Mwanaume kuzaa nje ya ndoa

Mwanaume kuzaa nje ya ndoa

Naomba kukujibu kwa uelewa wangu

(1) mahusiano yanaweza kuendelea kutokana na mazoea mlokuwa nayo na uyo mtoto ambae tayari ni kiunganishi

(2) mapenzi ni lazima yatapungua tena mwanamke hatoweza kukuamini tena sababu usaliti wenye kidhibitisho huumiza sana na hali hiyo inaweza kumbadili ata matendo yake akatafuta na yeye kipoozeo cha hayo maumivu kwa fikra kwamba uyo binti ulozaa naye tayari umehamishia mapenzi kwake.

(3) Apo kwenye kuivunja ndoa itategemeana una mjali kiasi gani, namaanisha kama umeongeza mapenzi zaidi tofauti na mwazo kwa mwanamke ni vigumu kutengana ila ukileta ubabe sababu ya uanaume wa kuzaa nje ya ndoa basi utadaiwa talaka usiku na mchana
Hiyo namba mbili itakuwa ni tabia yake tu.
 
Uvumilivu huu ndio unafanya watu wafe kwa presha! Jirani yetu hapa tumemzika mkewe hivyohivyo yeye amejenga nyumba mbili halafu ealikua na mgogoro na mkewe akamtambishia mkewe kuwa zile nyumba anaenda kumuandikishawanamke mwenzake! Yule dada presha ikapanda alipofikishwa muhimbili tu akafariki dunia! Inategemea kila inshu mtu anaipokeaje! Sasa hlo ni suala la nyumba je ingekua mtoto wa nje sijui ingekuwaje
Kwahili tukio huwezi generalize.
 
Kwa kweli ni bora niolewe tu na single daddy, maana mtoto nimemkuta na nikakubali kwa hiari yangu kuwa ntakuwa mama yake, nikaamua mwenyewe nipende boga na ua lake. Kuliko mtu aniletee mtoto wa nje ndani ya ndoa. Mungu aniepushe na kikombe hicho, maana heeeeeeeee
Mtoto wa nje ya ndoa anatokea wakati mke hajazaa?! Unaweza kuwa umeolewa na umeshazaa na ukaletewa mtoto. Mwanamke aliyeachika kuolewa ni bahati sana labda kama alikuwa anacheat na huyo jamaa.
 
Mtoto wa nje ya ndoa anatokea wakati mke hajazaa?! Unaweza kuwa umeolewa na umeshazaa na ukaletewa mtoto. Mwanamke aliyeachika kuolewa ni bahati sana labda kama alikuwa anacheat na huyo jamaa.
Wanaachika na wanaolewa vizuri tu. Na hata wasipoolewa tena sidhani kama ndo itakuwa mwisho wa maisha yao
 
Tatizo ndoa zetu hizi za kikristu hazivunjiki hadi kifo. . . Ningevumilia ila upendo na uaminifu kwa mume wangu ungepungua

Ila kama ni uislam taraka fasta
nani kakwambia ndoa za kikristo hazivunjiki wewe.......utaishije na mtu kushakuwa kama jini shetani?....zinavunjika sana tuu
 
Habari zenu wakuu,

Naombeni kuuliza, hasa wanawake wanaweza kuwa katika position nzuri sana. Inapotokea mume wako umemkuta na mtoto, ukakubali akakuoa na mkafanikiwa katika ndoa kupata nae mtoto mmoja. Lakini ikatokea huyo mume wako akazaa na binti mwingine tena nje ya ndoa.
1. Utaweza kuendelea na relationship hiyo?
2. Kama utaendelea, je unaweza kuwa na kiwango kile kile cha mapenzi kama mwanzo?
3. Je, unaweza ukatamani kuvunja ndoa ila kwa sababu wewe ni mwanamke ukashindwa? Au utaendelea kwa sababu ya neno "uvumilivu"

Nawasilisha.
Utafiti: Asilimia kubwa ya wanaume wanalea watoto wasio wao.

Mbona sisi hatuna ngebe tunalea watoto mliozalia nyumbani kwetu?? sembuse sisi tunaozalisha nje huko??

Hebu punguzeni wivu, acheni tuwape wanawake wenzenu haki yao.
 
Mbona hao hao wanawake wanabeba ujauzito wa nje ya ndoa japo mnalala kitanda kimoja;
halafu watoto wenyewe wanakuwa na akili sana;
Ndo hapo naposhangaa...

Najiuliza kinachowauma ni kuzaa nje au kunjunji nje??

Anaweza akatokea mwanaume mmoja akazaa na mwanamke mmoja wa nje, na akatokea mwingine akalamba wanawake wa nje zaidi ya mia bila kuwazalisha... Nani mwenye afadhali???
 
wee una wasiwasi gani bwana...ulishamzalisha hana jipya na wala hana soko tena. so hamna shida wewe jigegedee tuu
Hivi mnadhan mkituzalisha ndo hatuwez endelea na maisha? Kwamba hatutapendwa ama? Acheni kujidanganya.
 
