Mwanaume Kuvaa Kanga...

Mwanaume Kuvaa Kanga...

Mkuu sio kwa ubaya ni kwa Mapenzi na hua napenda kumuona amevaa kanga sio avae kivuani anavaa kama vile Kikoi..

Huyo ni mwanaume. Sasa kama unapenda kumuona hivyo, basi hata mtoto wenu wa kiume naye utamwambia avae tu, halafu badae utaona kitakachotokea.
Kuna vitu hupaswi kabisa kumwambia mumeo. Tena shukuru huyo anakwambia Kwa maneno, wengine utachezea makofi ya kutosha.
 
Cku waenda kumtembelea mshkaji wako mara pap wamkuta kavaa sare ya dera au khanga imeandikwa ...nampa papa
Mkuu unajua wanaume wa sikuizi tuu mbona zamani wazee wetu wanavaa? mfano my Dad akiwa nyumbani anavaa kikoi na flana ata vaa kanzu kama kuna mgeni,sasa huyu wangu mie Lahaullah,hanielewi kabisaaaaaaaaaaaa..
 
Huyo ni mwanaume. Sasa kama unapenda kumuona hivyo, basi hata mtoto wenu wa kiume naye utamwambia avae tu, halafu badae utaona kitakachotokea.
Kuna vitu hupaswi kabisa kumwambia mumeo. Tena shukuru huyo anakwambia Kwa maneno, wengine utachezea makofi ya kutosha.
Mkuu nadhani hujanielewa,kikoi unakijua? if yes kuna tofauti gani baina ya kikoi na kanga?
 
Duh! Yaan unafananisha kikoi na kanga?
Ngoja nikuache kama ulivyo. Endelea kumshawishi, ipo siku atakubali.
 
Mkuu unajua wanaume wa sikuizi tuu mbona zamani wazee wetu wanavaa? mfano my Dad akiwa nyumbani anavaa kikoi na flana ata vaa kanzu kama kuna mgeni,sasa huyu wangu mie Lahaullah,hanielewi kabisaaaaaaaaaaaa..
Sio akuelewi kumbuka nivigumu xnaa mwanaume kuvaa mavazi ya kike tofaut na nyie mnaweza vaa mavazi ya kiume
 
Mkuu wala usitoa povu,sikua na maana mbaya baada ya kuva kikoi avae kanga kwani si sawa na kikoi tuu au?
Haviwezi kuwa sawa,ni sawa na ulinganishe baibui na kanzu kwa kuwa vyote vina mikono mirefu.
Au ziwa na bahari kwa kuwa vyote vinaweza beba meli.
 
Sio akuelewi kumbuka nivigumu xnaa mwanaume kuvaa mavazi ya kike tofaut na nyie mnaweza vaa mavazi ya kiume
Mkuu sijawambia avae atoke njee,na sio kwamba kikoi havai ila baada ya kuvaa kiko why asivae kanga?
 
Back
Top Bottom