Mwanamalundi
JF-Expert Member
- Aug 30, 2007
- 3,126
- 1,439
.......mwanaume zima unashika shika mikoba ya wanawake!! we vipi??? Yalikuwa ni maneno yaliyonichoma barabara moyo wangu tena kutoka kwa mwanamke ninayempenda kuliko wote, yaani mke wangu!!!
Ilikuwa hivi, ametoka kazini akanipitia mimi kazini kwangu tukawa tunajirudisha home taratiibu na stori mwanana za kutaniana hivi na vile bora tumekutana tunaopendana!!!
Ugomvi ulianzia nilipopokea simu ya mfanyakazi mwenzangu akinitaarifu kuwa report niliyotuma, attachment haikwenda ambayo ndiyo report yenyewe!!! So nitume tena na kwa haraka sana coz makao makuu wanaisubiri jioni hiyo hiyo!!! Niliwasha laptop yangu nikakuta ina umeme kidogo sana nilichofanya ni kuibeba kwenye flash na nikalazimika kumuomba mke wangu laptop yake ili niitumie kwa muda huo!!!
Ye wife anatumia mini laptop ambayo inaingia kwenye mkoba wake anaoweka na vitu vingine vya kike, kiukweli sikusubiri jibu lolote toka kwake nikafungua mkoba wake na kutoa min laptop yake nikaiwasha na kuanza kutumia, kumbe mwenzangu muda wote huo hakuniona ila alinielewa kuwa nahitaji laptop yake!!!
Aliposimamisha gari na kunigeukia akakuta natumia tayari, daah!!! Yalimtoka maneno ambayo sijawahi kuyasikia kinywani mwake tangu namfahamu (moja wapo ni hayo niliyotumia kama title aya ya kwanza)!! Alikasirika mwanamke mpaka nikashangaa, sikumjibu kitu kwani nilituma niliyoyatuma nikazima laptop yake nikamrudishia!!!
Katika kudadisi kwangu niligundua yafuatayo;
1. Alikasirika sababu nimefungua mkoba wake, Je wana JF mimi kama mume mtu siruhusiwi kugusa mkoba wa mke wangu na kuufungua??
2. Alikasirika mimi kuwasha laptop yake kwa madai kwamba ile ni kitu binafsi kama ilivyo simu so nilipaswa kusubiri aniwashie!! Wana JF laptop pia ni restricted kwa mume/mke???
Kifupi mie sijaongea nae kitu mpaka sasa coz mihasira mingi na nimejikuta nina mengi yanazunguka kichwani nataka kwanza nitulie ili nilianzisha tuelewane vizuri!!!
Ila bado najiuliza nilikuwa sahihi ama nimekosea??? Wana JF mnaonaje hili????
Nawasilisha
Mdada una maneno ya busara sana.... Basi tu!!!!
Mtoa mada fuata huu ushauri.......
haya matoto ya kike hayaendi,,ni bora kufuga mabata 10 kuliko mwanamke 1..
hahahaahhah unanifahamuje mkuu huo ndio uhalisia jamani khasamahani kuna mtu ametumia id yako na kuchakachua maoni na ushauri akijidai ni wewe ninaekufahamu...ni hayo tu mpendwa
Sisi wanawake ni selfish sana sana ,mfano rahisi utakuta wote mnafanya kazi ila hela itakayotumika ni ya mume tuuu kwa kila kitu home ya kwako niyakuvaa tu soooo selfish .huyo dada ana jambo la ziada lakukuambia juu ya kauli yake .mimilait ningezaliwa mwanaume nsingeruhusu kuchezewa namna hiyo muna thamani kubwa sie viumbe dhaifu na wadogo sana kwenu.mwite kwa sauti mwambie kaa pale explain kila neno ulilolitoa siku ile alaaah unammezea mate ya nini hataki mwambie akapumzike kwao.na at last usipumbazike kingono akiri hayo maneno yake .mwanaume bila udicteta haya matoto ya kike hayaendi,,ni bora kufuga mabata 10 kuliko mwanamke 1.huwa namwambia mume wangu mwanaume lazima uongee kwa sauti ijulikane nibaba ameongea la sivyo hata watoto watakupanda kichwani!!we bana bana pua atakuaibihs hivohivo mbele za watu.
sijakufahamu vizuri wewe ni she au he?Sisi wanawake ni selfish sana sana ,mfano rahisi utakuta wote mnafanya kazi ila hela itakayotumika ni ya mume tuuu kwa kila kitu home ya kwako niyakuvaa tu soooo selfish .huyo dada ana jambo la ziada lakukuambia juu ya kauli yake .mimilait ningezaliwa mwanaume nsingeruhusu kuchezewa namna hiyo muna thamani kubwa sie viumbe dhaifu na wadogo sana kwenu.mwite kwa sauti mwambie kaa pale explain kila neno ulilolitoa siku ile alaaah unammezea mate ya nini hataki mwambie akapumzike kwao.na at last usipumbazike kingono akiri hayo maneno yake .mwanaume bila udicteta haya matoto ya kike hayaendi,,ni bora kufuga mabata 10 kuliko mwanamke 1.huwa namwambia mume wangu mwanaume lazima uongee kwa sauti ijulikane nibaba ameongea la sivyo hata watoto watakupanda kichwani!!we bana bana pua atakuaibihs hivohivo mbele za watu.
sijakufahamu vizuri wewe ni she au he?
kuna siri mbele ya kudhalilishwa viumbe hawa ni hatari sana anaweza kukua kwa pressure ukiangalia hivi hivi,Hizi ni siri zenu. Si jambo jema kuziweka hadharani. Fikiria kama mkeo ni mwana JF, atajisikia vipi akisoma hapa?