Mwanaume Mwenye Bahati Mbaya Kuliko Wote Uinge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanaume Mwenye Bahati Mbaya Kuliko Wote Uinge

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Felixonfellix, Apr 29, 2010.

 1. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Mick akiwa hospitali baada ya ajali mbaya hivi karibuniWednesday, April 14, 2010 9:49 PM
  Mkulima wa nchini Uingereza Mick Wilary ambaye anadaiwa kuwa ndiye mtu mwenye bahati mbaya kuliko wote nchini Uingereza kutokana na ajali kibao zinazomkumba, amepata ajali kwa mara nyingine tena iliyoivunja miguu yake yote miwili.Mick Wilary, mwenye umri wa miaka 58 anadaiwa kuwa ndiye mtu ambaye hana tabasamu kutokana na bahati mbaya zinazomkumba na kumfanya akumbwe na ajali mbaya zinazoyatia maisha yake hatarini.

  Mick ameishakumbwa na ajali mbaya zaidi ya 30 na ajali hizo zimepelekea kuvunjika kwa mifupa ya viungo vyake 15.

  Katika tukio la hivi karibuni, Mick anaendelea kupatiwa matibabu hospitalini baada ya miguu yake kupondwa na tingatinga.

  Katika tukio hilo dereva wa tingatinga akiliendesha tingatinga hilo modeli ya JCB bila ya kuwa mwangalifu, alimgonga Mick na kumbamiza ukutani.

  Katika tukio hilo mguu wa kushoto wa Mick ulivunjika na kupinda kuelekea mabegani wakati mguu wake wa kulia ulijeruhiwa na kugeuka ukiangalia nyuma.

  Hata hivyo pamoja na ajali hiyo mbaya ya kutisha, madaktari katika hospitali ya Newcastle wamefanikiwa kuiokoa miguu yake na wamesema kuwa ndani ya miezi sita Mick ataweza tena kuitumia miguu yake kutembea.

  Ajali ya kuvunjika kwa miguu yake imetokea ikiwa ni miezi michache baada ya kuvunjika kwa enka za miguu yake yote miwili baada ya kuteleza na kuanguka chini alipokanyaga kiazi mviringo.

  Miongoni mwa ajali mbaya zilizowahi kumkumba Mick ni kupasuka kwa fuvu la kichwa chake kwenye sakafu alipopigwa mweleka na paka.

  Mick pia ameishawahi kuvunjika mbavu, shingo na mikono katika mfululizo wa ajali mbaya zinazoendelea kumkumba ambazo zimeifanya sura yake ikose tabasamu wakati wote.
   
 2. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Duh.Mkuu endelea kutupa NEWS bin News..duh kumbe kunawatu wana pata mikasa kwa namna ya kipekee kabisa..hii inasikitisha sana..duh Namuombea kwa Mola Apone haraka na Aepushwe na ajari mbaya tena...AMINA..
   
 3. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  ANAHITAJI DAMU YA MWANAKONDOO.....! mmmh
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kweli jamaa ana bahati mbaya. mara kakanyaga kiazi, mara paka.
  ila apunguze uoga, inawezekana ni muoga kupita kiasi ndo maana anapata ajli mara kwa mara.
   
 5. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,010
  Trophy Points: 280
  Duh hii kali. Mbona mi naona kama ndie mwanamume mwenye bahati kuliko wote Uingereza? Maana mtu huputa ajali mara moja tu na kukumbana na mauti bali huyu mara 30 na bado anaendelea kutafuna mema ya nchi? Ni bahati iliyo je.
   
Loading...