Mwanaume Muoaji ana sifa zifuatazo...

Mwanaume Muoaji ana sifa zifuatazo...

Money Penny

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2016
Posts
18,204
Reaction score
17,561
Hapa ndio wabongo wengi wanafeli hasa akina Dada ambao hamjaolewa

Ukinichukia Sawa ukiniita old school Sawa maana hapa Nina Miaka 63, nawasaidia Kupunguza malalamiko ya wanaume

Kihalali kabisa na hata ukiuliza walioolewa wenye ndoa za Amani watakwambia kuwa:

Mwanaume MUOAJI, anaetafuta MKE hawezi kukufanyia haya yafuatayo:
1. Kukupiga denda hadharani

2. Kukukumbatia hadharani

3. Kukushika ziwa au Chuchu hadharani

4. Kukushika wowowo hadharani

5.Kuzini na wewe kabla hajakuoa

6. Mahusiano yenu yatakuwa ya muda mfupi Sana, sio zaidi ya Miezi 3

7. Hatokuonyesha Mali zake au fahari ya vitu vya kuonekana kwako kabla hajakuoa

8. Hatokuita usiku usiku sijui mkatembee atahakikisha mitoko yenu ni mchana, penye watu wengi na mwisho kukaa nae itakuwa SAA 12 jioni

Sasa kama wewe bwana ulienae hafanyi haya, ujue unamsindikiza tu kipindi hiki cha Covid19 au unamsindikiza kumpata MKE wake Halali🙈

Mwenye sikio na asikie, nipo hapa namalizia maombi ya siku 3 ya kuombea Taifa letu dhidi ya CORONA 🙏

Mnakaribishwa wanaume kuchangia pia huenda kuna Mengi nimesahau
 
Back
Top Bottom