Saint_Mwakyoma
JF-Expert Member
- Jun 8, 2019
- 867
- 1,216
Anatuvuruga mkuu
Mwanaume unaanzaje kukimbia changamoto?
Kukimbia na kurudi, utaishi hivyo kwa muda gani?
Ukikimbia usipopata ndiyo jumla unawatelekeza?
Nini maana ya kuwa kichwa cha familia?
Aliyesema mwanaume lazima awe nacho muda wote ni nani?
Ulioa ili muishi katika raha tu na ikifika wakati wa karaha mkimbiane?
Unaishije na mtu hawezi kuelewa kuna kupanda na kushuka katika maisha?
Unaishije na mtu anaye kuonyesha kujali wakati ukiwa nazo tu, na usipokuwa nazo hakujali? Huoni unatumika?
Unakubalije kuwa mtumwa wa mtu mwingine?
Humu kuna vijana wadogo wanaposoma thread kama hizi ile spirit ya kuwa mwanaume mwenye kuyakabili majukumu inapungua wakiamini mambo yakiwa magumu wakimbie na siyo kupambana kutafuta suluhisho.
Na SIVYO mwanaume anavyopaswa kuwa.
Uliamua kuyavulia nguo, YAOGE mzee.




