Mwanaume kuiomba airtime voucher!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanaume kuiomba airtime voucher!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by sweetdada, Mar 23, 2011.

 1. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Wanandugu wapendwa hope mu wazima..

  Hee!!nimeshangazwa na kitenndo cha mwanaume mmoja eti ananisumbua kwa muda wa mwezi kwa madai ananipenda..sasa cha kushangaza na ambacho sielewi..kila akipiga simu ataongea dakika tano afu ananambia"please call me back credit inaisha"...
  hee!!mi nabaki kutoa macho huyu vipi??na mi namwambia hata mie yangu imeisha basi nikisema hivyo anaendelea kuongea..
  cha kuchekesha leo asubuhi kanipigia tena simu kaongea mwisho akasema "nitumie vocha ya 2000 basi"..hee!!mi nikabaki mdomo wazi,nikamwambia sina hela..akakata simu.

  Jamani nimeshangaa ajabu sijawahi kuona dunia nzima mwanaume anakuwa hivi especially akiwa anatongoza..huyu hata kama anataka kunifanya mie 'kitonga' si angesubiri basi akubaliwe..akaaa!!kani put off mnooo na kaniharibia siku yangu ya leo ..mxiiiiiii

  Wanaume ndo mnaenda wapi kwa hii style jamani aii
   
 2. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Ngoja nikae kimya kwa thatha, ila nitarudi na nashukuru kwa kunifanya nianze na tabasamu siku ya leo
   
 3. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Umekutana na Sharobaro huyo dada maana mmmhh vocher ya 2000 kazi unayo
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  :lol::lol::lol: Kumbe inawauma na nyie kuombwa vocha basi mkae mkijua kuwa na sisi huwa inatu-put off nyie kutuomba vocha every now and then, sweetdada leo imekula kwako acha kubana mtumie mshikaji vocha banaa mbona nyie mkituomba huwa tunawatumia halafu mnaishia kutu-beep:lol::lol::lol:
   
 5. CPU

  CPU JF Gold Member

  #5
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Namba za sim mlipeana vipi??
  Mnajuana au hamjuani???
   
 6. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  ....ushaambiwa ndo wako stage ya kutongozana unapouliza wanajuana au hawajuani una maanisha nini shem (LZ)?kujuana ndo kupi?:juggle:
   
 7. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  ni mfanyakazi mwenzangu so tunafahamiana na namba za simu kwa wafanyakazi humu kwetu kupeana its normal kwa wajili ya kikazi zaidi.sasa mwenzangu badala ya kuitumia kikazi akaamua kuitumia kibinafsi zaidi
   
 8. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  You said it all The Finest....Nimefurahi kusikia kuwa hata wadada nao wanaboreka wakiombwa 'vocha' au wakimbiwa naishiwa credit call me back! Inatuboa pia inapotokea mara kwa mara. Inaboa zaidi ukituma hiyo vocho pengine buku 2, then unaambulia msg ya ahsante tu, next time you hear from her its either a beep, tafadhali nipigie, au mzinga mwingine wa vocha!
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Inaonyesha wewe mchunaji sana.

  Kwani ungempunguzia 300/= kuna ubaya gani?

  Siku hizi mapenzi kusaidiana bana
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kama mfanyakazi mwenzako kwa nn umeamua kumzalilisha?

  Sio vizuri kuwa mstaarabu yaani kuombwa vocha imekuuma hivyo ukimpa je?
   
 11. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Fidel, umeshasema "mapenzi kusaidiana"..mi sina mapenzi nae,yeye ndo ananitongoza..sasa iweje uniombe nikucall au vocha wakati hata sijakukubali,je nikikukubali si utaomba mahela mpaka nikome..akaa!hebu nielewe na wewe..au na wewe ndo walewale 'KITONGA'
   
 12. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #12
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Hahahahahahahah lol
  kweli bongo kuna vituko
  Mchore chini huyo
  Hana mbele wala nyuma
  Wanawake tunapenda kudekezwa
  Tena ile mara ya kwanza mtu anapokutongoza

  Huyo kijana alitakiwa akuletee kanga,akupeleke nje kwa dinner,
  Na ye ndo akupe vocher

  Khaa nani anataka mtu wa mamna hiyo
  Angesubiri mpaka umwite mpenzi
  Ndo angeanza hayo mambo..

  Hembu mweleze ukweli

  Na asikukatishe tamaa kwani wanaume wengi
  hawako hivyo kabisa..
  mwingine ataenda ku kopa fedha ili akufurahishe

  Embu achana na hiyo michosho
  u deserve better girl...
   
 13. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kumdhalilisha vipi sasa?kwani mfanyakazi mtongozaji ndo ana haki ya kuomba vocha?
  angekuwa mshkaji sawa ningeona kawaida,ila siku zoote tuko kama strangers ni hi hi
  kumbe mwenzangu anakufa kisabuni ,akaamua kuvunja ukimya
  sasa ndo uniombe nikupigie na vocha juu!!
  Hivi kuna mtu ananielewa kweli?au wote mnaona namfanyia mbaya????????
   
 14. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Riwa they should know it works both ways sasa hapo sweetdada apige hesabu wanaume tunapoombwa vocha tena sio 2000 huwa wanasema 5000 sijui ampigie mama anaumwa kumbe changa la macho next time she will beep you telling you kwamba imeisha anaomba umtumie nyingine kumbe changa la macho:lol::lol:
   
 15. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #15
  Mar 23, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Amtumie vocha bwana, dah vocha tu tena ya 2000 l.o.l
   
 16. semango

  semango JF-Expert Member

  #16
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mkuu umemaliza habari yote.ma she wanapenda sana haki sawa kwenye vitamu tu lakini haki sawa kwenye majukumu ina wa-put off.hapo jamaa hajafanya cha ajabu.anajaribu kudumisha haki sawa.credit yake kapiga na mmeongea kwa dakika tano so inakua zamu yako na wewe kuwezesha mawasiliana coz kama mnaweza kuongea for 5 minutes then ni ushahidi tosha kua hata wewe huwa unaonesha kuenjoy mazungumzo.so kama unaenjoy mazungumzo, cha ajabu ni kipi kuombwa kuchangia kuwezesha mazungumzo yaendelee?
   
 17. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #17
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Well said, thank you afrodenzi..sasa baton ya senks ndo siioni.finally i got someone who supports me.:wink2:
   
 18. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #18
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Inawezekana wewe ni boss wake huko ofisini,anajua una hela nyingi na labda umemuonyesha unampenda sana na anataka umlee kama mwanae sasa......ha ha ha ha ha.......its a turn off for real,mimi kusema wewe tu hii story nimehisi kutapika....sijui wewe uliyeambiwa....
  kama unampenda ongea nae mwambie hupendi,kama huna feelings nae mpotezee!!:washing:
   
 19. RR

  RR JF-Expert Member

  #19
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Acha ubali SD...sio umpatie hiyo buku mbili ili akupendage zaidi?
   
 20. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #20
  Mar 23, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Sasa si bado anakutongoza bado kidogo utaingia kingi

  Jamaa akichanga fresh point zake utaingia king na mtaanza kubenjuka
   
Loading...