Ni kweli ila hapo lazima mwanaume ajutie kosa na akuambie kila analolifanya kule .. ila me kwa mama ilikuwa rahisi sababu baba alichukua mtoto na kumpeleka kwa dada yake na akawa anaishi huko mpaka sasa hivi majukumu na matumizi ya mtoto dada yake baba anasema na mama mtu kumuona mtoto anaenda huko kwa anti.. nadhani ni makubaliano yao ili kuondoa sintofahamu. Muhimu upendo ukiwa nayo Hayo huwezi revenge
Miss Chagga, hiyo reference umefanya ukimaanisha baba alizaa kabla ya kumwoa mama au wakiwa kwenye ndoa?
 
Miss Chagga, hiyo reference umefanya ukimaanisha baba alizaa kabla ya kumwoa mama au wakiwa kwenye ndoa?
akiwa kwenye ndoa na huyo mtoto kapishana miezi mitatu na mdogo wangu wa tatu .. yani mama akiwa mjamzito miezi mitatu mzee kapiga nje na mimba hiyo
 
akiwa kwenye ndoa na huyo mtoto kapishana miezi mitatu na mdogo wangu wa tatu .. yani mama akiwa mjamzito miezi mitatu mzee kapiga nje na mimba hiyo
Duh, hapo kuna kazi. Kwa mbali naona upungufu wa upendo ktk moyo wangu. Maana naona ishara ya dharau tayari. Anyway mi naacha, naanza maisha yangu upya na wana'ngu.
Ni ngumu kumeza, it's better kama huyo mtoto amezaliwa kabla cjafahamiana na mume wangu.
 
Ukifikiria unakuwa upo sawa na mawazo yako, yakikukuta ni tofauti. miss chagga yupo sahihi na ndiyo ukweli wa kimaisha ingawa kovu haliondoki moyoni
 
ndoa ni mambo mengi yanawaunganisha ila ukitanguliza swala la tendo tu lazima umweke pembeni .. ila me kama mimi nitaangalia uchumi tuliojenga wote nimuachie mtu mwingine nooo nitapambana sababu hata nikienda kuishi na mwanamgu huko haimaanishi ile dhrau imeisha no.. nitapambana to hell kulinda uchumi wetu na kuweka mapambano zaidi kupata zaidi.. na pia watoto napenda wanangu waishi na baba yao ...
 
Ukifikiria unakuwa upo sawa na mawazo yako, yakikukuta ni tofauti. miss chagga yupo sahihi na ndiyo ukweli wa kimaisha ingawa kovu haliondoki moyoni
Hilo kovu ndo linaloniuma sana. Halafu we n ke au me? Kama ni me bas geuza kichwa cha mada ili uwe mtendewa ndo utaelewa hisia zangu.
 
Tatizo ndoa zetu hizi za kikristu hazivunjiki hadi kifo. . . Ningevumilia ila upendo na uaminifu kwa mume wangu ungepungua

Ila kama ni uislam taraka fasta
Hakuna ndoa isiyo na TALAKA, kuna mstari kwenye Biblia unaelezea kuhusu talaka,pale Mume au Mke inapojulikana ni mziinifu basi Talaka inaruhusiwa
 
Hilo kovu ndo linaloniuma sana. Halafu we n ke au me? Kama ni me bas geuza kichwa cha mada ili uwe mtendewa ndo utaelewa hisia zangu.
Mimi ni Me na nilishamkamata redhanded mke wangu jamaa linamfaidi ila bado ninaye. Kabla sijambamba alikuwa akinitesa ila baada ya kumfumania cha moto anakipata ingawa kovu haliwezi kutoka. Una la ziada kuniuliza?
 
Hakuna ndoa isiyo na TALAKA, kuna mstari kwenye Biblia unaelezea kuhusu talaka,pale Mume au Mke inapojulikana ni mziinifu basi Talaka inaruhusiwa
Talaka lazima uipime ndugu yangu. Ukichambua faida na hasara za kukaa naye ukapata upande wa kukaa naye upo juu ya talaka. Unakubali yaishe ili maisha yaendelee (rejea namba 137)
 
Mimi ni Me na nilishamkamata redhanded mke wangu jamaa linamfaidi ila bado ninaye. Kabla sijambamba alikuwa akinitesa ila baada ya kumfumania cha moto anakipata ingawa kovu haliwezi kutoka. Una la ziada kuniuliza?
"Cha moto anakipata".... Hcho ndo kinanifanya nishindwe kuishi kiivyo
 
"Cha moto anakipata".... Hcho ndo kinanifanya nishindwe kuishi kiivyo
Hapo wewe mzani wako utakuwa umeegemea hasara za kuishi naye. Wengi wenu hasa wanawake wanacheat kama kukomoa au kulipa kisasi. Ukimbamba anapima mzani na kugundua ulivyo wa maana kwake atabaki tu ila kila nyendo unaiangalia na yeye atajitahidi kukuonyesha kuwa ameacha hatorudia, maisha yanasonga mnangojea chumba chenye kuta nne.
 
Back
Top Bottom