Mwanaume kamili, unakuaje mmbea aisee?

Mwanaume kamili, unakuaje mmbea aisee?

mzee wa kasumba

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
1,440
Reaction score
2,963
Hii fani waachieni wadada tena wa uswahilini.

Nimempa mwana habari zangu za kasumba, usiku akaenda kumhadithia mke wake, mke wake akazitawanya kwa mashoga zake. Sasa ziko wazi.

Leo nimemchana mwana, mwana sio mwana wala nini. Bora Kama una Mambo yako ufe nayo tu mwenyewe. Nailaumu nafsi yangu kumuamini mwana.
 
Hahah Pole sana. Hapo mbea ni mke wa jamaa. Juu ya kiuno kuna balaa zake.

Samson alinyolewa hivi hivi akiona huku anagugumia utam plus hasira akijua nguvu zake ndio kwishney.
 
Usikute mke wa jamaa nae kawapigia mashoga zake kuwachana kuwa hawajatunza siri na hao marafiki wa huyo mke wa jamaa na wenyewe wamewapigia simu mashoga zao kuwachana kwa kutoa siri..
Kiufupi wanaiga utakachofanya..😅
 
Usikute mke wa jamaa nae kawapigia mashoga zake kuwachana kuwa hawajatunza siri na hao marafiki wa huyo mke wa jamaa na wenyewe wamewapigia simu mashoga zao kuwachana kwa kutoa siri..
Kiufupi wanaiga utakachofanya..
 
Ukiwajua watu walivyo, Hutawai kumwelezea mtu jambo lako, Waone Hivyo hivyo
 
Ila hakuna watu wanaosema watu kama wanandoa waliona amani kwenye ndoa yao...ukimpa siri yako mmoja wao kuna kitu kinamuwasha tu amwambie mwenzie wakiwa wanapiga story....ila ni baadhi sio woote
Mkuu mimi hii nimeiona kwa wanaume wengi sana,sijui mwanaume akitoa siri za wana kwa mkewe ndo anajisafisha....utasikia Juma ana michepuko mitatu na mtoto wa nje anamwambia mkewe na mkewe anawaambia mashoga zake ni upuuzi tu
 
Ukitaka kuona mwana anafeli mpe story za uongo uongo utashangaa kuja kuzisikia mtaani hahah afu unacheka tu huku unawaona wajinga
 
Siri yako ni yako mwenyewe akishiriki mwingine si siri tena

@bima_lee.orchestra

Waliimba hao ndugu miaka ileee ulikuwa wapi wewe?
 
Sasa wewe mwenyewe umeshindwa kutunza siri yako halafu mwana unataka akutunzie ajabu hii.
 
Ila hakuna watu wanaosema watu kama wanandoa waliona amani kwenye ndoa yao...ukimpa siri yako mmoja wao kuna kitu kinamuwasha tu amwambie mwenzie wakiwa wanapiga story....ila ni baadhi sio woote
Hahaha mkuu umesema kweli, wife akipata ishu yyte akifika tu lazima animwagie, yan hakai na kitu nikiwepo lazima aniambie dah
 
Pole sana lakini hakuna watu wanapiga umbea na kusengenya watu kama mtu na mkewe hata umbea wa ma best friend unapigwa hapo...kama kuna mengine ulikua unamwambia hujayasikia ni vile hayakukufikia tu. Wanaume mjue tu wake wa rafiki zenu wanawachekea lakini wanawachora mno kwa mengi
 
Back
Top Bottom