kuwa bado hustahili kuoa!

Nimewaza. Wakati mtoto analia nilikosa cha kufanya. Maana sikutaka kuprolong tatizo.

Kamangempa maji, ningempa kwa Muda gani? Eventually mtoto alitakiwa kunyonya.

Ilikuwa ni lazima niongee na Mama yake akubali amchukue amnyonyeshe.

Hapa ndio niliona sina ujanja.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimewaza. Wakati mtoto analia nilikosa cha kufanya. Maana sikutaka kuprolong tatizo.

Kamangempa maji, ningempa kwa Muda gani? Eventually mtoto alitakiwa kunyonya.

Ilikuwa ni lazima niongee na Mama yake akubali amchukue amnyonyeshe.

Hapa ndio niliona sina ujanja.


Sent using Jamii Forums mobile app

1. Unanishangaza unaposema hujui ufanye nini kwa mtoto wako? Like serious? Inaonyesha wewe huna muda na familia kabisaa, unapaswa ujue mambo mbalimbali yahusuyo wanao maana kuna mkeo kuumwa ghafla hapo akapoteza fahamu mtoto utampa nani akulelee? Ndiyo maana hapo juu nikasema hujafikia hadhi ya kuitwa baba!

2. Huna mazoea na mwanao ndiyo maana kakuliza baba zima! Unatakiwa mtoto wako akujue, akikuona aone katatuliwa matatizo yake yote. Siyo baba humjui mtoto na mtoto hamjui baba duuuh, watakuita mkoloni! 😂😂

3. Hivyo viugomvi vya kususiana watoto ni upuuzi wa hali ya juu, kwa uzoefu wangu huyo mtoto mpaka kalia alishahangaika na hiyo njaa sana, maana najua wana sign za awali kuonyesha njaa. Kwa nini usitafute suluhu kabla ya kuleta matatizo mengine, ulimng'ang'ania mtoto wa nini na hujui anakula nini!? Ni upuuzi mkubwa, jifunze kuepuka matatizo madogo madogo katika ndoa yatayopelekea mtoto kuathirika!
 
Mm wife nilimpa vitasa, nikamtoa sebuleni baadae nikafikiria dogo akiamka sijui itakuaje! Nikamfata nikamwambia"Nakupa dakika tano uwe umeshalala kitandani" akaenda chumbani faster.

Huyo wa kususia kunyonyesha angekuwa wa kwangu sijui ingekuwaje

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi kupiga wanawake hasa mkeo ni ujanja?

Tena unajisifia kabisa kwenye mitandao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom