Mwanaume ndiye mwenye maamuzi ya mwisho

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,738
3,199
Mniwie radhi kwa kukosa maneno mazuri ya kubeba ujumbe huo kwa kiswahilini Sanifu.naamini ujumbe unaeleweka kwa wadau.

Katika mahusiano yoyote ya ndoa au urafiki wa kawaida kunakuwa na mmoja
mwenye kubeba maamuzi ya mwisho juu ya maswala yanayowahusu.

Wenzetu Wadosi(wahindi) Bohora.Mwanamke ndiye mtoa maamuzi ya mwisho. akikataa imetoka.Hata baadhi ya wenzetu waswahili utakuta mwanamke ndiye kinara katika maamuzi!

Mwanamke akijikweza na kukalia kiti kama kichwa cha wanandoa/mahusiano
wengi wao inakuwa ni shida kwa mume na jamii inayomzunguka.

Binafsi napenda mwanaume ashike usukani katika uwajibikaji na kutoa maamuzi.Kama huamini nikisemacho jaribu kakaliwa na mke/mpenzi utajuuutra.

Kuna mdada niliwahi kuwa naye aliniambia katika kila uhusiano aliowahi kuwa nao alikuwa yeye anaamua atakacho.Kumfunga break ilikuwa patashika lakini mwishoni alinyooka kwa mbinde.

So men, chagua mwanamke utakayemmdu,wenye roho za YESEBEL tupa kule.

Wakatawale mifugo.
 
Wanaume tatizo lenu mnarogeka kirahisi.
Kitandani goigoi na maamuzi yenu gougoi
 
Mkuu mbona suala la mwanamke kuwa kichwa cha nyumba halipo hata kwenye vitabu vya dini??
Vitabu vyote vinamtambua mwanamume Kama mkuu wa familia na final say!
Sasa hao wengine waliokaliwa na wake zao ni maf..la!!
 
Wanaume tatizo lenu mnarogeka kirahisi.
Kitandani goigoi na maamuzi yenu gougoi
Tuombe radhi wengine aisee!!
Ugoi goi anao huyo uliyenaye!
Kama huamini Karibu pm kwa mechi moja ya kirafiki!!
 
HADITHI NA SOMO;
Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.

MWL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?

JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.

MWL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?

ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga.

MWL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.
Na wewe Bruno??

BRUNO: mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiwe......"

Akameza mate kisha akaendelea....

"Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali."

MWL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Clara tueleze unataka kuwa nani??

CLARA: Nataka kuwa mke wa BRUNO!!

SOMO;
Wanawake aina ya Clara ni wengi mno, walikuwepo enzi hizo na wanaendelea kuzalishwa kwenye familia zetu, wanaopenda njia za mkato kwenye maisha.

Wengi hushkuru kujikuta wamezaliwa wanawake, wakihisi maisha yatatafutwa na wenzi wao wao watakuwa watumiaji tu. Anajua ataolewa, atawekwa ndani, hataumiza kichwa kuhusu maisha.

Lakini taabu huja baadae baada ya mwanaune kuanguka kimaisha au kufariki. Mwanamke hubaki kuwa mzigo tu, na mwanaume hubaki kuwajibika kama Punda.

Lakini ni kweli katika zama hizi tunahitaji wanawake aina hii?
 
Siongei kishabiki ila mimi, mwanamke kushika usukani kwenye maisha yangu/yetu labda niwe kwenye "comma"... Kumsikiliza nitamsikiliza, kukubaliana au kutokubaliana nae ni juu yangu...
 
Tatizo kubwa ni income inequality, unakuta mama anakipato kikubwa zaidi automatically lazima awe muamuz wa mambo.

Duc in Altum
 
Jinsi nilivyo mbishi nikapata mwanamke wa kunitawala itakua poa
 
Ha ha ha! Eti, roho ya Yezebeli. Dah! Huyo mama ndo alichangia kwa kiasi kikubwa anguko la mfalme AHABU. Mungu atusaidie kufanya machaguo sahihi.
yap! huyohuyo mkuu! Mwanamke.anakuwa na mamlaka ndani ya nyumba na kwenye jamii lazima mjue kuwa yeye ni ncharge! ukikosea hapo hata ndugu/furaha ya.mahusiano yanapotea.
 
HAta mimi sipendi wanaume wanaotawaliwa na wanawake... unaachaje bibie anakutawala mpaka ulimwengu wote tufahamu buanaa.!
Wadada wazuri kama rubii ndo mnaongoza kuwakalia wanaume! wengine anaogopa akikwacha pengo halitazibika,atakosa wa kuuza nae sura Samaki Samaki,Fish market,Escape one etc!
 
Mkuu mbona suala la mwanamke kuwa kichwa cha nyumba halipo hata kwenye vitabu vya dini??
Vitabu vyote vinamtambua mwanamume Kama mkuu wa familia na final say!
Sasa hao wengine waliokaliwa na wake zao ni maf..la!!
Wapo mwanakwetu! vitabu vipo lakini.mahusiano yanaendeshwa bila kanuni,wengine wanaona ndio mahaba niue kumpa mama kila jukumu,yeye anakaa pembeni.
 
HADITHI NA SOMO;
Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.

MWL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?

JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.

MWL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?

ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga.

MWL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.
Na wewe Bruno??

BRUNO: mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiwe......"

Akameza mate kisha akaendelea....

"Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali."

MWL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Clara tueleze unataka kuwa nani??

CLARA: Nataka kuwa mke wa BRUNO!!

SOMO;
Wanawake aina ya Clara ni wengi mno, walikuwepo enzi hizo na wanaendelea kuzalishwa kwenye familia zetu, wanaopenda njia za mkato kwenye maisha.

Wengi hushkuru kujikuta wamezaliwa wanawake, wakihisi maisha yatatafutwa na wenzi wao wao watakuwa watumiaji tu. Anajua ataolewa, atawekwa ndani, hataumiza kichwa kuhusu maisha.

Lakini taabu huja baadae baada ya mwanaune kuanguka kimaisha au kufariki. Mwanamke hubaki kuwa mzigo tu, na mwanaume hubaki kuwajibika kama Punda.

Lakini ni kweli katika zama hizi tunahitaji wanawake aina hii?
zama hizi tunahitaji wanawake wanaowajibika lakini wakipata vipato vikubwa au vinavyolingana nasisi wasipole mamlaka tuliyopewa na Mungu Mwenyezi(sio mungu wa congo yule )
 
Siongei kishabiki ila mimi, mwanamke kushika usukani kwenye maisha yangu/yetu labda niwe kwenye "comma"... Kumsikiliza nitamsikiliza, kukubaliana au kutokubaliana nae ni juu yangu...
Hapo mwingine atasema hapendwi!.lakini bora lawama kuliko kumpa usukani mkaenda polini muishie kuliwa na Ngwena
 
Tatizo kubwa ni income inequality, unakuta mama anakipato kikubwa zaidi automatically lazima awe muamuz wa mambo.

Duc in Altum
kweli na ukitaka kumdhibiti unaweza ishia kupigwa chini! na kila mtu atajua mama ndie mwenye kisu!
 
Back
Top Bottom