Mwanaume mkimya (si muongeaji) Vs mwanaume mcheshi ( muongeaji)

Mwanaume mkimya (si muongeaji) Vs mwanaume mcheshi ( muongeaji)

Lara1 wewe tu bora upate mkimya mana ukipata muongeaji kama mbwiga wa clouds fm heheeeee sipati picha ya mtoto atakaezaliwa, nahisi mtoto atakuwa kama subwoofer.heheee mana lara ukianza zile falsafa zako khaaaaaa!
Mkimya! Mwanaume mkimya ndo mpango mzima, i kind of ind it Sexy! Controversial! Undefined! Cool and Reserved.

You cant tell what he is thinking, you will always be guessing. Pia mkigombana ananyamaza tu unatoa single za rap na rnb ikibidi hata country yeye anakuangalia tu machoni hatii neno!

Afu wanakuaga more of actions. TALK IS CHEAP!!!!!!!!!!
 
Nahisi kama wachangiaji wengi wanachanganya madesa. Kuna tofauti kubwa sana ya UKIMYA,UCHESHI,UPOLE na UONGEAJI na KUPUMBAA.Mtu anaweza akawa mpole ila asiwe mkimya, anaweza akawa mpole ila mcheshi. Wapo pia waongeaji ila ni wa pole.si kila mkimya ni mpole na si kila mpole ni mkimya. Pia si kila mcheshi ni muongeaji. Pia tutofautishe UPOLE na KUPUMBAA. Upole ukizidi kupitiliza mtu huonekana kama amepumbaa hivi. Ama upole wa kawaida huweza kuambatana na ucheshi/ukimya au hata uongeaji.
Ni asilimia ngapi ya wadada humu wanawachagua manaume wakimya si waongeaji na wangapi wanawachagua wanaume wacheshi waongeji.
kama choice zao na kwa nini?
 
raha sana! wamseme hata anaringa ili nimfaidi mwenyew. lol... ila mwanaume anaeongea ongea hovyo wanaboa. .. nimemsoma huyo wako wa airport. yaani mtu hamjuani ila atajieleza utafikir yupo kwenye chumba cha interview.
Umenichekesha sana yaani mtu aongee utadhani yuko kwenye chumba cha interview lkn kweli wapo waongeaje wa namna hii.
 
Kwa kweli kila kitu kinatakiwa kiwe kwa kiasi. Kuna wengine waongeaji sana lkn wanaongea point na wanachangamsha mno na kuna wengine si waongeaji sana lkn akiongea lazima aongee pumba. Sasa integemea historia ya mtu kwani haya yote mtu hajifunzi bali hujikuta yuko hivyo. Sipati picha hiyo nyumba itakavyokua kama mama na baba wote watakua wakimya.
 
Mcheshi mzee wa chai ....yupo gudume... Huyo huko nadhani mtaendana. Ila ukitaka mkimya njoo kwangu tu.
 
Nilikutana na dada mmoja hivi nikamtokea...tobaaa kumbe dada mwenyewe kipusa...yani dk mbili tu keshanitambulisha kwa marafkizake...nusu saa nishajua tabia zake ..kilichifata nilibadilisha njia nisikutane nae maana ningemgonga ingekuwa kero..asiwe muongeaji kupita kiasi
 
Vp wagomvi siku hizi hamtupendi!? Maana kipindi mnazivunja ungo mlitupenda sana kule mashuleni
 
Mpole huwa wanamimambo makubwa sana huwa wasiri pia na muongeaji huwa mrahisi kumsoma tabia
 
Simpendi mpòle huwa wanasuprise events tofauti na muonekano wao
 
Raha ya kuwa mpole ukitongoza madem hawakatai wanakuonea huruma
Na wewe kama ndio unajua kutia huruma basi ni mchekea tu
Balaa ni pale
Ni pale wamekaa wadada wanapiga stori
Mwisho wa siku wanajikuta hamna uliyem bakiza wote ushasuuza
 
Nilikutana na jamaa mmoja airport Dar kaanza tu from nowhere kuniongelesha wakati tuko kwenye foleni ya kukaguliwa pass. kwa muda mfupi nilimjua nje ndani...nilichowaza cha kwanza asije nipa begi nimshikie anaenda washroom akanibebesha unga....anaongea pumba tupu; kuanzia stori za mai wife wake, story za kukana uraia wake...alivyo na mke wa kizungu, hapo ni ndani ya kama dk 10 tu. Nikajitahidi kujifanya sina interest na kama simsikii vile waaapiii. Mpaka majirani walikuwa wanamshangaa...maana alikuwa anaropoka kwa sauti...nadhani alitaka kila mtu amsikie kama si kumkoma.Lol. sasa huyu naye ni mume wa mtu. Kha.

Imagine mme wa mtu mxxxxm
 
Sisi wakimya ni watu hatari sana
Nakuunga mkono ndugu yangu
dfaa21591e742e6f88ba2ec93884a878.jpg
 
Nakuunga mkono 200% wengi ni wakimyaa ila gusa... Uwiii utajuta...
Unaweza ukagusa pia anaweza kukuachia ....ukiona amekubadilikia sana ujue umeutumia ukimya na upole wake kwa kumchukulia poa sanaaa hivyo anataka kukuonyesha na yeye huwa sio wa polepole
 
Back
Top Bottom